Naomba nianze kujibu para ya mwisho ya post yako. Sidhani kwamba hao ma RC waliopewa agizo la kupeleka vijana kulima watakuwa wajinga kiasi cha kuwakusanya vijana na kuwataka wakalime kilimo cha kizamani kisicho na tija! Ni wazi majembe na mashoka yanaweza kutumika kusafisha maeneo ingawa vipo vifaa vya kisasa vinavyowezatumika. Lakini vijana wenye dhamira ya kujitafutia maendeleo watakuwa tayari kwa lolote.
Joka kuu najua wewe umeshuhudia yaliyojiri katika awamu ya kwanza Mwalimu Nyerere alipoanzisha Jeshi LA Kujenga Taifa. Vijana waliomaliza shule za msingi na hawakuwa na ajira walijiunga kwa wingi lkn wasomi hawakutaka kujiunga wakaona huko si mahali pao kwa sababu JKT kulikuwa na kazi za kilimo na za kutumia maguvu. Ikafika hatua wasomi wakatakiwa wajiunge kwa nguvu tena kwa mujibu wa sharia. Waliandamana kupinga lkn serikali ile haikuwa na mdhaha. Mwishowe wasomi wrote walipitia JKT wakashika majembe kama vijana wenzao. Ironically wasomi wale walipotoka pale walilipenda jeshi na kulisifia hadi leo! Matunda ya JKT mpaka Leo hayajasahauliwa. Zoezi la vijana kuoNdolewa kwenye kucheza pool likisimamiwa vizuri litaleta matokea mazuri yatakayo furahiwa na vijana na pia wote ambao kwa sasa wanaoona jambo hili halina tija.
Nikirudi kwenye mifano yako ya nchi zilizoendelea na white au blue colar jobs nk tufike mahali tutambue kwamba tutakuwa tunakosea kujifananisha na yaliyojiri ama yanayojiri kwenye nchi zilizoendelea. Tulipoanza kushabikia utandawazi na kuanza kuangalia maendeleo ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea kama Indonesia, Malaysia nk na kudhani tunaweza kuiga kutoka huko tumejikuta bado tuko palepale na pengine tumejirudisha nyuma zaidi maana utandawazi ule ukawa ni utandawizi ambao Rais Magufuli ameachiwa kazi ya kuhangaika nao.
Utamaduni wa Nchi husika una mchango mkubwa kwenye maendeleo. Utamaduni wa Watanzania unachangia sana kwenye hali hii tuliyonayo. Hili linahitaji mjadala.....
..maelezo yako kwa kiasi kikubwa ni mazuri.
..mimi nimekwenda JKT, na napenda kukuhakikishia kwamba vijana waliokuwa PRODUCTIVE ktk makambi yale ni wale waliokuwa na ujuzi fulani waliotokea shule za UFUNDI, KILIMO, UALIMU, au UGANGA. wengine waliosoma klf, pcm, pcb, etc walikuwa wanapotezewa tu muda wao, na walikuwa hawana tofauti kubwa na wazururaji tunaowapiga vita mijini.
..pia makambi ya JKT yalikuwa yamekubuhu kwa UDHALILISHAJI wa watoto wa kike kwa maafande na viongozi wa serikali kuwalazimisha UGONI. hilo ni suala ambalo halizungumziwi kwa uwazi na undani ktk mijadala inayohusu JKT kwa mujibu wa sheria.
..kwenye nchi kama GHANA wana "jkt" tofauti na hii ya hapa kwetu. vijana hawaendi kulimishwa kwa jembe la mkono, au hata trekta, bali wanakwenda kufanya kazi kwenye maidara mbalimbali ya serikali kulingana na taaluma waliyosomea.
..siamini kama tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu linapaswa kushughulikiwa kwa utaratibu wa agizo hili la Raisi kwa ma-rc na ma-dc. miaka ya nyuma vijana wasiokuwa na kazi waliwahi kukusanywa na kupelekwa kulima ktk vijiji vya GEZAULOLE na KIBUGUMO nje ya jiji la Dsm.
..tukikuza uchumi wetu, tukaweka mazingira mazuri ya WAZALISHAJI, na siyo waagizaji, kuanzisha shughuli zao kwa wingi hapa Tz vijana wengi wanaozurura watapata mahali pa kwenda.
..zaidi, siyo siri kwamba kilimo Tz hakilipi na matokeo yake vijana wengi wanakimbia vijijini kuja mjini wakitafuta nafuu ya maisha. kwa hiyo tunatakiwa tuweke mazingira mazuri kwa wale wanaolima sasa hivi ili wafanikiwe na mazingira hayo yatavutia wengi zaidi kulima.
NB:
..Kilimo kwanza imeishia wapi? Mpango ule ulikuwa mzuri kama ungepata msimamizi mzuri kama Magufuli.