Watu, Taasisi, na Mifumo...

Watu, Taasisi, na Mifumo...

Japo kuna uhutaji wa katiba mpya, suala hili nchi hii lipo kisiasa sana. Sehemu kubwa ya push ya katiba ni kwa ajili ya upinzani wapate madaraka wala sio nia ya dhati ya kusaidia taifa.

Ndio maana wananchi wa kawaida hata hawasukumi hayo mabadiliko yafanyike.

..wapinzani wanataka katiba mpya ili waingie ikulu?

..ccm wanang'ang'ania katiba mbovu ili wasitoke ikulu?
 
Yote kweli ila wananchi (ukiondoa wanasiasa) wanataka nini?

..wanasiasa nao ni sehemu ya wananchi.

..kwa hiyo inahitajika katiba inayotoa HAKI SAWA kwa vyama vyote vya siasa.

..wengine wasiohitaji chochote kwenye katiba waachwe waendelee na maisha yao.
 
Hapa ndiyo kuna tatizo kubwa kwa Africa ambalo Barack Obama aliliona alipohutubia Bunge la Ghana mwaka 2009 na akasema "Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions."
Ukiwa na strongman akifa na mambo yake YANAKUFA. Lakini Strong Institutions hata Rais akifa zenyewe zinabakia.

Mfano wa strong institutions ni Katiba ya Wananchi, Tume Huru ya Uchaguzi, Mahakama Huru na Bunge Huru. Vile vile TISS inayolinda masilahi ya nchi na siyo ya Rais, Jeshi, Polisi na Magereza.

Kwa Afrika nchi zenye Strong institutions ni Afrika Kusini, Kenya, Egypt.

Maguvu ya Magufuli yalisababisha Bunge liwe butu, Mahakama iwe imamuogopa yeye. Maguvu yakamfanya ajenge kiwanja cha ndege kijijini kwake na kumteua mtoto wa Dada yake Dotto James kuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali
Hakuna institutions bila watu!

Institution siyo mashine.

Watu ndo wanatengeneza hizo strong institutions.

Mabadiliko ya kifikra ni ya lazima. Hayaepukiki.

Huwezi kuwa na katiba nzuri, katiba ya ‘wananchi’, bila ya watu kuiandika, kuifuata, kuilinda, kuihifadhi, na kuitetea.

Unaweza kuwa na katiba mpya, ambayo ni nzuri kabisa, lakini huifuati, huilindi, huitetei, na kadhalika.

Hakuna tume huru ya uchaguzi inayojiendesha yenyewe.

Hakuna bunge wala mahakama zinazojiendesha zenyewe.

Na ukitaka mabadiliko ya kweli kwenye hizo taasisi, basi ni lazima pia ubadilike kifikra.

Hakuna mabadiliko yoyote yale ya maana pasipo na mabadiliko ya kifikra.

Mindset lazima ibadilike. Matendo nayo lazima yabadilike.

Ukibadili katiba na ukaacha kubadili fikra, hutoenda popote.

Utaishia kukwama pale pale ulipo.
 
Hayo maneno ya motivesheni spika tu, katiba mpya ndio mpango mzima.

Jamaa baada ya kuona muda wa kukaa madarakan kwa mujibu wa katiba umekwisha akatumia ushawish wake kuondoa ukomo wa kukaa madarakan km katiba inavyoelekeza ili aendeleze mapambano na km mungu akimjaalia uhai miaka michache ijayo atatimiza miongo miwili na yupo mstar wa mbele kupigania katiba mpya ya jamhur,najiuliza atajisikiaje ikiwa Bi Mkubwa akituletea katiba mpya km tunavyotaka lkn akakopi kipengele cha ukomo wa kukaa madarakan km katiba ya cdm inavyojitanabaisha???
 
Hakuna institutions bila watu!

Institution siyo mashine.

Watu ndo wanatengeneza hizo strong institutions.

