Watu, Taasisi, na Mifumo...

Watu, Taasisi, na Mifumo...

Kwa hiyo Katiba ya South Africa unadhani inaheshimiwa kwa sababu ya mindset za watu au sababu ya institutions imara ambazo ni mazao ya Katiba?
Institution ni nini? Kuna institution bila watu? Watu walio na mindset ya kufuata na kutekeleza sheria ndo wanafanya institutions zifanye kazi.

Hakuna katiba bila watu. Hakuna institutions bila watu.

Na watu hao lazima wawe na mindset iliyo tofauti ili kuzifanya hizo institutions zifanye kazi.
 
Hakika... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Institution ni nini? Kuna institution bila watu? Watu walio na mindset ya kufuata na kutekeleza sheria ndo wanafanya institutions zifanye kazi.

Hakuna katiba bila watu. Hakuna institutions bila watu.

Na watu hao lazima wawe na mindset iliyo tofauti ili kuzifanya hizo institutions zifanye kazi.
Najuwa ni thread yako lakini kubali mawazo ya wengine. Hakuna nchi imefanikiwa kwa kutegemea strong men kwa kuwa strength Ina tofautiana kati ya mtu na mtu.

Hata yule Lee Kuan Yuan aliyeijenga Singapore alikuwa ni strong man lakini alitumia fursa aliyoipata kujenga strong institutions. Ndiyo maana hata baada ya Lee kutoka madarakani na kufariki, Singapore inaendelea
 
Sasa unanilazimisha nikubali mawazo ya wengine?

Duh!!

Weird!!!.

Hizo “strong institutions” zinajiendesha zenyewe eh? Hazina watu?

Institutions ni nini? Nimekuuliza hili swali lakini hujajibu bado.

Umeng’ang’ana tu “strong institutions”….

Au umekariri tu lakini hata hujui maana yake?
 
Sheria zinazoongoza hizo taasisi zinatungwa na watu, na hao watu ndio huziongoza hizo taasisi wakifuata misingi ya sheria na taratibu iliyowekwa na watangulizi, ukikomalia tu taasisi ni watu, mifumo ni watu, na sijui nini kingine ni watu unakuwa unakosea kwani hao watu huja na kuondoka, na mara nyingi hao watu huja na uwezo na tabia tofauti zinazoweza kuharibu ufanisi wa hizo taasisi.

Hivyo chini ya sheria/taratibu zilizowekwa, hizo taasisi na mifumo mingine hubakia strong regardless ya ni mtu gani anaeziongoza, ndio maana sasa tunataka Katiba Mpya ili chini yake tupate miongozo mahususi ya wapi tunataka taifa letu lielekee, na kila Rais na wengine watakaokuwa madarakani wabanwe na hizo sheria, mengi uliyoandika kwenye uzi wako hayajitoshekezi, bado unatakiwa ujifunze zaidi haya mambo.

Kwa muktadha huo, unaposema Katiba Mpya isubiri mpaka watu wapate elimu hilo halipo, na zaidi unataka kutudumaza kama taifa, haihitajiki kutoa elimu kwa watu, muhimu ni Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) iwekwe pale ituongoze, hao watu unaowataka wapewe elimu wataipata hiyo elimu kwa vitendo pale hiyo Katiba Mpya itakapoanza kutumika, kama taasisi/ taifa tayari ipo, hakuna haja kufundisha watu sheria, hizo sheria watazikuta pale ziwaongoze.
 
Kwa muktadha huo, unaposema Katiba Mpya isubiri mpaka watu wapate elimu hilo halipo, na zaidi unataka kutudumaza kama taifa, haihitajiki kutoa elimu kwa watu, muhimu ni Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) iwekwe pale ituongoze, hao watu unaowataka wapewe elimu wataipata hiyo elimu kwa vitendo pale hiyo Katiba Mpya itakapoanza kutumika.
Utasema yote, lakini mwisho wa siku huwezi kukwepa watu!

Watu waliopo ndo inabidi wazifuate na kuzitekeleza sheria zilizopo.

Wasipozifuata na kuzitekeleza, hizo sheria haziwezi kujitekeleza zenyewe.

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki ng’o!!

