Watu wa fani ya ushushushu wanasema wana hisia sita hivi hiyo ya sita ni ipi?

Duh. Ushetani+usalama wa taifa is related to sixth sense?

Mbona tofauti sana na ninavyojua mimi?
kuna sense za kishetani. nilishawahi kuwa na mwanamke ambaye mkilala naye guest chumba hiki, tukio la ajabu likitokea chumba cha tatu kwenye guest hiyohiyo anaelewa kinachoendelea, kama ni hatari, kama ni salama, etc. tulilala siku moja mchana, kumbe chumba kama cha nne ndani ya lodge ileile, kuna mwanaume alikuja na mwanamke kwa nia ya kuja kumuulia mle ndani. wakati amempiga kabali, yule dem aliniambia chumba fulani kuna tukio baya linatendeka......tukatoka nje, kukaa kidogo kumbe yule dada akapata mwanya wa kutoa walau sauti, ikatoka kwa nguvu na sisi tumekaa nje, jamaa alikuwa anataka kumuua. alitoka nduki akasingizia kuna mtu ndani amewavamia, wakati tunashangaa ameshazunguka nje alikokuwa amepaki amesepa. hatujachukua namba ya gari, hatujafanya lolote, na hatujui alielekea wapi hata kabla hatujapiga simu polisi, hatuzijui mji ule sisi wageni na wahudumu nao walikuwa wamelala kwani mchana hakuna wateja sana. nikamuuliza kulikoni uligundua kitu wewe haupo kule, akanisimulia mengi sana. actually bibi yake ni mganga wa kienyeji kumbe na alishataka kumrithisha, ana mashetani ndani yake.

nilikaa naye kama mwaka, duh, kumbe mashetani huwa yanahamia kwa mtu bwana. ndo maana ukilala na mwanamke mwingine kama ana mikosi unaondoka nayo, kama ana mashetani unaondoka nayo pia. mimi pia nikawa na hisia za ajabu, tukio ambalo litatokea kesho, kama ni zuri au baya, nalijua leo. mwanzoni niliona poa sana kwasababu yale niliyoota kwenye ndoto jana, au pengine nilikuwa nayahisi/fikiri kichwani yanakuja kama yalivyo. nilikuja kugundua kumbe nina mashetani hadi nilipoombewa yakafumuka na kuongea mambo ya ajabu.

hao wanausalama wengine, hasa hao wanaosafirik wenye misafara ya wakubwa, kama wanaenda mwanza leo, jana yake wameshajua everything kitakachotokea kesho kule mwanza, wanajua ktk ulimwengu wa roho. kama kuna adui anajiandaa, everything. na wanatoa makafara makubwa sana kulisha mashetani yanayowapa hiyo huduma. usije kuweka mtego wa kumdhuru rais au kiongozi wa juu wa kiafrica (labda wazungu) ukafikiri hawatagundua. unapoteza muda.
 
Ni bora ungesema unachojua kuliko muda ulioupoteza hapo kwa faida ya wengine
Okay. Ukiachilia mbali 5 common senses ambazo ni kusikia, kuona, kunusa, sense ya ngozi na kugusa hii sixth sense inakuwa unazaliwa nayo.

Inahusu hisia, naifananisha na instinct sema its deeper.
 
hivi mleta mada umewahi kukutana na MTU ambae anajua kusoma binadamu na mazingira? kabla hata hujasema chochote... ukiongea ndo anakufunga kabisa!
MTU ambae akifika kwenye mazingira anajua nini kilikuwepo, nini kinaendelea, na nini kinakuja!

kuna watu hawana maono Ila wana utambuzi wa hali ya juu, na ufahamu wa binadamu na mazingira kuliko MTU wa kawaida.( mama angu Mimi mwenyewe yuko hivo, hadanganyiki, anaweza kukupa unachohitaji kabla hujasema, anajua ulipo kabla hujamwambia anajua shida zako za ndani bila kumweleza, anaweza kusolve tatizo lako LA kifikra bila kumshirikisha, ni mshauri mzuri pia)
nahisi hicho ndiyo no.6 yao! japo sina uhakika
 
Ukiwa na roho mtakatifu utajua mengi sana kama mimi kama sehemu hatari hujua na nikimwambia mtu kitu kinatokea
Kiukweli kuna watu wanajua huyu mtu hatari mfano ukitaka kumjua binadamu macho yake ni muhimu kwa kuwa ni mlango wa roho
 
hivi mleta mada umewahi kukutana na MTU ambae anajua kusoma binadamu na mazingira? kabla hata hujasema chochote... ukiongea ndo anakufunga kabisa!
MTU ambae akifika kwenye mazingira anajua nini kilikuwepo, nini kinaendelea, na nini kinakuja!

kuna watu hawana maono Ila wana utambuzi wa hali ya juu, na ufahamu wa binadamu na mazingira kuliko MTU wa kawaida.( mama angu Mimi mwenyewe yuko hivo, hadanganyiki, anaweza kukupa unachohitaji kabla hujasema, anajua ulipo kabla hujamwambia anajua shida zako za ndani bila kumweleza, anaweza kusolve tatizo lako LA kifikra bila kumshirikisha, ni mshauri mzuri pia)
nahisi hicho ndiyo no.6 yao! japo sina uhakika
Ongea na mama yako basi nimletee mwanangu Amfunze awe na uwezo huo.
 
Mlango Wa sita no HISI.

Humfanya MTU aweze kubashiri kinachotaka kufanywa na MTU mwingine
Au
Kujua MTU anawaza nini kwa muda huo

Mbashiri anaweza kupatia sawia au kukosea kabisa.

