GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Sijui kama na mikoa mingine ina watu wa wenye ujasiri huo!. Nimeshaona hayo zaidi ya mara moja Kanda ya Ziwa.
Wakati fulani, nilikuwa nikienda sehemu fulani jijini Mwanza kwa gari la taasisi fulani. Hilo gari lilikuwa na watu wazima pamoja na wanafunzi wa shule fulani ya huko huko jijini Mwanza. Moja ya njia gari letu lilikopita ni kando kando ya Ziwa Victoria. Ilikuwa ni majira ya Mchana.
Ghafla, wanafunzi waliokuwemo kwenye hilo gari walianza kupiga kelele zilizoashiria wameona kitu kisichokuwa cha kawaida. Na ndivyo ilivyokuwa. Waliwaona wanaume watu wazima wakioga ziwani jirani na gari letu lilikokuwa likipita. Kumbe walikuwa wanaoneshana hayo "maajabu".
Niliwakemea na wakatulia, lakini hata mimi binafsi nilishangazwa na ujasiri wa hao watu kuthubutu kuoga hadharani majira ya Mchana.
Wakati mwingine tena, nilienda maeneo ya machimbo ya dhahabu wilayani Misungwi mkoani Mwanza. Kutokana na shughuli iliyonipeleka huko kunihitaji kuwepo huko muda mrefu, nililazimika kutafuta makazi ya muda. Nilipangisha kwenye gesti iliyo huko huko machimboni.
Wateja wengi wa hiyo gesti walikuwa ni watu wanaojishughulisha na shughuli za madini(dhahabu).
Siku moja, majira ya saa tisa Alasiri, nilishtushwa na niliyoyashuhudia . Nilikuwa naenda bafuni kuoga, ndipo nikamkuta mmoja wa wapangaji wa hiyo gesti akioga huku mlango ukiwa wazi.
Siku nyingine tena, majira kama hayo hayo, saa tisa Alasiri, nilimkuta mpangaji mwingine akioga huku mlango wa bafuni ukiwa wazi kabisa
Matukio hayo mawili yalinisukuma kuwauliza wenyeji niliozoeana nao maana ya hayo mambo. Mmoja wa niliowauliza aliniambia kuwa kuwa inawezekana ni masharti ya dawa alizopewa na mganga wa Kienyeji, eti ili zimsaidie kufanikiwa kwenye shughuli ya dhahabu.
Hivi karibuni tena, nimeyaona matukio kama hayo mara mbili. Safari hii, ni mwanaume mtu mzima kuoga kwenye mto ulio pembezoni mwa barabara, Mchana, tena akiwa ametazama upande wa barabarani, kwa hiyo watu wanaopita, wakiwemo watoto, wanawaona wakiwa kama walivyozaliwa. Hayo yametokea Geita Vijijini.
Inahitaji ujasiri wa ziada kuweza kufanya hivyo.
Kuuliza si ujinga! Je! Kuoga hadharani ni sehemu ya utamaduni wa baadhi ya watu?