Watu aina ya Robert Heriel wanahitaji wanawake wa kipekee mno

Watu aina ya Robert Heriel wanahitaji wanawake wa kipekee mno

Tatzo mambo ya mahusiano Huwa hayatabiriki,
Ujanja mwingi ni sababu hajapata KE anaemuelewa[emoji4]
Kabisaaa. Kwanza kuchamba kwingiii kutoka na nnya.

Unless kama mtu anaweza kumuumba mtu mwenye vigezo avitakavyo
 
Unamuomba Mungu akupe mke au mme shetani anawahi timing anakupa wa kwake, kifuatacho ni ndoa ndoano.
Hakuna utii, Hakuna heshima, kifuatacho ni upendo kufa kabisa, inabakia ndoa mfu, ndio zilizo nyingi kuachana mnaogopa watoto, ndugu, marafiki, kugawana mali, nk mnabakia kugawana vyumba tu.
 
Mambo huwa ni tofauti kabisa, yani cha ajabu huyo robert ataseto, atatulia, na kuendeshwa na mwanamke wa kawaida sanaaaa yani kawaida kuanzia kichwani hadi mwili, nakuhakikishia hata takko atakua hana....
 
1 Coríntios 7
1 Yahusu sasa mambo yale mliyoandika: naam, ni vizuri kama mtu haoi;

2 lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.

3 Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe.

4 Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo.

5 Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribu kwa sababu ya udhaifu wenu.

6 Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, si amri.

7 Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmoja anacho kipaji chake kutoka kwa Mungu; mmoja kipaji hiki na mwingine kile.

8 Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo.

9 Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.

10 Kwa wale waliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mke asiachane na mumewe;

11 lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.
 
Utatukanwa na kuchukiwa shauri yako.
Hata hivyo Jambo moja katika Hii Dunia.
Wengine wanaweza kukuona unaakili na hapohapo kuna wengine watakuona hamnazo. Hivyo ndivyo Dunia ilivyoumbwa Mkuu. Ili kuweka mambo katika msawazo
Kabsa mkuu hakuna haja yakufanya jambo ufurahishe kundi fulani , ww ishi kwa uhalisia wako kuna watu wengne watakua sawa na ww na wengne hawatakua sawa , hi dunia usipokuwa imara utajikuta asilmia 50 ya maisha yako unaishi maisha ya Watu wengne.
 
Wote huwa malaika kabla ya ndoa, wanawake ni comedian wazuri watakapo jambo lao sio chuoni, kazini, kupalilia ndoa.
Huwezi jua tabia ya mtu hadi uishi nae.
Akiwa comedian awe real ata jua mwenyewe cha msingi ni kuwa na msimamo usioyumbishwa kama mwamba , anae fit apo atatulia apo ,asiye fit apo atajikataa mwenyewe tu.
 
Akiwa comedian awe real ata jua mwenyewe cha msingi ni kuwa na msimamo usioyumbishwa kama mwamba , anae fit apo atatulia apo ,asiye fit apo atajikataa mwenyewe tu.
Hio ni kuoa kuacha kuoa kuacha hadi utampata atakaefiti
 
Kabsa mkuu hakuna haja yakufanya jambo ufurahishe kundi fulani , ww ishi kwa uhalisia wako kuna watu wengne watakua sawa na ww na wengne hawatakua sawa , hi dunia usipokuwa imara utajikuta asilmia 50 ya maisha yako unaishi maisha ya Watu wengne.

Ni kweli Kabisa.
Nipo kwaajili ya wale tunaofanana.
Siku zote njiwa hutembea na njiwa, kunguru Kwa kunguru.
Siwezi lazimisha uvuguvugu au uchotara ili ati niyapate makundi yote.
Wale tuliokundi moja watanielewa.
 
Mkuu upo sahihi sna , nashangaa sana inakuaje mtu na akili Zake, anafunga ndoa na mwanamke mjinga mjinga asiyejitambua ! Mwisho wa siku ni kulia lia huku mitandaoni , akitafuta ushauri .
Unazungumzia akili gani? Mke wa Nikki wa pili alikuwa sio mjinga mjinga alikuwa best student kwa CPA Tanzania nzima lakini mwisho wa siku akaja kugawa uchi kizembe tu mpaka kupelekea mahusiano yao kuvunjika.
Kifupi ni hivi hauwezi kupata kitu kilichokamilika bila kuwa na kasoro nature ndio ipo hivyo....unaweza kupata mwanamke mwenyewe akili za darasani lakini katika maisha/maendeleo asiwe na msaada wowote,unaweza kupata mwanamke mkali+elimu+kipato kumbe engine ilishakufa kitambo tu.
Katika mahusiano/ndoa tanguliza MUNGU kwanza ukitanguliza utashi wako binafsi utaumia tu
 
Habari za Jumatano hii! Leo nilikuwa na tafakuri nzito kuhusu personality ya watu kama R. Heriel humu jamiiforam. Si Robert tu, kuna huyu mtu anaitwa Wyatt Mathewson pia.

