Watu kuachana siyo dhambi, talaka siyo dhambi

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Ndugu zangu habari, kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Huwa kwenye harakati zangu za ulinganiaji wa dini ya kiislamu nikiwa mimi ni mwalimu, mwanafunzi na mlinganiaji wa dini kwa Quraan na Sunna katika njia ya waja wema waliotangulia, ninakutana na kesi nyingi za ndoa ambazo mimi ninapewa fursa ya kuzitatua. Walillaahil hamdu huwa nafanikiwa kwa idhini na uwezo wa Allaah.

Sasa kuna jambo nimeliona ni tatizo kubwa katika jamii yetu. Kuanzia kwa wazazi wa wanandoa, na viongozi wa dini, wana kawaida na desturi mbovu na inayoharibu mustaqabal wa watu katika jamii.

Mapenzi ni kiumbe, nayo yameumbwa na Allah. Yanazaliwa, yanakuwa, yanaishi, yanazeeka na kufa. Na kuna mengine hata uzeeni hayafiki yanaishia mwanzoni tu na yanakufa. Kwa sababu chanzo cha ndoa ni mapenzi, na bila mapenzi hakuna ndoa tena. Hivyo basi yanapokufa mapenzi, na ndoa pia ipo matatani.

Sasa kwenye jamii zetu watu wanapofunga ndoa, inakuwa kama wamejiloga. Inapofikia watu wamechokana na mapenzi yamekwisha, watu wa nje hasa wazazi na viongozi wa dini (wasio na elimu ya hiyo dini) wanaona kuachana ni kama dhambi kubwa sana isiyosameheka.

Hali hiyo inapelekea wanandoa wanapopeleka kesi zao za ndoa kwa wazazi na ndugu kutatua changamoto zao, basi ndugu wale watalazimisha wanandoa wale warudi wakayamalize wenyewe. Sasa swali la kujiuliza, wakayamalizeje wenyewe wakati mpaka linafika kwenu ujue kwao limewashinda, mnataka nini zaidi kiendelee baina yao?

Wakati mwingine mnapoona baina ya wanandoa hawa wana kila dalili baina yao hakuna mapenzi tena, ama kuna usaliti ambao tayari umeua mapenzi na imani, yaani mfano mke kapenda mtu mwingine nje hamtaki mumewe tena, wasaidieni wanandoa hawa kuachana kwa kuchunga maslahi yao. Kuliko kulazimisha kuendelea kuwa pamoja, ni hatari.

Hili siyo dhambi na wala hutoambiwa umewaachanisha, ila umeepusha madhara zaidi yanayoweza kutokea. Hivi hamuoni kesi za mauaji ya baina ya wanandoa zilivyoshamiri, mfano wa yule jamaa kule Mwanza, Unaambiwa kesi ilifika kwa wazazi ila wazazi wakawasisitiza waendelee kuvumiliana!

Kuvumiliana nini na mapenzi yameisha?

Ukienda kwa uongozi wa dini hasa wa kiislaam, mwanamke anapokwenda kwao (kwa sababu katika uislaam, anayetoa talaka ni mume, na ikitokea mke hana mapenzi tena kwa mumewe na maudhi yamekithiri, mke hawezi kutoa talaka na ikiwa mume hataki kutoa talaka, basi ataenda kwa kiongozi wa dini, Qadhi) adai ndoa yake ivunjwe, kiongozi wa dini akiletewa kesi kama hiyo, eti atauliza "Kwanini unataka ndoa ivunjike?" Swali hili halina maana, kwa sababu kwani wakati anataka kuolewa ulimuuliza kwanini anataka kuolewa?

Wazazi na ndugu mnapoletewa kesi za ndoa na watoto wenu mzitatue, na mkajiridhisha bila shaka hapa hakuna mapenzi tena, wasaidieni wanandoa hao kuachana. Kufanya hivyo kuna manufaa zaidi kuliko kulazimisha waendelee kuvumiliana.

