Watu hawakumuelewa Rais Magufuli

Watu hawakumuelewa Rais Magufuli

Nimekuwa nikiongea na wewe kwa muda mrefu nikidhania kuwa naongea na mtu mwenye akili timamu, kumbe naongea na punguani anayetembea uchi barabarani. Mwenye high standards hawezi kuwa na fantasy zake kichwani kuhusiana na rais. Reality tuliyonayo ni kwamba rais wa awamu ya tano ni JPM, iwe unataka au hutaki.

Huo mchezo wa kutiwa vidole sehemu ya kujambia, inaonekana unafanyiwa sana huko mitaani kiasi ambacho huna hata aibu za kistaarabu, unamwaga siri zako hadharani. Nyinyi ndio wasomi wa mijini, hopeless generation, mkishapata degree zenu za magumashi mnaona kama vile mmeshakuwa na uelewa wa kipekee kuhusiana na kila issue. Mnaanza kuwadharau babu na bibi zetu wanaoishi vijijini kwa sababu ya maisha artificial mnayoishi Dar. Mnasahau kwamba kama wangeamua kutowasomesha wazazi wenu leo hii mngekuwa mnatembea uchi huko vijijini mkiwa hamna matumaini yoyote ya maisha yenye neema. A bunch of bastards.
Kwamba JPM ni rais haimaanishi tumuimbie utakatifu asiokuwa nao. Hata yeye mwenyewe haitamsaidia.

Na tukisema ni straightforward wakati kapinda kuliko mizengwe ya Mizengo tutadhihirisha upunguani.

Kusema kwamba Watanzania wengi ni illiterate hivyo huwezi kusema wamemchagua mtu kwa kujua si dharau, ni ukweli.

Hata ukitaka kupiga mbiu gani, huwezi kubadili ukweli kwamba mtu aliyeuza nyumba za serikali kwa kaka yake na kimada wake kinyume na utaratibu ni "straightforward".
 
Habari wana JF
Jana Rais Magufuli aliwahutubia kwa muda mfupi wakuu wa mikoa baada ya kuwaapisha. Rais aliongea mambo machache lakini yaliyobeba maana kubwa kuhusu uwajibikaji na watu kufanya kazi hasa akitia msisitizo kuwa tumeshachelewakwa kuwa haya yalitakiwa kuanza miaka kumi iliyopita.
Ni ukweli uliyodhahiri kuwa tumechelewa tena sana kutokana na nchi yetu iliyojaliwa kuwa na raslimali nyingi pamoja na ardhi kubwa yenye rutuba.
Jambo la kushangaza watu wameibuka na kauli mbalimbali wakiwemo wanasiasa, ambazo zimebadili maana halisi iliyokuwa kwenye baadhi ya maneno ya Mh. Rais.

Mh. Rais aliwaambia ma-RC "kuna watendaji wengine kazi yao ni kuwanyanyasa wananchi nendeni mkawashughulikie. Nyinyi mna mamlaka ya kumweka mtu ndani masaa 48, wawekeni ndani ili wawaheshimu wananchi". Lakini kauli hii imepindishwa na watu, hata wengine wakisema wakuu wa mikoa wameagizwa waende kuwakamata vijana wasiokuwa na kazi!
Hivi kweli hawa wakuu wa mikoa ni watu wasiojitambua ambao wanaweza kuitumia sheria inayowapa mamlaka hayo kuwaonea watu wasiokuwa na hatia?

Jambo jingine ambalo linapotoshwa ni kauli ya Rais kuzuia watu kucheza pool table asubuhi na kuwataka vijana kufanya kazi badala ya kuzurura pale alipokazia kuwa ikiwezekana walazimishwe kufanya kazi kwenye kambi maalum.
Watanzania wenzangu hivi ni kutokufuatilia sheria au ni upotoshaji wa makusudi? Niwaulize wanasheria akina Tundu Lissu, sheria inasemaje kuhusu muda wa kufungua bar na sehemu mbalimbali za starehe? Sheria inasemaje kuhusu uzembe na uzurulaji?
Mimi sioni kama mh. Rais ametunga sheria mpya ya kwake bali anasimamia sheria ambazo zilikosa usimamizi ambazo leo ni matokeo yaliyozalisha makundi ya vibaka mitaani.

