Watu, Taasisi, na Mifumo...

Watu, Taasisi, na Mifumo...

Kabisa. We should not tolerate any belittling of our elected leadership, particularly the President.
 
Man naona hii mada uliyoileta hapa ni wachache sana wamekuelewa nini unajaribu kuwahabarisha.

Zaidi utagundua tu kwamba watu wamekariri mambo bila kuwa na uelewa nayo,na hiyo ndio shida kubwa inayotukabili.

Kwamba wao wanaamini tukishakuwa tu na 'katiba mpya ya wananchi' basi kila kitu kitajiendea smoothly regardless of anything else.


Leo hii ukijaribu kuwaambia kuwa tunaweza kuwa Taifa lenye mafanikio na maendeleo makubwa hata kama tutakuwa na katiba mbovu zaidi ya hii, ila cha msingi tuwe na jamii inayojitambua,isiyo na nidhamu ya woga,yenye fikra sahihi na mitazamo sahihi,lazima watakuona wewe CHIZI.


Wamekariri katiba mpya na Taasisi imara,sasa sijui hivyo vitu vitakuja kusimamaiwa na malaika kutoka mbinguni au watu hawa hawa wenye akili kama hizi?
Popote ulipo agiza kreti zima la Heineken!

Umenielewa vizuri sana.

Sina cha kuongeza.
 
Mwendazake aendelee kwenda asigeuke nyuma
Michango kama hii kwenye mada muhimu na nzito kama hii inaonesha umuhimu wa kuanza kubadili mindset za watanzania kabla ya mambo mengine.

Nyani Ngabu yupo sahihi.

Unakomaa na habari za kumshambulia mtu aliyekufa na kuzikwa!!!
 
Mwisho wa siku sisi watu, wananchi, ndo tunawajibika.

Kwa nini tumwachie mtu mmoja awe juu ya katiba?

Sisi wananchi tuko wengi sana, wengi mno kuliko Rais. Rais ni mtu mmoja tu.

Tukiamua, Rais hawezi kutufanya chochote kile.

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki hata iweje, endapo kweli tunataka mabadiliko.
 
Huyu mpuuzi alitoa kauli hii kwa sababu alijua fika katiba ya chama kimoja wanaweza kuidharau bila wao kuathirika kwa vyovyoye vile. Watatumia polisiccm kupiga, kutia vilema, kubambikia kesi ná hata kuua bila wao kuathirika kwa namna yoyote ile na pia kutumia Tume FEKI ya uchaguzi kuiba uchaguzi nchi nzima bila wao kuathirika vyovyoye vile, lakini tukiwa na Katiba mpya ambayo itakuwa na vipengele vyenye kutoa adhabu kubwa kwa wote wataokiuka Katiba mpya na pia Tume huru ya uchaguzi ambayo haitakubali kuchezewa hata na Rais ili kuchagua uchaguzi basi maneno haya ya KIPUMBAVU asingethubutu kuyatoa. Mahali pa kuanzia ni Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi




Mifumo ni watu. Taasisi ni watu. Na vyote hivyo ni kwa ajili ya watu.


Hakuna mfumo uliojiumba wenyewe tu na unaojiendesha wenyewe. Hakuna taasisi iliyojitengeneza yenyewe. Hakuna taasisi inayojiendesha yenyewe. Kumekuwepo na manung’uniko mengi sana kuhusu ukosekanaji wa mifumo bora na taasisi bora hapa Tanzania.

Muundo wa serikali yetu kwa sasa ni ‘top heavy’. Rais wetu ana madaraka makubwa sana na mengi mno. Sawa, hiyo ni kweli kabisa. Lakini, kilicho cha muhimu kabisa kabla hatujaanza kubadili namna tunavyojiongoza, ni lazima kuwepo na mabadiliko ya kifikra.

Ni lazima tubadilike kifikra na ndipo tutaweza kujenga mifumo imara na taasisi zilizo bora. Fikra kama za ‘ameula’, pale mtu anapoteuliwa kwenda kuutumikia umma, hazijengi chochote kile kilicho bora na imara.

Fikra za kwamba ‘Rais hakosei’, hazijengi chochote kilicho bora na imara. Fikra za kumuona Rais ni kama mungu mtu flani hivi, ni lazima zikome.

Fikra za kinafiki nazo lazima zikome. Kama mtu upo serikalini na hukubaliani na mwelekeo wa serikali unayoifanyia kazi, achana nayo. Jiuzulu. Siyo kujifanya unaunga mkono ili mradi tu uendelee kuitwa waziri lakini kumbe moyoni huamini katika chochote serikali hiyo inachokisimamia!

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki endapo kweli tunataka kuliendesha taifa letu kiutofauti na tunavyoliendesha sasa. Hata tukija kupata katiba bora kabisa duniani, endapo fikra zetu hazitobadilika, katiba hiyo itakuwa ni kazi bure tu. Our collective national ethos has to change. No two ways about it!

Peace ✌️. I’m outta here like last year.
 
Back
Top Bottom