Watu wa fani ya ushushushu wanasema wana hisia sita hivi hiyo ya sita ni ipi?

kanonb

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
372
500
Habari wana jamvi

Ni tumaini langu kuwa mko wazima kabisa (kwa namna pekee napenda kutoa pongezi kwa team nzima ya Jamii Forum kwa kazi kubwa wanayoifanya bila kuchoshwa na mitazamo ya watu as we all know) lakini nilikuwa na swali ambalo limekuwa likinisumbua sana hususani kwenye hii issue ya intelligence wanasema mtu huwa ana hisia tano yaani kuona, kuonja, kusikia,kunusa,kuhisi kwa kutumia ngozi.

Lakini hawa watu wa fani ya ushushushu wanasema wana hisia sita hivi hiyo ya sita ni ipi???
 
Habibu B. Anga

Verified Member
May 7, 2013
6,568
2,000
Kama ukiongelea masuala ya kiroho, Yes kuna "sixth sense" au yafaa kusema wako wanao amini kuna sxith sense..

Katika ulimwengu wa kawaida hakuna sixth sense katika namna ambayo unatafsiri..

Wanaposema sixth sense ni vile wanatumia lugha, kujaribu kuelezea uwezo mkubwa wa kuelewa, kupambanua, kuchambua, na kufikiri tofauti na mtu wa kawaida..

Wapo wanaozaliwa na uwezo huu wa hali ya juu kufanya hayo lakini pia unaweza kujifunza kuwa na uwezo huo..

Ndio kusema sio kwamba maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wote wamezaliwa "Super humans", hapana.. Wengi wao uwezo wao wa kufikiri ni kama mimi na wewe tu bali wanachokuzidi ni kwamba wamefundwa namna ya kuitumia akili yao ya kawaida waliyo nayo kudevelope "sixth sense"..
 
Juma chief

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
2,657

umenifilisi wazo mkuu....
means kwamba wenye sixth sense ya kuzaliwa ni wachache,ila wengi wanafundwa......

tuletee uzi basi wa kujifunda na hiyo hisia ya 6..

una ualimu flani hivi wa intell,aidha umefundwa au kujifunda....
 
Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,475
2,000
yani uweze kumshuku mtu(mmoja tu) kwamba amekuja kwa ajili ya kumuuwa VIP tena nadani ya umati mkubwa wa atu na kweli mkimlaza chini na kumpekua mumkute na silaha ziwezazo kudhuru

hiyo ndio wanasema mlango wa sita kwa wana usalama
 
Habibu B. Anga

Verified Member
May 7, 2013
6,568
2,000
yani uweze kumshuku mtu(mmoja tu) kwamba amekuja kwa ajili ya kumuuwa VIP tena nadani ya umati mkubwa wa atu na kweli mkimlaza chini na kumpekua mumkute na silaha ziwezazo kudhuru

hiyo ndio wanasema mlango wa sita kwa wana usalama
Yes, umetoa mfano mzuri sana Mkuu..

Ila jambo unalotakiwa kufahamu ambalo nahisi wengi hawalijui au hawalifahamu ni kwamba.. Mfano huo mfano ulioutoa kuwa Afisa Usalama anamspot mtu mmoja kuwa ni hatari katika kundi la watu elfu.. Unapaswa kujua sio kwamba Afisa huyu ana uwezo wa kimiujiza (sixth sense) kwa namna ambayo naona watu wanaamini na kujiaminisha..

Maafisa wote Usalama wanafundishwa kitu kinaitwa "Micro expressions"
Hivi ni viashiria vidogo vidogo sana katika mjongeo wa mwili (body language) na Usoni (facial expression).. Viashiria hivi vidogo vidogo vinamuwezesha Afisa kung'amua dhamira ya muhusika..

Ni somo refu!
 
asante kwa maelezo mazuri
Infantry Soldier pita huku
 
qurious

Senior Member
Jan 13, 2012
134
225
Yes, umetoa mfano mzuri sana Mkuu..

Ila jambo unalotakiwa kufahamu ambalo nahisi wengi hawalijui au hawalifahamu ni kwamba.. Mfano huo mfano ulioutoa kuwa Afisa Usalama anamspot mtu mmoja kuwa ni hatari katika kundi la watu elfu.. Unapaswa kujua sio kwamba Afisa huyu ana uwezo wa kimiujiza (sixth sense) kwa namna ambayo naona watu wanaamini na kujiaminisha..