Viongozi wa dini pamoja na mahakama na polisi, kesi za ndoa zinapofika kwenu jaribu kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza baadae katika kulazimisha kuiweka ndoa iliyokwisha mapenzi. Wasaidieni kuachana, siyo dhambi.

Na sisi wanaume wa kiislaamu, jukumu la talaka Allaah aliliweka mikononi mwetu kwa maana kubwa sana.
Ukiona mke hapa mapenzi hakuna, hanipendi tena hata nimfanyie nini, au simpendi tena, talaka siyo dhambi kabisa. Tena ukilazimisha kuishi pamoja katika hali hiyo ndiyo dhambi sasa.

Mimi huwa nikipata kesi kama hiyo na nikithibitisha pasi na shaka hapa kuna madhara makubwa yanaweza kutokea, ninashauri wanandoa hao waachane. Mume akikataa kutoa talaka, namwambia mke nenda kwenu, anza maisha mapya.

Tupunguze hizi kesi za watu kuuana na kudhuriana kila siku kwa ajili ya migogoro ya ndoa, ambayo yakitokea wazazi na ndugu eti wanatoa ushuhuda, eti kweli walikuwa na mgogoro kabla ila tuliwaambia wavumiliane. Wavumiliane kuuana?

IMG-20220914-WA0001.jpg

IMG-20220914-WA0002.jpg

Talaka siyo dhambi.

Allaah ni mjuzi zaidi wa kila kitu.
 
Ndugu zangu habari, kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Huwa kwenye harakati zangu za ulinganiaji wa dini ya kiislamu nikiwa mimi ni mwalimu, mwanafunzi na mlinganiaji wa dini kwa Quraan na Sunna katika njia ya waja wema waliotangulia, ninakutana na kesi nyingi za ndoa ambazo mimi ninapewa
Uzi ni Mzuri sana Sheikh, ila vijana wa hovyo hawataki kupita hapa. Wanapita kwenye thread nyingine za hovyo.
 
Serikali kwa kushirikiana na makanisa na uongozi wa misikiti waweke issue ya talaka iwe simple tu. Yaani ata mkianza leo, ndani ya week mshaachana kila mtu 50 zake.
 
Utaratibu wenyewe ni mgumu balaa. Yaani mpaka mnaona Bora tuendelee kuishi hivi hivi pamoja na shida zetu.
 
Uzi ni Mzuri sana Sheikh, ila vijana wa hovyo hawataki kupita hapa. Wanapita kwenye thread nyingine za hovyo.
WACHA WAUANE... HATUWEZI JUA... HUENDA NDIO NAMNA ALLAAH ANAVYOWADHIBU WAOVU...
 
Ndugu zangu habari, kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Huwa kwenye harakati zangu za ulinganiaji wa dini ya kiislamu nikiwa mimi ni mwalimu, mwanafunzi na mlinganiaji wa dini kwa Quraan na Sunna katika njia ya waja wema waliotangulia, ninakutana na kesi nyingi za ndoa ambazo mimi ninapewa fursa ya kuzitatua. Walillaahil hamdu huwa nafanikiwa kwa idhini na uwezo wa Allaah.

Sasa kuna jambo nimeliona ni tatizo kubwa katika jamii yetu. Kuanzia kwa wazazi wa wanandoa, na viongozi wa dini, wana kawaida na desturi mbovu na inayoharibu mustaqabal wa watu katika jamii.

Mapenzi ni kiumbe, nayo yameumbwa na Allah. Yanazaliwa, yanakuwa, yanaishi, yanazeeka na kufa. Na kuna mengine hata uzeeni hayafiki yanaishia mwanzoni tu na yanakufa. Kwa sababu chanzo cha ndoa ni mapenzi, na bila mapenzi hakuna ndoa tena. Hivyo basi yanapokufa mapenzi, na ndoa pia ipo matatani.

Sasa kwenye jamii zetu watu wanapofunga ndoa, inakuwa kama wamejiloga. Inapofikia watu wamechokana na mapenzi yamekwisha, watu wa nje hasa wazazi na viongozi wa dini (wasio na elimu ya hiyo dini) wanaona kuachana ni kama dhambi kubwa sana isiyosameheka.