Hapa Tanzania haiingii akilini kwa mtu anayejua hasa kutumia zile dutu nyeupe zilizo katika fuvu la kichwa ukimwambia hakuna kitu chochote cha kufanya kukuingizia kipato. Huko ni kukosa ubunifu na kuyaacha mambo yaende kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Katika nchi iliyo na ardhi zaidi ya 70% haijakaliwa na watu wala haimilikiwi na mtu. Ardhi ni mtaji wa kwanza kwa sababu juu ya ardhi ndipo kila kitu kinafanyika.

Kila Mtanzania aliye na akili timamu kutoka moyoni mwake ukiacha anachokisema mdomoni ili kuwahadaa, anajua kuwa sasa hivi vijana wengi wamekuwa wavivu hawataki kazi ngumu, wamekuwa ni watu wanaotaka kuvuna wasipopanda. Kiasilia hilo jambo halipo wala haliwezekani, hata Simba porini anapambana kupata mawindo.

Rai yangu kwa Watanzania wenzangu, acheni kupotosha maana halisi ya maneno ya Mh. Rais ambaye ameonesha uthubutu wa kukemea maovu yaliyokuwa yameshamiri hapa nchini. Ili Tanzania isonge mbele hata tufikie katika huo uchumi wa kati, haina budi kila Mtanzania kutimiza wajibu wake kwa moyo wa uzalendo, na si kukosoa kila jambo ilimradi kila mtu aonekane anajua kuliko mwenzie.
Wanasiasa wa vyama vya upinzani acheni kuwa na roho zilizojawa na hamu na maombi ya kuiombea serikali ishindwe mpate mashiko katika uchaguzi ujao. Hivyo mtakuwa na malengo ya kushika dola tu na si kutaka Tanzania iendelee. Kwani Nchi inaweza endelezwa na yeyote na chama chochote.

Nahitimisha kwa kusema nchi ilipofikia haitaji tena siasa wala kubembelezana, sasa twende kwa mwendo wowote ikibidi hata kukimbia ilimradi tufike.
Huyu mtu haongei kwa mafumbo. Alisema, tulimsikia na tulielewa alichosema. Wewe ndio unataka kupindisha. Kama unafikiri kwa mtazamo wako amekosea just say so. Usijaribu kuwaaminisha kutuaminisha vinginevyo.
 
Kwamba JPM ni rais haimaanishi tumuimbie utakatifu asiokuwa nao. Hata yeye mwenyewe haitamsaidia.

Na tukisema ni straightforward wakati kapinda kuliko mizengwe ya Mizengo tutadhihirisha upunguani.

Kusema kwamba Watanzania wengi ni illiterate hivyo huwezi kusema wamemchagua mtu kwa kujua si dharau, ni ukweli.

Hata ukitaka kupiga mbiu gani, huwezi kubadili ukweli kwamba mtu aliyeuza nyumba za serikali kwa kaka yake na kimada wake kinyume na utaratibu ni "straightforward".
Mungu akubariki ndugu yangu, nakutakia jioni njema.
 
Huyu mtu haongei kwa mafumbo. Alisema, tulimsikia na tulielewa alichosema. Wewe ndio unataka kupindisha. Kama unafikiri kwa mtazamo wako amekosea just say so. Usijaribu kuwaaminisha kutuaminisha vinginevyo.
Hebu ipitie upya utaona ukweli wa nilichokisema
 
Sasa hayo maendeleo mnayoyataka yatakuja kwa watu kucheza pool table na betting huku ardhi ikiendelea kustawisha majani?
Acheni kujitia upofu wakati hali halisi mnaijua,vijana wamekimbia vijijini baada ya kuona kilimo hakina tija serikali ilipaswa iandae mpango kazi unaotekelezeka was kuwa kwamua vijana kiuchumi,Lowassa alipo sema ataanzisha bank ya kusaidia Bodaboda na mama lishe alilenga kundi kubwa la vijana ikiwemp hao jobless wanaocheza kamali na pool asubuhi
 
Watu wamepotosha kuhusu ni nani Rais aliongelea anaweza kuwekwa ndani.
Kwa hiyo kwa kuwa kuna watu wanafanya kazi usiku na kuwa free mchana basi waruhusiwe kuingia baani asubuhi? Je, atapumzika saa ngapi?
Hiyo sheria katika nchi yetu bado haijapitwa na wakati.
Kwa hiyo kama mnahitaji wapumzike, je mmeshawapangia muda wa kupumzika kuwa iwe ni saa ngapi hadi saa ngapi?
 