Mabadiliko ya kifikra ni ya lazima. Hayaepukiki.

Huwezi kuwa na katiba nzuri, katiba ya ‘wananchi’, bila ya watu kuiandika, kuifuata, kuilinda, kuihifadhi, na kuitetea.

Unaweza kuwa na katiba mpya, ambayo ni nzuri kabisa, lakini huifuati, huilindi, huitetei, na kadhalika.

Hakuna tume huru ya uchaguzi inayojiendesha yenyewe.

Hakuna bunge wala mahakama zinazojiendesha zenyewe.

Na ukitaka mabadiliko ya kweli kwenye hizo taasisi, basi ni lazima pia ubadilike kifikra.

Hakuna mabadiliko yoyote yale ya maana pasipo na mabadiliko ya kifikra.

Mindset lazima ibadilike. Matendo nayo lazima yabadilike.

Ukibadili katiba na ukaacha kubadili fikra, hutoenda popote.

Utaishia kukwama pale pale ulipo.
Kwa hiyo Katiba ya South Africa unadhani inaheshimiwa kwa sababu ya mindset za watu au sababu ya institutions imara ambazo ni mazao ya Katiba?
 
Nyumbu hawawezi kukuelewa, wanakomalia mfumo huku wao wamemkumbatia Mbowe
Hapa mbona CCM ndiyo hawawezi kuelewa? Alichoandika mwanzisha mada ndicho kina Mbowe wanapigania. Utapunguzaje nguvu za madaraka ya rais bila kubadili katiba? Utabadilishaji mawazo ya watu bila kubadili sheria na kanuni za na namna uchaguzi unavyoendeshwa ili watu wasione tena kama vyeo ni ''kuula''?
 
That’s a defeatist attitude that I don’t subscribe to.
Fikra kama hizo zako ni ushahidi mwingine kuwa tunahitaji mabadiliko ya kifikra kwanza kabla ya kubadili hayo mengine.

Hukujifunza chochote toka kwenye Orange Revolution huko Ukraine?

Hukujifunza chochote toka kwenye Arab Spring?
Umeelezea vizuri sana. Lakini bila kwanza mabadiliko ya katiba mabadiliko ya fikra hayawezi kuja, au yatakuja baada ya muda mrefu sana. Kama ulivyosema tatizo kubwa la Tanzania ni wananchi karibu wote kuona kuwa kuwa kiongozi ni ''kuula''. Si hilo tu ila uongozi wa kisiasa unachukuliwa kama certificate ya kufanya chochote kwa wananchi. Kwa kifupi maono yetu kuhusu uongozi ni nini bado ni yale ya zamani wakati wa Watemi, Wamangi nk. Leo kuna waziri wa Afya wa Uingereza amelazika kujiuzu kwa sababu ya kumbusu mwanamke wake wakati kuna social distancing rule. Hebu fikiria ingekuwa Bongo! All in all namna tunavyowapata viongozi na katiba kwa ujumla vibadilike ili kusukuma watu wabadilike mawazo
 
Mangi, unarudi kulekule kwenye hoja yangu.

Tukitaka mabadiliko ya kweli basi lazima tubadili na mindset.

Hatuwezi kupata mabadiliko tunayoyatamani, kama tukiendelea na hizi mindset za kikondoo!!!

Huko ilikowezekana, nao ni binadamu tu kama sisi.

Tukiamua tunaweza.

We just need to get over that fear factor.
Ndugu,
Labda turudi nyuma kidogo.
Kati ya kuku na yai nani alitangulia? Au basi nani anafaa kutangulia? Nani ndio amlete mwingine?
Kwa hapa tulipo yafaa tuanze na katiba bora.
Hii itatuwezesha kujenga misingi imara kufuta madhaifu yaliyopo na hatimae mifumo bora ya uendeshaji wa nchi na taifa bora.
 