Pengine ni naongelea mambo ya kifalsafa zaidi ambayo huna uwezo wa kuyaelewa!
 
Kwa muktadha huo, unaposema Katiba Mpya isubiri mpaka watu wapate elimu hilo halipo, na zaidi unataka kutudumaza kama taifa, haihitajiki kutoa elimu kwa watu, muhimu ni Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) iwekwe pale ituongoze, hao watu unaowataka wapewe elimu wataipata hiyo elimu kwa vitendo pale hiyo Katiba Mpya itakapoanza kutumika, kama taasisi/ taifa tayari ipo, hakuna haja kufundisha watu sheria, hizo sheria watazikuta pale ziwaongoze.
🤣🤣

Una matatizo ya uelewa!

Hakuna niliposema “katiba mpya isubiri mpaka watu wapate elimu”.

Unazungumzia kitu ambacho sijakizungumzia kabisa!
 
Utasema yote, lakini mwisho wa siku huwezi kukwepa watu!

Watu waliopo ndo inabidi wazifuate na kuzitekeleza sheria zilizopo.

Wasipozifuata na kuzitekeleza, hizo sheria haziwezi kujitekeleza zenyewe.

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki ng’o!!

Pengine ni naongelea mambo ya kifalsafa zaidi ambayo huna uwezo wa kuyaelewa!
"Watu waliopo inabidi wazifuate na kuzitekeleza hizo sheria" paragraph yako ya pili.

Ndio maana nimekwambia hizo sheria imara ndio zinawasimamisha watu, hapo ni kwamba watu ndio wanazikuta sheria na kuzifuata, na Katiba Mpya ndio itakuwa muongozo wetu wa kule tunakoelekea kama taifa.

Hakuna falsafa yoyote hapo, umeanzisha mada ambayo huna uelewa wa kutosha kuihusu, ndio utulie uelekezwe.
 
Wewe ni bure kabisa! Kwaheri.
 
Una matatizo ya uelewa!

Hakuna niliposema “katiba mpya isubiri mpaka watu wapate elimu”.

Unazungumzia kitu ambacho sijakizungumzia kabisa!
Kwenye main thread yako, para ya 4 unazungumzia "tubadilike kifikra" hizo fikra za watu utazibadilisha kwa mtindo upi tofauti na kuwaelimisha hao watu?
 
Wewe ni bure kabisa! Kwaheri.
Lazima ukimbie tu, hamna point ya maana uliyoandika kwenye thread yako, nimetumia maneno yako mwenyewe kukubana, wala sijaweka yangu; shukuru wapo wasiojielewa wamekwambia "naunga mkono hoja"
 
Huu ni mfano mmoja wa wanafiki waliojaa ndani ya maccm na Serikali. Kabla hajateuliwa kuwa Katibu Mkuu alikuwa anaunga mkono Katiba mpya lakini alipoteuliwa akasema hayo ni mawazo yake kama Katibu Mkuu wa maccm anaunga mkono mawazo ya chama ya kuipinga Katiba Mpya.
Mifumo ni watu. Taasisi ni watu. Na vyote hivyo ni kwa ajili ya watu.

Hakuna mfumo uliojiumba wenyewe tu na unaojiendesha wenyewe. Hakuna taasisi iliyojitengeneza yenyewe. Hakuna taasisi inayojiendesha yenyewe. Kumekuwepo na manung’uniko mengi sana kuhusu ukosekanaji wa mifumo bora na taasisi bora hapa Tanzania.

Muundo wa serikali yetu kwa sasa ni ‘top heavy’. Rais wetu ana madaraka makubwa sana na mengi mno. Sawa, hiyo ni kweli kabisa. Lakini, kilicho cha muhimu kabisa kabla hatujaanza kubadili namna tunavyojiongoza, ni lazima kuwepo na mabadiliko ya kifikra.

Ni lazima tubadilike kifikra na ndipo tutaweza kujenga mifumo imara na taasisi zilizo bora. Fikra kama za ‘ameula’, pale mtu anapoteuliwa kwenda kuutumikia umma, hazijengi chochote kile kilicho bora na imara.