Acheni kujitia upofu wakati hali halisi mnaijua,vijana wamekimbia vijijini baada ya kuona kilimo hakina tija serikali ilipaswa iandae mpango kazi unaotekelezeka was kuwa kwamua vijana kiuchumi,Lowassa alipo sema ataanzisha bank ya kusaidia Bodaboda na mama lishe alilenga kundi kubwa la vijana ikiwemp hao jobless wanaocheza kamali na pool asubuhi
Mkuu unamaanisha Tanzania siku hizi hakuna watu wanaolima, au wanaonufaika na kilimo?
 
Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Au unaota ndoto tu kwamba mungu yupo kama unavyoota kwamba Magufuli ni "straightforward" ?
Haya ni maongezi tu sio ugomvi, maana naona mihemko inatuzidi nguvu, povu linatutoka kwa sababu ya kumuongelea mtu ambaye nina uhakika hanijui mimi wala hakujui wewe. Hayo mambo ya kumuongelea Mungu ni ya kiimani na sio mada inayoendelea.
 
Kwa hiyo kama mnahitaji wapumzike, je mmeshawapangia muda wa kupumzika kuwa iwe ni saa ngapi hadi saa ngapi?
Mimi sijaelewa hapa mnapinga nini! Vijana kuambiwa kufanya kazi au?
 
Vijana wavivu wavivu wale wasiopenda kazi, asubuhi asubuhi wanacheza Pool table kamata wote peleka mashambani. Wale wanaoshinda kwenye vibanda umiza asubuhi mpaka jioni wakiangalia filamu za kihindi kamata wote peleka mashambani. Wale wavuta bangi na vibaka wanaoshinda vijiweni kamata wote peleka mashambani. Ni amri sio ombi...hapa kazi tu!
Wewe unawaza hili sasa. Lakini hujui yalishafanyika miaka iliyopita na matokeo yake yalikuwa 0. I wish nchi ingekuwa rahisi hivyo kuongoza kwani ungekuta tuna maendeleo kibao. Mimi sipendi uvivu na najua watanzania wengi ni wavivu lakini hii njia haifanyi kazi...
 
Haya ni maongezi tu sio ugomvi, maana naona mihemko inatuzidi nguvu, povu linatutoka kwa sababu ya kumuongelea mtu ambaye nina uhakika hanijui mimi wala hakujui wewe. Hayo mambo ya kumuongelea Mungu ni ya kiimani na sio mada inayoendelea.
Unaweza kuona ugomvi na mihmko kutokana na ugoigoi wa fikra zako tu.

Kwa udogo na ugoigoi wa fikra zako, unachoishia kuona hapa ni kwamba tunamzungumzia mtu, huoni zaidi ya hilo.

Sasa kama tunaongelea mtu asiyekujua wewe wala mimi unapata wapi hoja ya kunijibu mimi kwa jambo kama hilo?

Kama mambo ya kumuongelea mungu si mada inayoendelea mbona umeyaleta?
 
Goi goi wa fikra ni wewe unayeleta matusi jukwaani wakati maongezi yalikuwa ni ya kiungwana, na huu ni udhaifu mkubwa sana wa wasomi wa miaka hii ya karibuni. Mmepewa uhuru mwingi kwenye malezi matokeo yake ndio haya, unatukana matusi ambayo sisi tuliyatukana tulipokuwa primary school miaka zaidi ya 30 iliyopita!!.

Waliomchagua JPM wanazo criterias zao na kadri muda unavyokwenda utendaji kazi wake utathibitisha kuwa lilikuwa ni jambo la busara kumpa nafasi ya kuiongoza nchi hii. Hizo fantasies ulizonazo kichwani kwako, utaendelea kubaki nazo lakini tunaoitazama Tanzania halisi tunamtambua rais JPM.
 
Penye mfano mujarab wenye ashakum, wewe uliyekosa upembuzi mwenye fikra goi goi utaona tusi tu.

Uungwana na utwana ni dhana ya dunia iliyopita.

Mimi hata sijasema kwamba ni msomi, licha wa miaka hii ya karibuni. Hilo umelipata wapi? Au unaota tu kama unavyoota kwamba Magufuli ni straightforward na kuna mungu?

Nchi ya watu wasio na elimu haichagui kiongozi, inachaguliwa tu. JPM kachaguliwa na kitengo, wananchi ni rubber stamp tu.
Ndiyo maana Tanzania hakuna primaries.

Fantasy uliyotuonyesha hapa ni kwamba mtu aliyeuza nyumba za serikali kinyume cha taratibu kwa hawara yake na mdogo wake, watu ambao hata hawakuwa wafanyakazi wa serikali, ni "straightforward".
 