Hapa ndiyo kuna tatizo kubwa kwa Africa ambalo Barack Obama aliliona alipohutubia Bunge la Ghana mwaka 2009 na akasema "Africa doesn't need strongmen, it needs strong institutions."
Ukiwa na strongman akifa na mambo yake YANAKUFA. Lakini Strong Institutions hata Rais akifa zenyewe zinabakia.

Mfano wa strong institutions ni Katiba ya Wananchi, Tume Huru ya Uchaguzi, Mahakama Huru na Bunge Huru. Vile vile TISS inayolinda masilahi ya nchi na siyo ya Rais, Jeshi, Polisi na Magereza.

Kwa Afrika nchi zenye Strong institutions ni Afrika Kusini, Kenya, Egypt.

Maguvu ya Magufuli yalisababisha Bunge liwe butu, Mahakama iwe imamuogopa yeye. Maguvu yakamfanya ajenge kiwanja cha ndege kijijini kwake na kumteua mtoto wa Dada yake Dotto James kuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali
Amen
 
Umeelezea vizuri sana. Lakini bila kwanza mabadiliko ya katiba mabadiliko ya fikra hayawezi kuja, au yatakuja baada ya muda mrefu sana. Kama ulivyosema tatizo kubwa la Tanzania ni wananchi karibu wote kuona kuwa kuwa kiongozi ni ''kuula''. Si hilo tu ila uongozi wa kisiasa unachukuliwa kama certificate ya kufanya chochote kwa wananchi. Kwa kifupi maono yetu kuhusu uongozi ni nini bado ni yale ya zamani wakati wa Watemi, Wamangi nk. Leo kuna waziri wa Afya wa Uingereza amelazika kujiuzu kwa sababu ya kumbusu mwanamke wake wakati kuna social distancing rule. Hebu fikiria ingekuwa Bongo! All in all namna tunavyowapata viongozi na katiba kwa ujumla vibadilike ili kusukuma watu wabadilike mawazo
Akina Ndugai wanajiwekea 'kinga' ili wasiwajibike kwa matendo yao maovu. Sasa wanafanya vioja na kukejeli wananchi kila uchao. Ni miungu watu.
 
Mambo ya msingi umeongea NN, lakini kubadilika kifikra si mbadala wa katiba mpya, tupate katiba mpya, mengine yafuate.

Yawezekana katiba mpya isitusaidie "sana" lakini hii ya sasa ndio haitusaidii "kabisa". Imagine watu wenye kinga ya kutokushitakiwa ni wangapi? Ikipatikana katiba mpya iliyoondolewa hicho kipengele hata mimi na wewe tunaweza kufile mashitaka, ile tu viongozi fulani fulani wakiona wanaweza kushitakiwa hata kama ni miungu watu kiasi gani wataanza polepole kubadilika kifikra.

Kubadilika kifikra ni process ndefu, katiba ni process fupi, Katiba ikiwa bora itasaidia kushape fikra za watu (si kwa asilimia zote).
Cc Nyani Ngabu
 
Ndugu,
Labda turudi nyuma kidogo.
Kati ya kuku na yai nani alitangulia? Au basi nani anafaa kutangulia? Nani ndio amlete mwingine?
Kwa hapa tulipo yafaa tuanze na katiba bora.
Hii itatuwezesha kujenga misingi imara kufuta madhaifu yaliyopo na hatimae mifumo bora ya uendeshaji wa nchi na taifa bora.
Yote yanaweza kwenda sambamba.

Mabadiliko ya kifikra huchukua muda. Pengine hata vizazi na vizazi.

Licha ya hivyo, mabadiliko ya kifikra bado ni ya lazima.

Hatuwezi kuwa taifa tunalotaka na kutamani kuwa bila kubadilika kifikra.

Imagine tuna katiba mpya. Inakiukwa lakini hakuna la maana tunalofanya na wakiukaji wanaendelea kukiuka bila hofu yoyote ile.

Change of mindset is a must. No two ways about it. No way around it.
 
Back
Top Bottom