Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lizzy nilipata bahati ya kuona picha za huyo mtoto aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakavimba in short ni kwamba hizo picha zilikuwa zinahuzunisha sana na zinatisha ni kama vile macho ya huyo mtoto yalikuwa yameliwa na wadudu tuwe na huruma na watoto jamani.Kila siku tunaongelea mapenzi tunasahau watoto....embu leo tuwe kifamilia zaidi.
Leo kuna kipindi nlikua naangalia kikanisikitisha sana.Kuna mwanamke yeye anamwadhibu mtoto wake kwa kumnywesha pilipili na kumuogesha maji baridi kabisa...wakati mwingine eti anamlisha sabuni.
Nikakumbuka wakati nakua kuna mtoto wa jirani yetu yeye alikua naishi na babu yake, siku moja aliachwa nyumbani alafu akaenda kucheza....babu yake alivyorudi alichofanya ni kumchapa alafu akamweka kwenye gunia lenye yale majani yanayowasha alafu akamtundika wakati chini moto unawaka.Yule mtoto alitoka mwekundu kama nini sijui....sikumbuki kama kuna jirani aliyethubutu kumkemea yule mzee.Nyingine tuliwahi kua na msichana wa kazi ambae alikua na mtoto wa zaidi ya mwaka mmoja.....ilikua tukiwa shule yule dada anamfunga mtoto wake kwenye mguu wa kitanda ili eti asimsumbue.Yule mtoto analia na kukojoa pale pale mpaka analala...tukirudi basi tunakakuta kamelala uvunguni.Anagombezwaaa ila tukiwa hatupo tu anafanya vile vile.
Bila kusahau wale watu wanaoishi na watoto wa wenzao pamoja na wa kwao alafu wanawatreat fofauti.Kuna baadhi ya ndugu zangu nimewahi kuishi nao wa aina hiyo.....unakuta wale watoto wasio na mtu wa kumlilia wananyanyaswa ila wale wakwao na wale wenye ndugu au wazazi wao wenye uwezo wanalelewa vizuri tu.
Na yule aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakageuka!!
Kusema kweli hizi hali zote zinasikitisha.Kuona mtu mzima anamnyanyasa mtoto kwa sababu yoyote ile na kwa kisingizo chochote kile haifai.Wengi wao hawana wa kumlilia na kushtaki sio kitu ambacho kinaweza kufanyika kirahisi kwasababu kitendo cha kumpeleka mzazi au ndugu anaekulea kwenye vyombo vya sheria mara nyingi itaongeza matatizo zaidi ya kupunguza..
Naomba niwaombeni wanajamii tuwe na huruma jamani.Awe mtoto wako...wa ndugu au jirani jaribu kutokua mnyanyasaji.Kama mzazi kua na ukaribu na mwanao ili hata kama kuna mtu mwingine anaemnyanyasa iwe shuleni, mtaani au nyumbani iwe rahisi kukwambia.Na kwa wale ambao wanaishi na watu ambao sio wazazi halisi wa wanao (mama na baba wa kambo) kua na tabia ya kuongea na mwanao kujua mambo yanayoendelea nyumbani ukiwa haupo.
Mateso ya utotoni hua yanaacha makovu mabaya sana....JALI NA KUA NA HURUMA huo ndo ubinadamu!
Lizzy hapa ndipo napokupendeaKila siku tunaongelea mapenzi tunasahau watoto....embu leo tuwe kifamilia zaidi.

Lizzy nilipata bahati ya kuona picha za huyo mtoto aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakavimba in short ni kwamba hizo picha zilikuwa zinahuzunisha sana na zinatisha ni kama vile macho ya huyo mtoto yalikuwa yameliwa na wadudu tuwe na huruma na watoto jamani.
Lizzy hapa ndipo napokupendea
Be blessed
Nakumbuka shuleni(msingi) tulikuwa tunafanyishwa kazi za bustani, kusomba tofali na nyingine nyingi eti elimu ya kujitegemea walimu wanakula mshiko usipofanya unakula SSS... Enzi hizo utasikia watoto wa walimu, afisa elimu, mtendaji walikuwa ni wagonjwa wa kudumu hivyo hawatakiwi kufanya kazi ngumu
Lizy umenikumbusha kipindi wazazi wangu walipofariki!!! jina langu lilibadilika na kuwa mbwa, nguruwe, masikini, fisi, paka mweusi ila namshukuru Mungu aliyejuu leo niliyekuwa paka mweusi nimekuwa dhahabu kwao wao!!