Fikra za kwamba ‘Rais hakosei’, hazijengi chochote kilicho bora na imara. Fikra za kumuona Rais ni kama mungu mtu flani hivi, ni lazima zikome.

Fikra za kinafiki nazo lazima zikome. Kama mtu upo serikalini na hukubaliani na mwelekeo wa serikali unayoifanyia kazi, achana nayo. Jiuzulu. Siyo kujifanya unaunga mkono ili mradi tu uendelee kuitwa waziri lakini kumbe moyoni huamini katika chochote serikali hiyo inachokisimamia!

Mabadiliko ya kifikra hayakwepeki endapo kweli tunataka kuliendesha taifa letu kiutofauti na tunavyoliendesha sasa. Hata tukija kupata katiba bora kabisa duniani, endapo fikra zetu hazitobadilika, katiba hiyo itakuwa ni kazi bure tu. Our collective national ethos has to change. No two ways about it!

Peace ✌️. I’m outta here like last year.
 
Huu ni mfano mmoja wa wanafiki waliojaa ndani ya maccm na Serikali. Kabla hajateuliwa kuwa Katibu Mkuu alikuwa anaunga mkono Katiba mpya lakini alipoteuliwa akasema hayo ni mawazo yake kama Katibu Mkuu wa maccm anaunga mkono mawazo ya chama ya kuipinga Katiba Mpya.

Noma sana.

Watu hawana principles kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sasa unanilazimisha nikubali mawazo ya wengine?

Duh!!

Weird!!!.

Hizo “strong institutions” zinajiendesha zenyewe eh? Hazina watu?

Institutions ni nini? Nimekuuliza hili swali lakini hujajibu bado.

Umeng’ang’ana tu “strong institutions”….

Au umekariri tu lakini hata hujui maana yake?
Katiba ndiyo inazaa strong institutions kama Bunge, Tume huru ya uchaguzi, Mahakama, Jeshi, Polisi, Magereza nk

Strong men watakuwa zao la institutions
 
Hakuna strong institutions bila watu.

Au hizo strong institutions ni ma satellite?
 
Katiba ndiyo inazaa strong institutions kama Bunge, Tume huru ya uchaguzi, Mahakama, Jeshi, Polisi, Magereza nk

Strong men watakuwa zao la institutions
Bora unisaidie, jamaa kaleta mada asiyojua alichoandika.
 
Nyani Ngabu ni mbishi na hataki kuelewa wala kubadili alivyokariri.

Kwangu strong men ni kama akina Kagame, Museveni na Mugabe. Ukiwa strong wewe ukifa au ukitoka madarakani na mambo yako uliyoyasimamia yanaishia hapo. Lakini nchi zenye strong institutions ni kama South Africa. Thabo Mbeki alipochemsha, akakaa pembeni na Jacob Zuma aka step in and thereafter akaja Cyril Ramaphosa.

Tanzania ilikuwa na Magufuli kama strong man ambaye maguvu yake yalikuwa makubwa kuliko institutions. Aliyoyafanya Mwendazake tunayajua
 
Asipoelewa na hapa basi.
 
Hizo institutions ni nini? Ni mashine?
 
Man naona hii mada uliyoileta hapa ni wachache sana wamekuelewa nini unajaribu kuwahabarisha.

Zaidi utagundua tu kwamba watu wamekariri mambo bila kuwa na uelewa nayo,na hiyo ndio shida kubwa inayotukabili.

Kwamba wao wanaamini tukishakuwa tu na 'katiba mpya ya wananchi' basi kila kitu kitajiendea smoothly regardless of anything else.

Leo hii ukijaribu kuwaambia kuwa tunaweza kuwa Taifa lenye mafanikio na maendeleo makubwa hata kama tutakuwa na katiba mbovu zaidi ya hii, ila cha msingi tuwe na jamii inayojitambua,isiyo na nidhamu ya woga,yenye fikra sahihi na mitazamo sahihi,lazima watakuona wewe CHIZI.

Wamekariri katiba mpya na Taasisi imara,sasa sijui hivyo vitu vitakuja kusimamaiwa na malaika kutoka mbinguni au watu hawa hawa wenye akili kama hizi?
 
Back
Top Bottom