Nilichojifunza kuhusu watu wa kariba hii ni;
1. Wanahitaji wanawake wasomi ili waweze kueleweka. Watu kama Huyu taikon kwenye jamii zetu za kiafrika mara nyingi huwa hawaeleweki kutokana na upeo duni wa waafrika wengi. So wanaitaji wanawake wasomi haswa siyo wa kubabaisha.

2. Wanahitaji wanawake wasiopenda bata na mambo ya kipuuzi. Watu kama Taikon wanaitaji wanawake wasiyo na upuuzi upuuzi. Wakati wa utani ni utani wakati wa kazi ni kazi. Wanawake wengi wa uswazi type ya wanaume km taikon atawaua. Hawatowezana.

3. Wanaitaji wanawake wapole but charming too. Watu wa kaliba ya taikon ni wakali kwa asili. Hivyo wanawake wengi wa sasa walio jeuri,wajuaji na viburi hawatowezana kabisa na wanaume wa kariba hii. Wanaitaji wanawake wa kujishusha.

4. Mwanamke anayeolewa na mwanaume wakaliba ya taikoon anatakiwa awe mvumilivu sana, but bright!akiwa lofa lofa atakufa kabla ya wakati wake.

Kwa sifa hizo nne,wanawake wa kaliba ya wanaume km taikon wapo wachache sana TZ na afrika kwa ujumla. Hivyo mara nyingi watu wa kaliba hii hupata shida mno kudumu kwenye mahusiano mapya mara baada ya break up. Hii ni miongoni mwa changamoto kubwa kwa watu wakaliba hii ya taikon.

Wengi slay quens wa insta,watsap,fb,tiktok,twita nk hawawezi kuvumilia vurugu za akina taikon wa fasihi. Wataona wanaonewa,wataona hawajaolewa na romantic men,wataona wanaendeshwa na mfumo dume na kadhalika.

Kama ambavyo masikini ni wengi na matajiri wachache,basi vivyo hivyo wanawake wenye akili ni wachache na malofa niwengi,na ndo hao waloolewa na wanaume wengi.

Mwisho, ukiwa lofa oa lofa mwenzio,ukiwa mjanja oa mjanja mwenzio,ukiwa tajiri oa tajiri mwenzio au uchumi wakati
Matajiri wanapokataa watoto wao kuolewa na malofa haimaanishi wanaweka ubaguzi nooo. Ndivyo inavyotakiwa kuwa.

NB; samahanini ikiwa taikon na wyatt hamjapenda kutumia majina yenu.
Hope nimefikisha ujumbe na niko ready for criticism
Kuna vitu kwenye maisha ukivichukulia serious sana hautoboi
 
Unazungumzia akili gani? Mke wa Nikki wa pili alikuwa sio mjinga mjinga alikuwa best student kwa CPA Tanzania nzima lakini mwisho wa siku akaja kugawa uchi kizembe tu mpaka kupelekea mahusiano yao kuvunjika.
Kifupi ni hivi hauwezi kupata kitu kilichokamilika bila kuwa na kasoro nature ndio ipo hivyo....unaweza kupata mwanamke mwenyewe akili za darasani lakini katika maisha/maendeleo asiwe na msaada wowote,unaweza kupata mwanamke mkali+elimu+kipato kumbe engine ilishakufa kitambo tu.
Katika mahusiano/ndoa tanguliza MUNGU kwanza ukitanguliza utashi wako binafsi utaumia tu
Mkuu utashi wangu alinipa Mungu ukiwa umekamilika ili niutumie , katika kila jambo natanguliza utashi wangu kwanza , kama njia ya kutukuza kazi ya Mungu .
 
Kwa Dunia hii ya Sasa au TZ yetu hii suala la Mwanamke bikra tulitoe kabisa akilini sisi wanaume.. Ety unataka Mwanamke msomi kuanzia Diploma then awe na bikra, Tabia njema.
Hizi mambo hazipo kwa Sasa bikra nyingi zinatolewa huko mavyuoni..
Binafsi nikipata Demu wa level yoyote ya elimu ni mzuri na mweupe hapo then atakubali kuishi na mm hapo kazi imeisha Dadeq😂
 
😄😄😄😄
Mkuu umenifurahisha Sana.
Kwanza nikupe pongezi kwa sababu umepatia Kwa 90%.

Sifa ya Mwanamke ambaye anaweza kuwa MKE wa Watu dizaini yetu, yaani Watibeli, au Bob Senior ni kama ifuatavyo;

1. Awe mwanamke mzuri mwenye sifa za kike.
i) uzuri WA maumbile, sura, rangi,
ii) Uzuri wa Tabia,
iii) lazima nikukute Bikra. Watibeli ni sheria kuoa Bikra na sio vinginevyo.