Hali hiyo inapelekea wanandoa wanapopeleka kesi zao za ndoa kwa wazazi na ndugu kutatua changamoto zao, basi ndugu wale watalazimisha wanandoa wale warudi wakayamalize wenyewe. Sasa swali la kujiuliza, wakayamalizeje wenyewe wakati mpaka linafika kwenu ujue kwao limewashinda, mnataka nini zaidi kiendelee baina yao?

Wakati mwingine mnapoona baina ya wanandoa hawa wana kila dalili baina yao hakuna mapenzi tena, ama kuna usaliti ambao tayari umeua mapenzi na imani, yaani mfano mke kapenda mtu mwingine nje hamtaki mumewe tena, wasaidieni wanandoa hawa kuachana kwa kuchunga maslahi yao. Kuliko kulazimisha kuendelea kuwa pamoja, ni hatari.

Hili siyo dhambi na wala hutoambiwa umewaachanisha, ila umeepusha madhara zaidi yanayoweza kutokea. Hivi hamuoni kesi za mauaji ya baina ya wanandoa zilivyoshamiri, mfano wa yule jamaa kule Mwanza, Unaambiwa kesi ilifika kwa wazazi ila wazazi wakawasisitiza waendelee kuvumiliana!

Kuvumiliana nini na mapenzi yameisha?

Ukienda kwa uongozi wa dini hasa wa kiislaam, mwanamke anapokwenda kwao (kwa sababu katika uislaam, anayetoa talaka ni mume, na ikitokea mke hana mapenzi tena kwa mumewe na maudhi yamekithiri, mke hawezi kutoa talaka na ikiwa mume hataki kutoa talaka, basi ataenda kwa kiongozi wa dini, Qadhi) adai ndoa yake ivunjwe, kiongozi wa dini akiletewa kesi kama hiyo, eti atauliza "Kwanini unataka ndoa ivunjike?" Swali hili halina maana, kwa sababu kwani wakati anataka kuolewa ulimuuliza kwanini anataka kuolewa?

Wazazi na ndugu mnapoletewa kesi za ndoa na watoto wenu mzitatue, na mkajiridhisha bila shaka hapa hakuna mapenzi tena, wasaidieni wanandoa hao kuachana. Kufanya hivyo kuna manufaa zaidi kuliko kulazimisha waendelee kuvumiliana.

Viongozi wa dini pamoja na mahakama na polisi, kesi za ndoa zinapofika kwenu jaribu kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza baadae katika kulazimisha kuiweka ndoa iliyokwisha mapenzi. Wasaidieni kuachana, siyo dhambi.

Na sisi wanaume wa kiislaamu, jukumu la talaka Allaah aliliweka mikononi mwetu kwa maana kubwa sana.
Ukiona mke hapa mapenzi hakuna, hanipendi tena hata nimfanyie nini, au simpendi tena, talaka siyo dhambi kabisa. Tena ukilazimisha kuishi pamoja katika hali hiyo ndiyo dhambi sasa.

Mimi huwa nikipata kesi kama hiyo na nikithibitisha pasi na shaka hapa kuna madhara makubwa yanaweza kutokea, ninashauri wanandoa hao waachane. Mume akikataa kutoa talaka, namwambia mke nenda kwenu, anza maisha mapya.

Tupunguze hizi kesi za watu kuuana na kudhuriana kila siku kwa ajili ya migogoro ya ndoa, ambayo yakitokea wazazi na ndugu eti wanatoa ushuhuda, eti kweli walikuwa na mgogoro kabla ila tuliwaambia wavumiliane. Wavumiliane kuuana?

View attachment 2356659
View attachment 2356661

Talaka siyo dhambi.

Allaah ni mjuzi zaidi wa kila kitu.
Mapenz matamu sana kuishi Kwa stress ni kujitakia tu
 
Back
Top Bottom