Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

Watu wa Dar es Salaam muache hii tabia, mnakera

Du! rohombaya mkuu

Mkuu ukilegea sana utakuwa na wageni hata 10 kwa siku, matokeo yake utapoteza mda wako wa kutafuta. Isitoshe kama ni mawasiliano ya kawaida tu hata simu inatosha sana, si lazima kuonana uso kwa uso. Cha ajabu nchi za wenzetu walioendelea kuonana na mtu lazima kufanya appointment, tena kuonana kwao ni kimaslahi zaidi, si mambo ya ujomba, undugu na blabla
 
Hahahaha,aisee nimecheka kweli mpaka nimeona muda swaumu uongezeke.

We ukitaka muambie kwamba una kipande cha madini ya dhahabu ndio ujue kwamba watu wa Dar ni wakarimu saana.

Unajua wengie huwa wakija huko Mikoani masifa meengi,ila sio siri nyumba tunazoishi Dar baadhi yetu ndi kiwako,yaani unaona hadi aibu kumualika ndugu yako aje kutembea.Lakini tukikutana nje aaa unafikiria nakaa Masaki vile.

Hapo hapoa Dar tu kuna watu wanakutana kwenye misiba na harusi tuu,lakini makwao hawatembeleani,kila mmoja anamuimbisha mwenzie Songi.
 
KIONGOZI ni kama ulikuwa nami moyoni,binafsi nimeishi Dar kwa miaka 10 nikisoma na kufanya kazi,nimekuwa nikiwathamini sana ndugu na jamaa wanaokuja wakitokea mikoani.Ni miaka minne sasa nipo nje ya Dar,ajabu ninapokwenda huwa natamani kuwaona jamaa na marafiki,ninapowapigia simu wengi wao wanakuwa na majibu hayo hayo!!...SIJUI NI UGONJWA GANI HUU?..Mara nipo bize,mara tuonane kesho,mara nitakupigia baadae,mara simu hazipokelewi,mara nipo katika foleni,mara....daaah!!ISIWE TAABU Nafahamu wengi wao ni HOFU ya kuonekana wamechoka ama kuogopa kumkarimu mgeni wa Mikoani.Nakupongeza rafiki yangu Tall (Tabata Kimanga) na Fulgence wa Mwanagati kwa kutokuwa na tabia hiyo!!!

hahahahahhahahah mkuu pole sana naona umetoa ya moyoni
 
Next ni diaspora....

Hawa watu wanachekesha sana....wakiwa mikoani wanaleta porojo kuonyesha watu wa Dar wamechoka huko walipo ndio kuzuri!!! Wakifika dar wanajaribu tena kuonyesha huko ughaibuni si lolote mambo yote hapa!!

Wewe umekuja dar kwa shughuli zako ukiona mtu anakuzingua ni kwamba hataki kuonana na wewe ila hawezi kukwambia. sasa sababu yeye kukataa kuonana na wewe huwezi kuijua ila kwasababu ya akili za kimasikini conclusion ni kuwa anakukimbia kwa sababu kachoka. kwanini isiwe the other way round anakukimbia labda anaona utampiga mizinga??!!
 
Hahahaha,aisee nimecheka kweli mpaka nimeona muda swaumu uongezeke.

We ukitaka muambie kwamba una kipande cha madini ya dhahabu ndio ujue kwamba watu wa Dar ni wakarimu saana.

Unajua wengie huwa wakija huko Mikoani masifa meengi,ila sio siri nyumba tunazoishi Dar baadhi yetu ndi kiwako,yaani unaona hadi aibu kumualika ndugu yako aje kutembea.Lakini tukikutana nje aaa unafikiria nakaa Masaki vile.

Hapo hapoa Dar tu kuna watu wanakutana kwenye misiba na harusi tuu,lakini makwao hawatembeleani,kila mmoja anamuimbisha mwenzie Songi.

mkuu pole na swaumu...mimi nampigia msela simu tukutane mahali tupate mbili tatu syori za hapa na pale siku iende wala sitaki kwenda kwake bado ananizungusha
 
Mimi nakaa Kibaha lakini nikifika mkoa najifanya mtu wa Dar. Si mibia hiyo ya ofa, si totoz hizo, hivi wanawake wa mkoa wanafikiri nanihii za wanaume wa Dar ziko torfauth na za mkoa/ mbona wanatupapatikia sana ? Au ni kwa sababu watu wa Dar wakihonga kima cha chini ni laki kama nitoavyo mimi.
 
karibu tena Dar kaka ukifika usiache kunitafuta mkuu
 
Tatizo unatafuta watu siku za kazi...
Mvizie Jumapili
 
Kama sisi tunaotokea MWANZA ukishamwambia nimekuja na samaki, dagaa, mahindi na jiani nitapitia mkaa andaa kabisa usafiri.
Utaanza kupigiwa saa 10jioni mumefika wapi?

Sasa ufike hapo hauna kitu, utasikia ngoja nimucheki huyu jamaa wa usafiri-jumla
 
Back
Top Bottom