Kilingana na kiwango chake cha HISI

Mfano ni magolikipa wakati Wa penalties wapo wanao weza kumsoma mpigaji na wakadaka penati
Hata 3 kati ya tano
Na wapo ambao hata moja hawawezi kuzuia

Kiimani kuna mambo mawili

1. Imani ya kimungu(Roho)

2.Imani ya nguvu za Giza (shetani)

HISI nguvu humuwezesha MTU kujua kitakachotoke aidha kizuri au kibaya au kumuona MTU mwingine katika nia yake ya dhati

Hapa wapo wale wanazuiliwa kusafiri, kupita baadhi ya njia , kugoma kula baadhi ya vyakula nk............

Yote kwa yote ni lazima uwe na kalama ya kuomba kwa dhati ya moyo kwa God au gods
 
Mbona watu wengi mnaitaja ila mnashindwa kutambua!!! Hiyo ya sita ni 'HISIA' hiyo ndio kitu ambacho wanakitumia, wanatafsiri maneno, matendo, mwenendo wako wa maisha na mashirikiano na watu mbalimbali na mengine kama hayo ndio yanayomfanya apate hiyo common sense ya sita, mfano unaweza kuwa na mtoto nyumbani kwako kama zamani alikua anarudi nyumbani pengine tuseme kabla ya saa 2 usiku akianza kurudi saa 4 au tano usiku utahisi kuna kitu kimebadilika kwake hivo utaanza kujiuliza na ktafakari nini kimetokea ili upate tafsiri ya yeye kurudi usiku huo
 
hivi mleta mada umewahi kukutana na MTU ambae anajua kusoma binadamu na mazingira? kabla hata hujasema chochote... ukiongea ndo anakufunga kabisa!
MTU ambae akifika kwenye mazingira anajua nini kilikuwepo, nini kinaendelea, na nini kinakuja!

kuna watu hawana maono Ila wana utambuzi wa hali ya juu, na ufahamu wa binadamu na mazingira kuliko MTU wa kawaida.( mama angu Mimi mwenyewe yuko hivo, hadanganyiki, anaweza kukupa unachohitaji kabla hujasema, anajua ulipo kabla hujamwambia anajua shida zako za ndani bila kumweleza, anaweza kusolve tatizo lako LA kifikra bila kumshirikisha, ni mshauri mzuri pia)
nahisi hicho ndiyo no.6 yao! japo sina uhakika
Inshort mama yako ni Usalama
 
Binadamu yeyote anavitu viwili vinavyomwongoza
1 Milango ya fahamu ambayo iko mi 5 hz zina deal na mambo ya utambuzi

2 Body sensitivity ambazo zipo 3

Kila binadamu ana body sensitivity 3 ila wanausalama wanakwenda kusomea zingine tatu ndo inakuja kuwa 6 kwani unatakiwa kujua duniani kuna aina tatu za elimu
1 Elimu ya kidini
2 Elimu ya kidunia hii ndio tunafundishwa mashuleni
3 Elimu ya utambuzi elimu hii wanafundishwa watu wachache ambao wanakuwa trained kwa ajili ya kudeal na watu wenye elimu hzo mbili yani ya dini na kidunia

Sasa bhasi tusiongee mengi sanaaa labda nikutajie kuanzia hisia ya 4 mpka 6 kwa ufupi

4 Ni uwezo wa kumsoma mtu kwa sura yake
kwa kumwangalia tu tutakubaliana ya kuwa sura inaongea sura inaweza elezea kila kitu kinachotokea ndani ya mwili wako mfano furaha,huzuni,shauku,hofu,jazba na kukata tamaa

5 Ni uwezo wa kumsoma mtu kupitia moyo wake hapa napenda kuwaelezea kidogo na kuwapa mfano juu ya usomaji wa moyo mtu aliyeiva ktk maswala ya ujasusi anauwezo mkubwa wa kujua ata anapomtongoza mwanamke anajua atajibu nini au anawaza nini kihisia juu yake kwan lipo somo maalumu kwa ajiri ya wanawake ktk tasinia ya ujasusi inamtambua mwanamke kama ni silaha ya maangamizi ( Weapons of Mass Distraction)

6 Ni uwezo wa kumsoma mtu ndani ya ubongo pia tunatakiwa kujua ubongo ndio command center ya mwili wa kila mwanadamu command zote zinatoka ndani ya ubongo na ukiweza kufuzu vizuri somo ili ambazo pass mark zake ni 70% utakuwa unawezo mkubwa sana wa mambo wa ujasusi
Nadhani hiki kitu ndo haswa wanacho jifunza hawa watu
 
hivi mleta mada umewahi kukutana na MTU ambae anajua kusoma binadamu na mazingira? kabla hata hujasema chochote... ukiongea ndo anakufunga kabisa!
MTU ambae akifika kwenye mazingira anajua nini kilikuwepo, nini kinaendelea, na nini kinakuja!

kuna watu hawana maono Ila wana utambuzi wa hali ya juu, na ufahamu wa binadamu na mazingira kuliko MTU wa kawaida.( mama angu Mimi mwenyewe yuko hivo, hadanganyiki, anaweza kukupa unachohitaji kabla hujasema, anajua ulipo kabla hujamwambia anajua shida zako za ndani bila kumweleza, anaweza kusolve tatizo lako LA kifikra bila kumshirikisha, ni mshauri mzuri pia)
nahisi hicho ndiyo no.6 yao! japo sina uhakika
Mmh atakuwa na madude aiseeh
 
Back
Top Bottom