Nampenda Mungu Jehovah aliyenitoa chini na kuniketisha kitini na Wafalme, ama kweli yy huviinua vinyonge!!!
Ni vibaya sana kumfanyia mtu vibaya kwakuwa ww huijui kesho yake!!!
pole sana dearLizy umenikumbusha kipindi wazazi wangu walipofariki!!! jina langu lilibadilika na kuwa mbwa, nguruwe, masikini, fisi, paka mweusi ila namshukuru Mungu aliyejuu leo niliyekuwa paka mweusi nimekuwa dhahabu kwao wao!!
Nampenda Mungu Jehovah aliyenitoa chini na kuniketisha kitini na Wafalme, ama kweli yy huviinua vinyonge!!!
Ni vibaya sana kumfanyia mtu vibaya kwakuwa ww huijui kesho yake!!!
Aisee Susy hapo juu.
Nimesikitika sana wakati naisoma posti yako lakini mwisho wa posti nimefarijika sana.
Hatupaswi kulipa visasi...na kuitwa kwako mbwa, nguruwe nk labda niyo vimekufikisha hapo ulipo. Samehe na chapa mwendo.
Pole kwa kuwapoteza wazazi wako, na Mungu aendelee kukupa nguvu.
Babu Asprin amekupenda ghafla.
Umenikumbusha sababu nilijaribu kufuatilia kwa karibu hicho kisa, you can imagine huyo mtoto after that incident baada ya kupelekwa CCBRT ambao ndio wataalamu wa macho baada ya kumfanyia uchunguzi akaambiwa harusiwi kukaa kwenye jua inabidi pia akae sehemu ambayo hakuna mwanga mpaka apone sasa na huyu mtoto alikuwa anasoma atakuwa amekosa mambo mangapiFynest bwana!Kisa chakunipa picha asubuhi yote hii?Tena digito!Sijui aliyefanya hivyo aliionaje kazi ya mikono yaketa afterwards!
Pole sana SusyLizy umenikumbusha kipindi wazazi wangu walipofariki!!! jina langu lilibadilika na kuwa mbwa, nguruwe, masikini, fisi, paka mweusi ila namshukuru Mungu aliyejuu leo niliyekuwa paka mweusi nimekuwa dhahabu kwao wao!!
Nampenda Mungu Jehovah aliyenitoa chini na kuniketisha kitini na Wafalme, ama kweli yy huviinua vinyonge!!!
Ni vibaya sana kumfanyia mtu vibaya kwakuwa ww huijui kesho yake!!!
Umenikumbusha sababu nilijaribu kufuatilia kwa karibu hicho kisa, you can imagine huyo mtoto after that incident baada ya kupelekwa CCBRT ambao ndio wataalamu wa macho baada ya kumfanyia uchunguzi akaambiwa harusiwi kukaa kwenye jua inabidi pia akae sehemu ambayo hakuna mwanga mpaka apone sasa na huyu mtoto alikuwa anasoma atakuwa amekosa mambo mangapi
Hehe babu DC ntakwambia siri yangu siku nyingine!Pole kwa yaliyokukuta na hongera kwa kuwapenda wanao na kutaka kuwafunza kabla ya dunia!Kumchapa mtoto kama kunaendana na kiasi ni sawa kabisa!Mi nakumbuka marehemu bibi yangu aliwahi kunichapa mara moja tu tena kwasababu nilidanganya.Siku hiyo nilikasirika nikajiambia namchukia ila tangu siku hiyo nilichukia uongo!Sasa hivi hua nashukuru Mungu alinipa vile viboko maana vilinijenga na nnampenda sana kwa hilo!Kwahiyo babu tembeza viboko inapobidi!
Nimeona mambo mengi ila mengine ni aibu hata kuyasema ilihali wale wanayoyafanya wanaona ni sawa na kawaida tu God forbidSo unfair!Sijui watu huruma ya kibinaadamu wameuza kwa bei gani!