Watu 20 wahofiwa kufariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mjini Nzega, leo Oktoba 21, 2023

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,451
9,374
Ajali Uchama Nzega: Basi la Alpha limegongana na lori la GBP.
1607753903.jpg
-1425393417.jpg
-1178587037.jpg
-222352854.jpg

===

Watu 20 wanahofiwa kufariki baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mjini Nzega.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo leo Jumamosi Oktoba 21, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la Alpha linalofanya safari zake kati Shinyanga na Dar es Salaam na kwamba wakati wa ajali, lilikuwa likitokea Shinyanga.

"Nimepata taarifa hiyo na sasa ndio naelekea eneo la tukio na taarifa kamili nitaitoa baada ya kufika na kujua hali ilivyo," amesema.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai amesema amepata taarifa ya ajali hiyo akiwa wilayani Sikonge katika maadhimisho ya miaka 100 ya Hospitali ya Misheni
inayomilikiwa na Kanisa la Moravian, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian.

Amesema baada ya baada ya kupata taarifa hiyo ameelekea kwenye eneo la tukio.

Hii ni ajali kubwa kuua idadi kubwa ya watu katika Mkoa wa Tabora kwa mwaka huu.

Mwananchi
 
Alfa ya Mwanza-Dar imepata ajali kwa kugongana uso kwa uso na Lori la Mafuta la kampuni ya GPB Nje kidogo ya Mji wa Nzega..,
Hali ya Abiria
Mpk sasa sina idadi kamili ya vifo Ila sio chini ya watu 7
IMG_2191.jpg



Kama una ndugu yako leo alikuwa anasafiri na Alfa kutokea Mwanza Piga simu Kumjulia Hali maana Hali ni mbaya..

Taarifa Kamili itatolewa na Mamlaka Husika...
 
Hapo kama sio kwenye kona au overtaking basi mmoja alikuwa kasi na ametanua. Kurudi kwenye saiti yake alishindwa ikabidi viumane tu
 
Back
Top Bottom