2. Awe Mwanamke Msomi
Elimu Dunia na Dini ni lazima, uwe na kiwango cha kutosha cha Elimu sio pungufu ya Diploma.
Kukosa sifa hiyo hauwezi kuwa kwenye hesabu za kuwa MKE wa Watu dizaini yetu.

3. Wanawake wenye AKILI
Akili ya kike, kujua Haki zake, Haki za wengine, na haki za mazingira.
Hatupendi Wanawake wajinga wenye Akili za kitoto na midoli.
Tunawajua Wanawake wenye Akili kwa namna wanavyotumia Uhuru wao, na vile wanavyotambua nafasi zao na zawengine.

4. Tunapenda Wanawake wanaojitegemea.
Tunapenda Wanawake heavyweight, ambao unaweza ukampa majukumu na bila ya kumuwekea wasiwasi.
Tabia Hii tunaweza kuwafundisha Wanawake wetu ikiwa tukagundua Hawana huo uwezo.

5. Wanawake wenye uwezo wa kuvunja mahusiano ikiwa wataona Haki haifanyiki.

Kimsingi Sisi Watibeli ni ngumu kuingia kwenye mahusiano hasa ya Ndoa Kwa sababu Wanawake wengi hawa-fit na mifumo yetu.

Sifa zetu Bora;
1. Tunajua kupenda na tunajali mno.
2. Tunapenda Haki, na kila kitu tunakipeleka kwa Haki.
3. Wanawake zetu tunawachukulia kama Malkia.
4. Tunato Uhuru na tunaishi bila kuigiza, na tunataka wake zetu waishi Kwa Uhuru na bila kuigiza.
5. Hatujali mambo madogo Dogo, hivyo hatuna Kisirani.
6. Tunaishi kishkaji na Wake na watoto wetu Kwa sababu tayari tumeshaweka mfumo a kila MTU anajua mipaka yake.
7. Sisi ni wacheshi na watu wa Sanaa.

Madhaifu yetu;
1. Ni wepesi kufanya maamuzi magumu bila kuangalia matokeo hasa heshima zetu zinapovunjwa.
2. Hatunaga msamiati Msamaha Kwa Makosa makubwa kama usaliti, Uchawi na ushirikina.
3. Tunajua mambo mengi Jambo ambalo linaonekana tuonekane wajuaji.
4. Tunaposema Jambo ndio ni ndio na hapana na Hapana.
5. Tunadharau Watu hasa tuliowaweka kwenye kundi la Watu wajinga.
7. Sisi ni wabaguzi hasa kwenye ishu sensitive kama Ndoa na kuanzisha mahusiano.
Sio rahisi kufanya ngono na kila Mwanamke. Tunakinyaa.

Kwetu ni Bora mara elfu kuishi bila MKE ikiwa hakuna Mwanamke anaye-fit vigezo vyetu

Wasalamu
Kuna jamaa mmoja ni msomi kwe
Hivyo ndio vitu tunavyomiliki Boss.
Kisichowezekana kwako Kwa wengine ni kama uji tuu😄😄
🤔🤔 kutokana na reply zako tu nime analize mambo machache muhimu.

1. Haujawahi kuwa kwenye relationships nyingi (sisemi watu wawe wana date kabla ya ndo).

2. Una maturity ndogo sana tukija kwenye suala la mapenzi, maana bado upo kwenye immagination phase ambayo wanayo wale watoto wanaobaleghe ila ukija kwenye reality ni tofauti kabisa NO OFFENCE!

3. Wewe ni very self centered person, egoistic na una selfish personality hii inaweza kuwa imechangiwa na mambo haya machache ambayo yanawapata vijana wengi sana duniani LABDA ni kwa sababu Umesoma, au umepata maendeleo ukiwa na umri mdogo (speculation) , hayo mambo yoote huwa hayana uhusiano na mapenzi but ukiforce kuyaingiza nothing good will happen.

USHAURI
Jaribu kutofautisha ndoto na uhalisia .

AND AGAIN
No offence ! Take this as constructive criticism.
 
Ndoa ni ibada na ndoa si kwa kila Mtu.
Hakuna dhambi kutooa, unaweza ukaishi mseja yaani bila mke lakini usizini.
Mwanadamu aliyekamili anaweza ishi bikira maisha yake yote bila ngono na asipate madhara yeyeto kiafya au kisaikolojia.
Tamaa ya ngono ni ishu ya mind na sio mwili. Mind ndio Ina control mwili. Na mwili unayo njia yake ya asili ya kucontrol hisia, tamaa ya ngono.
Kujichua, uzinzi, nk hizi ni matokeo ya tamaa.
 
Back
Top Bottom