Maafisa wote Usalama wanafundishwa kitu kinaitwa "Micro expressions"
Hivi ni viashiria vidogo vidogo sana katika mjongeo wa mwili (body language) na Usoni (facial expression).. Viashiria hivi vidogo vidogo vinamuwezesha Afisa kung'amua dhamira ya muhusika..

Ni somo refu!
Tupe somo mkuu coz unakarama ya uandishi uliotukuka
 
maalimu shewedy

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
860
1,000
Ha ha ha, muda sana sijakutana na hili neno.

Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa ni mtu wa so sana, sasa ikitokea mko naye kijiweni anaweza akawaambia mi natoka kidogo, hazipiti hata dakika kumi polisi wanatia timu kijiweni kumtafuta jamaa, ila ndo wanakuta alishatimua.
 
MarkHilary

JF-Expert Member
Feb 8, 2015
1,515
2,000
Kama ukiongelea masuala ya kiroho, Yes kuna "sixth sense" au yafaa kusema wako wanao amini kuna sxith sense..

Katika ulimwengu wa kawaida hakuna sixth sense katika namna ambayo unatafsiri..

Wanaposema sixth sense ni vile wanatumia lugha, kujaribu kuelezea uwezo mkubwa wa kuelewa, kupambanua, kuchambua, na kufikiri tofauti na mtu wa kawaida..

Wapo wanaozaliwa na uwezo huu wa hali ya juu kufanya hayo lakini pia unaweza kujifunza kuwa na uwezo huo..

Ndio kusema sio kwamba maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wote wamezaliwa "Super humans", hapana.. Wengi wao uwezo wao wa kufikiri ni kama mimi na wewe tu bali wanachokuzidi ni kwamba wamefundwa namna ya kuitumia akili yao ya kawaida waliyo nayo kudevelope "sixth sense"..
Madam,kwa mfano TISS wanapendelea sana watu wacha Mungu. Niliuliza nikaambiwa hawa pamoja na nidhamu ya hali ya juu waliyo nayo ambayo ni miongoni mwa misingi ya kazi hiyo, ni rahisi kufikia sixth sense kuliko aliye mbali na mambo ya dini

Naipenda sana hiyo kazi basi tu!
 
izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,814
2,000
Binadamu yeyote anavitu viwili vinavyomwongoza
1 Milango ya fahamu ambayo iko mi 5 hz zina deal na mambo ya utambuzi

2 Body sensitivity ambazo zipo 3

Kila binadamu ana body sensitivity 3 ila wanausalama wanakwenda kusomea zingine tatu ndo inakuja kuwa 6 kwani unatakiwa kujua duniani kuna aina tatu za elimu
1 Elimu ya kidini
2 Elimu ya kidunia hii ndio tunafundishwa mashuleni
3 Elimu ya utambuzi elimu hii wanafundishwa watu wachache ambao wanakuwa trained kwa ajili ya kudeal na watu wenye elimu hzo mbili yani ya dini na kidunia

Sasa bhasi tusiongee mengi sanaaa labda nikutajie kuanzia hisia ya 4 mpka 6 kwa ufupi

4 Ni uwezo wa kumsoma mtu kwa sura yake
kwa kumwangalia tu tutakubaliana ya kuwa sura inaongea sura inaweza elezea kila kitu kinachotokea ndani ya mwili wako mfano furaha,huzuni,shauku,hofu,jazba na kukata tamaa

5 Ni uwezo wa kumsoma mtu kupitia moyo wake hapa napenda kuwaelezea kidogo na kuwapa mfano juu ya usomaji wa moyo mtu aliyeiva ktk maswala ya ujasusi anauwezo mkubwa wa kujua ata anapomtongoza mwanamke anajua atajibu nini au anawaza nini kihisia juu yake kwan lipo somo maalumu kwa ajiri ya wanawake ktk tasinia ya ujasusi inamtambua mwanamke kama ni silaha ya maangamizi ( Weapons of Mass Distraction)

6 Ni uwezo wa kumsoma mtu ndani ya ubongo pia tunatakiwa kujua ubongo ndio command center ya mwili wa kila mwanadamu command zote zinatoka ndani ya ubongo na ukiweza kufuzu vizuri somo ili ambazo pass mark zake ni 70% utakuwa unawezo mkubwa sana wa mambo wa ujasusi
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
26,006
2,000
Kama ukiongelea masuala ya kiroho, Yes kuna "sixth sense" au yafaa kusema wako wanao amini kuna sxith sense..

