jembelamkono
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 2,733
- 2,021
Nchi wameila sana zaidi ya miaka 50 sasa wameshtuka usingizini wanaanza vitisho kwa wananchi haohao waliotunyonya miaka yote.
Jambo la kushangaza watu wameibuka na kauli mbalimbali wakiwemo wanasiasa, ambazo zimebadili maana halisi iliyokuwa kwenye baadhi ya maneno ya Mh. Rais.
Mh. Rais aliwaambia ma-RC "kuna watendaji wengine kazi yao ni kuwanyanyasa wananchi nendeni mkawashughulikie. Nyinyi mna mamlaka ya kumweka mtu ndani masaa 48, wawekeni ndani ili wawaheshimu wananchi". Lakini kauli hii imepindishwa na watu, hata wengine wakisema wakuu wa mikoa wameagizwa waende kuwakamata vijana wasiokuwa na kazi!
Hivi kweli hawa wakuu wa mikoa ni watu wasiojitambua ambao wanaweza kuitumia sheria inayowapa mamlaka hayo kuwaonea watu wasiokuwa na hatia?
Jambo jingine ambalo linapotoshwa ni kauli ya Rais kuzuia watu kucheza pool table asubuhi na kuwataka vijana kufanya kazi badala ya kuzurura pale alipokazia kuwa ikiwezekana walazimishwe kufanya kazi kwenye kambi maalum.
Watanzania wenzangu hivi ni kutokufuatilia sheria au ni upotoshaji wa makusudi? Niwaulize wanasheria akina Tundu Lissu, sheria inasemaje kuhusu muda wa kufungua bar na sehemu mbalimbali za starehe? Sheria inasemaje kuhusu uzembe na uzurulaji?
Mimi sioni kama mh. Rais ametunga sheria mpya ya kwake bali anasimamia sheria ambazo zilikosa usimamizi ambazo leo ni matokeo yaliyozalisha makundi ya vibaka mitaani.
Sasa hayo maendeleo mnayoyataka yatakuja kwa watu kucheza pool table na betting huku ardhi ikiendelea kustawisha majani?
Sasa nimeamini kuwa sisi wananchi wa Tanzania ni wavivu wa kufikiri na wavivu wa miili yetu,
Baadhi ya watu wameponda maagizo ya rais na wanaponda juhudi za rais katika utendaji wake wa kazi, wakiwepo wanasisa, mfano kuna mtu eti anaenda kucheza pool table eti anasubiri viwanda vifufuliwe aajiriwe huu ni ujuha usio na kifani.
Wengi wanaolalamika wanaishi mijini kwa misheni town huku wakiwa wameacha hekari na hekari vijijini kwao wakisubiri bibi na babu zao walime wao wakale mazao tu.
Kama kwetu kutakuwa na malalamiko maana vijana wanaenda kipindi cha mavuno tu so wazee wanaolalamika sana.
Rudini vijijini mkalime na bibi zenu mpate hela, mfano mimi nalima alizeti na mahindi kwa na mwaka huu natarajia kupata gunia zaidi ya 50.
TAFAKARI hakuna serikali inayoweza kuajiri wananchi wake wote. Na pia Nafanya ufugaji wa kuku wa mayai
Watu wamepotosha kuhusu ni nani Rais aliongelea anaweza kuwekwa ndani.Sasa hapo kwenye red ume quote nini na unatapinga na kutetea nini?
Hapo kwenye green, masikini Tanzania, ndiyo tuisahau kabisa Tanzania ya viwanda. Kwanza habari za bar saa ngapi sijui hadi saa ngapi unadhani watu wote ni waalim kwamba anaingia asubuhi na kutoka jioni? Hujui kuwa watu wana kazi tofauti na wana shift? Kingine kwa amri hiyo ya haari za asubuhi na jioni nadhani aliyeitoa amri hiyo si visionary leader, atakuwa ni ookkeeper tu, unajua nchi ya viwanda huwa hailali? tofauti ya usiku na mchana ni giza na jua, usiku kuwashwa taa na mchana kuwaka jua...maisha ya nchi za viwanda yametawaliwa na shift tu. Sasa kama tunaelekea huko inakuwaje kuweka amri kama hii.
Ama kwa hakika acha kuku aendelee kuwaaminisha vifaranga wake kuwa kesho atawanyonyesha.
Ardhi inatumiwa na majambazi kujificha. aibu. mapori teleee
Rais mwema na mkarimu wa awamu ya nne, mwenye kumchekea hata yule ambaye hampendi, ametupatia somo tosha kabisa kwamba ukimchekea nyani basi tegemea kuvuna mabua. Ndio maana watu wamemchagua huyu ambaye ni kauzu zaidi ya dagaa.Unamtetea tu. Magufuli ni rais anayependa udikteta.
Alishasema kwamba akichaguliwa watu watalimia meno.
Alishaliamuru bunge lipeleke fedha za tafrija yake kuchangia hospitali kinyume na katiba.
Alishafundisha mahakama jinsi ya kufanya kazi.
Katujazia wanajeshi kwenye wakuu wa mikoa.
Anawaagiza wakamate kamate watu na kuwafunga.
Utamteteaje raisi mbabe kama huyu?
Tukiwa hatuwezi kujua balance, mizani na kiasi tutakufa kwa excess, ya upole au ukali.Rais mwema na mkarimu wa awamu ya nne, mwenye kumchekea hata yule ambaye hampendi, ametupatia somo tosha kabisa kwamba ukimchekea nyani basi tegemea kuvuna mabua. Ndio maana watu wamemchagua huyu ambaye ni kauzu zaidi ya dagaa.
I see,we jamaa kweli ndo umeandika hivyo kwa kudhamiria au utani.Na kundi unalolilenga hapa ni kindi la aina gani ya vijana.1: Kuwachotea maji watu waliombali na huduma ya maji
2:Kubeba mizigo sehemu ya stand na maduka
3:Kuwa kibarua mashambani
4:Kusafisha na kupanga vifaa kwenye maduka
5:Kuhudumia mifugo
Kwa sasa hivi tunauhitaji ukali ili tuweze kunyooka. Upole umechangia katika kukuza tabia za kivivu, tabia za ufisadi, tabia za watu kupenda makundi ya kisiasa, kwa kifupi JPM sio mwanamitandao na mtanzania mwenye kuitanguliza nchi na sio siasa. Hayo mambo ya balance na mizani, yamekaa kama hadithi za kwenye zile novels za zamani, hayafanani na reality ya 2016.Tukiwa hatuwezi kujua balance, mizani na kiasi tutakufa kwa excess, ya upole au ukali.
Si kweli.Kwa sasa hivi tunauhitaji ukali ili tuweze kunyooka. Upole umechangia katika kukuza tabia za kivivu, tabia za ufisadi, tabia za watu kupenda makundi ya kisiasa, kwa kifupi JPM sio mwanamitandao na mtanzania mwenye kuitanguliza nchi na sio siasa. Hayo mambo ya balance na mizani, yamekaa kama hadithi za kwenye zile novels za zamani, hayafanani na reality ya 2016.
Wewe umesema nikutajie kazi zisizohitaji mtaji, zipo nyingi sana. Sasa cha msingi ni kuangalia kuna makundi ya aina ngapi ya vijana.I see,we jamaa kweli ndo umeandika hivyo kwa kudhamiria au utani.Na kundi unalolilenga hapa ni kindi la aina gani ya vijana.
Hivi taifa kama USA au German wanatumia UKALI?Kwa sasa hivi tunauhitaji ukali ili tuweze kunyooka. Upole umechangia katika kukuza tabia za kivivu, tabia za ufisadi, tabia za watu kupenda makundi ya kisiasa, kwa kifupi JPM sio mwanamitandao na mtanzania mwenye kuitanguliza nchi na sio siasa. Hayo mambo ya balance na mizani, yamekaa kama hadithi za kwenye zile novels za zamani, hayafanani na reality ya 2016.
Kwa jinsi nchi ilipofikia ni lazima maumivu yatokee ili nchi ibadilike. Nchi ilikuwa shamba la bibi. Hakuna utii wa sheria, kila mtu anafanya lake mradi lina manufaa kwake na watoto wake na si kwa taifa.
Sababu ya wasomi kujaa kwenye nafasi ya ukatibu mkuu, ni kuhakikisha akili bora kabisa zinaitumikia nchi. Wenye kiasi hawakuweza kupita kwenye michujo ya vyama, na wapiga kura waliona cha muhimu sioi kiasi bali ni mtu asiye tayari kuendekeza siasa za kinafiki. TZ haihitaji another diplomat, tumekuwa nao wengi tu na wamekuwa wakituzingua, ngoja tumpe muda mwanasayansi tuliyemchagua.Si kweli.
Tunahitaji kiasi. Ukali unafanya mambo kwa pupa bila tafakari wala mipango endelevu.
Sababu ya wasomi kujaa kwenye nafasi ya ukatibu mkuu, ni kuhakikisha akili bora kabisa zinaitumikia nchi. Wenye kiasi hawakuweza kupita kwenye michujo ya vyama, na wapiga kura waliona cha muhimu sioi kiasi bali ni mtu asiye tayari kuendekeza siasa za kinafiki. TZ haihitaji another diplomat, tumekuwa nao wengi tu na wamekuwa wakituzingua, ngoja tumpe muda mwanasayansi tuliyemchagua.
USA walipata uhuru kwenye miaka ya1700, wakati huo nchi yetu ilikuwa inafananaje?. Kina Issac Newton ni wasomi waliosoma karne nyingi zilizopita, wakati nchi yetu ilikuwa ni vichaka vitupu. Germany taifa kubwa sana, liko juu kuliko nchi zote za Ulaya, huwezi kuilinganisha na Tanzania. Ukali kwa nchi yenye miaka 55 ya uhuru ni muhimu sana, tunazo changamoto nyingi sana kwa hiyo tukiendelea kulegezeana, tutaendelea kulalamika kwanini wenzetu wanaendelea. Demokrasia ikizidi sana huzaa ujinga na kiburi, kila mtu anajiona ana haki, kumbe ni upuuzi mtupu.Hivi taifa kama USA au German wanatumia UKALI?