..Raisi anakosea kutoa kauli za VITISHO.

..pia kuwahimiza ma-rc na ma-dc kuwasweka mahabusu kwa masaa 48 watendaji wa serikali kunaweza kusababisha uonevu kwa wananchi wasio na hatia.

..zaidi utaratibu na pilikapilika za kukamata vijana wasio na kazi siyo jambo jipya hapa nchini. But one thing has remained constant, utaratibu huo haujawahi kutatua tatizo la uzururaji ambalo linasababishwa na ukosefu wa ajira.

..uchumi wetu, kutokana na sera mbovu za ccm, hauzalishi ajira za kutosha na zinazovutia kwa vijana wetu na hi yo kusababisha wazurure mitaani. Sijui kama unakumbuka tukio la vijana kujaa uwanja wa taifa wakati idara ya uhamiaji ilipotangaza nafasi za kazi.

..kwa hiyo Raisi na watendaji wake warudi kwenye drawing board na kuja na mikakati ya kupambana na tatizo la UKOSEFU WA AJIRA.
Watanzania wengi hatuna kumbukumbu na huwa hakuna maandishi mengi kuhusu Tanzania ya miaka ya nyuma na yaliyopo kidogo watu hatusomi. Haya mambo ya kukamata wazururaji yalikuwepo sana. Watu walihamishiwa mpaka kwenye vijiji vya ujamaa kwa nguvu! Na utendaji wa aina ya Magufuli sio mpya. Mrema alikuwa maarufu na anasifiwa kuliko Magufuli. Kwa kifupi Magufuli anaongoza kwa staili ya miaka ya nyumba ambayo mafanikio hayakupatikana. Ngoja niwaache na kibao cha Urafiki Jazz Band cha Gezaulole. Kipindi hicho ndicho ''wazururaji'' wanakamatwa kweli kweli. Polisi wakipita wanakusanya makundi ya vijana wasio na vitambulisho halafu wanawatoa kitu kidogo na kuwaachia.
 
Penye mfano mujarab wenye ashakum, wewe uliyekosa upembuzi mwenye fikra goi goi utaona tusi tu.

Uungwana na utwana ni dhana ya dunia iliyopita.

Mimi hata sijasema kwamba ni msomi, licha wa miaka hii ya karibuni. Hilo umelipata wapi? Au unaota tu kama unavyoota kwamba Magufuli ni straightforward na kuna mungu?

Nchi ya watu wasio na elimu haichagui kiongozi, inachaguliwa tu. JPM kachaguliwa na kitengo, wananchi ni rubber stamp tu.
Ndiyo maana Tanzania hakuna primaries.

Fantasy uliyotuonyesha hapa ni kwamba mtu aliyeuza nyumba za serikali kinyume cha taratibu kwa hawara yake na mdogo wake, watu ambao hata hawakuwa wafanyakazi wa serikali, ni "straightforward".
Unaongea maneno yale yale yenye ujumbe ule ule. Kitengo kilichotupatia Magufuli kibarikiwe sana kwani kimelipatia taifa mtu sahihi katika wakati sahihi.

Wewe ni msomi typical, ni aina ya watu wanaopenda sana kuwa negative kwenye maongezi, aina yako wewe wamejaa jijini Dar, watu wenye kuidharau asili yao, wenye kuwatusi wazee wao walio vijijini huku wakisahau kwamba wanapofariki na kusafirishwa kwenda kuzikwa kwao walipozaliwa, wale wanaofanya kazi ya kuwachimbia makaburi na kusikitishwa na vifo vyao, ndio hao hao ambao hawajasoma!.

Nchi wa watu wasio na elimu ndio iliyowaleta ulimwengu wazazi wako na wa kwangu. Afrika nzima haina primaries, mawazo yale yale ya wasomi wa mijini. Afrika ina safari ndefu sana na vizazi vitakavyolikomboa bara letu, vitafanya hivyo wakati sisi tukiwa makaburini, miaka mingi ijayo. Marekani ilipata uhuru mwaka 1776 miaka 240 iliyopita, nchi za Afrika zina miaka isiyozidi 60 ya uhuru, kwa hiyo bado tuna safari ndefu sana.
 
Futeni katiba na uchaguzi basi, rais achaguliwe na kitengo na kutawala kisultani.

Ya nini kupoteza hela nyingi kwenye uchaguzi na kuhadaa ulimwengu?
 
Back
Top Bottom