Katika ulimwengu wa kawaida hakuna sixth sense katika namna ambayo unatafsiri..

Wanaposema sixth sense ni vile wanatumia lugha, kujaribu kuelezea uwezo mkubwa wa kuelewa, kupambanua, kuchambua, na kufikiri tofauti na mtu wa kawaida..

Wapo wanaozaliwa na uwezo huu wa hali ya juu kufanya hayo lakini pia unaweza kujifunza kuwa na uwezo huo..

Ndio kusema sio kwamba maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wote wamezaliwa "Super humans", hapana.. Wengi wao uwezo wao wa kufikiri ni kama mimi na wewe tu bali wanachokuzidi ni kwamba wamefundwa namna ya kuitumia akili yao ya kawaida waliyo nayo kudevelope "sixth sense"..
Huu uwezo si ndio ule uliniuliza kama nimeshanufaika nao ama bado?
 
kanonb

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
372
500
Madam,kwa mfano TISS wanapendelea sana watu wacha Mungu. Niliuliza nikaambiwa hawa pamoja na nidhamu ya hali ya juu waliyo nayo ambayo ni miongoni mwa misingi ya kazi hiyo, ni rahisi kufikia sixth sense kuliko aliye mbali na mambo ya dini

Naipenda sana hiyo kazi basi tu!
Mhh!!! Inashangaza???? kufikia hisia ya sita na mambo ya kidini
 
Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,548
2,000
Ha ha ha, muda sana sijakutana na hili neno.

Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa ni mtu wa so sana, sasa ikitokea mko naye kijiweni anaweza akawaambia mi natoka kidogo, hazipiti hata dakika kumi polisi wanatia timu kijiweni kumtafuta jamaa, ila ndo wanakuta alishatimua.
kuna sense za kishetani. nilishawahi kuwa na mwanamke ambaye mkilala naye guest chumba hiki, tukio la ajabu likitokea chumba cha tatu kwenye guest hiyohiyo anaelewa kinachoendelea, kama ni hatari, kama ni salama, etc. tulilala siku moja mchana, kumbe chumba kama cha nne ndani ya lodge ileile, kuna mwanaume alikuja na mwanamke kwa nia ya kuja kumuulia mle ndani. wakati amempiga kabali, yule dem aliniambia chumba fulani kuna tukio baya linatendeka......tukatoka nje, kukaa kidogo kumbe yule dada akapata mwanya wa kutoa walau sauti, ikatoka kwa nguvu na sisi tumekaa nje, jamaa alikuwa anataka kumuua. alitoka nduki akasingizia kuna mtu ndani amewavamia, wakati tunashangaa ameshazunguka nje alikokuwa amepaki amesepa. hatujachukua namba ya gari, hatujafanya lolote, na hatujui alielekea wapi hata kabla hatujapiga simu polisi, hatuzijui mji ule sisi wageni na wahudumu nao walikuwa wamelala kwani mchana hakuna wateja sana. nikamuuliza kulikoni uligundua kitu wewe haupo kule, akanisimulia mengi sana. actually bibi yake ni mganga wa kienyeji kumbe na alishataka kumrithisha, ana mashetani ndani yake.

nilikaa naye kama mwaka, duh, kumbe mashetani huwa yanahamia kwa mtu bwana. ndo maana ukilala na mwanamke mwingine kama ana mikosi unaondoka nayo, kama ana mashetani unaondoka nayo pia. mimi pia nikawa na hisia za ajabu, tukio ambalo litatokea kesho, kama ni zuri au baya, nalijua leo. mwanzoni niliona poa sana kwasababu yale niliyoota kwenye ndoto jana, au pengine nilikuwa nayahisi/fikiri kichwani yanakuja kama yalivyo. nilikuja kugundua kumbe nina mashetani hadi nilipoombewa yakafumuka na kuongea mambo ya ajabu.

hao wanausalama wengine, hasa hao wanaosafirik wenye misafara ya wakubwa, kama wanaenda mwanza leo, jana yake wameshajua everything kitakachotokea kesho kule mwanza, wanajua ktk ulimwengu wa roho. kama kuna adui anajiandaa, everything. na wanatoa makafara makubwa sana kulisha mashetani yanayowapa hiyo huduma. usije kuweka mtego wa kumdhuru rais au kiongozi wa juu wa kiafrica (labda wazungu) ukafikiri hawatagundua. unapoteza muda.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom