Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wana JF,
Jana Rais Magufuli aliwahutubia kwa muda mfupi wakuu wa mikoa baada ya kuwaapisha. Rais aliongea mambo machache lakini yaliyobeba maana kubwa kuhusu uwajibikaji na watu kufanya kazi hasa akitia msisitizo kuwa tumeshachelewakwa kuwa haya yalitakiwa kuanza miaka kumi iliyopita.
Ni ukweli uliyodhahiri kuwa tumechelewa tena sana kutokana na nchi yetu iliyojaliwa kuwa na raslimali nyingi pamoja na ardhi kubwa yenye rutuba.
Jambo la kushangaza watu wameibuka na kauli mbalimbali wakiwemo wanasiasa, ambazo zimebadili maana halisi iliyokuwa kwenye baadhi ya maneno ya Mh. Rais.
Mh. Rais aliwaambia ma-RC "kuna watendaji wengine kazi yao ni kuwanyanyasa wananchi nendeni mkawashughulikie. Nyinyi mna mamlaka ya kumweka mtu ndani masaa 48, wawekeni ndani ili wawaheshimu wananchi".
Lakini kauli hii imepindishwa na watu, hata wengine wakisema wakuu wa mikoa wameagizwa waende kuwakamata vijana wasiokuwa na kazi!
Hivi kweli hawa wakuu wa mikoa ni watu wasiojitambua ambao wanaweza kuitumia sheria inayowapa mamlaka hayo kuwaonea watu wasiokuwa na hatia?
Jambo jingine ambalo linapotoshwa ni kauli ya Rais kuzuia watu kucheza pool table asubuhi na kuwataka vijana kufanya kazi badala ya kuzurura pale alipokazia kuwa ikiwezekana walazimishwe kufanya kazi kwenye kambi maalum.
Watanzania wenzangu hivi ni kutokufuatilia sheria au ni upotoshaji wa makusudi?
Niwaulize wanasheria akina Tundu Lissu, sheria inasemaje kuhusu muda wa kufungua bar na sehemu mbalimbali za starehe? Sheria inasemaje kuhusu uzembe na uzurulaji?
Mimi sioni kama mh. Rais ametunga sheria mpya ya kwake bali anasimamia sheria ambazo zilikosa usimamizi ambazo leo ni matokeo yaliyozalisha makundi ya vibaka mitaani.
Hapa Tanzania haiingii akilini kwa mtu anayejua hasa kutumia zile dutu nyeupe zilizo katika fuvu la kichwa ukimwambia hakuna kitu chochote cha kufanya kukuingizia kipato. Huko ni kukosa ubunifu na kuyaacha mambo yaende kwa kudra za Mwenyezi Mungu.
Katika nchi iliyo na ardhi zaidi ya 70% haijakaliwa na watu wala haimilikiwi na mtu. Ardhi ni mtaji wa kwanza kwa sababu juu ya ardhi ndipo kila kitu kinafanyika.
Kila Mtanzania aliye na akili timamu kutoka moyoni mwake ukiacha anachokisema mdomoni ili kuwahadaa, anajua kuwa sasa hivi vijana wengi wamekuwa wavivu hawataki kazi ngumu, wamekuwa ni watu wanaotaka kuvuna wasipopanda. Kiasilia hilo jambo halipo wala haliwezekani, hata Simba porini anapambana kupata mawindo.
Rai yangu kwa Watanzania wenzangu, acheni kupotosha maana halisi ya maneno ya Mh. Rais ambaye ameonesha uthubutu wa kukemea maovu yaliyokuwa yameshamiri hapa nchini.
Ili Tanzania isonge mbele hata tufikie katika huo uchumi wa kati, haina budi kila Mtanzania kutimiza wajibu wake kwa moyo wa uzalendo, na si kukosoa kila jambo ilimradi kila mtu aonekane anajua kuliko mwenzie.
Wanasiasa wa vyama vya upinzani acheni kuwa na roho zilizojawa na hamu na maombi ya kuiombea serikali ishindwe mpate mashiko katika uchaguzi ujao.
Hivyo mtakuwa na malengo ya kushika dola tu na si kutaka Tanzania iendelee. Kwani Nchi inaweza endelezwa na yeyote na chama chochote.
Nahitimisha kwa kusema nchi ilipofikia haitaji tena siasa wala kubembelezana, sasa twende kwa mwendo wowote ikibidi hata kukimbia ilimradi tufike.