Watoto!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Mar 23, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kila siku tunaongelea mapenzi tunasahau watoto....embu leo tuwe kifamilia zaidi.

  Leo kuna kipindi nlikua naangalia kikanisikitisha sana.Kuna mwanamke yeye anamwadhibu mtoto wake kwa kumnywesha pilipili na kumuogesha maji baridi kabisa...wakati mwingine eti anamlisha sabuni.

  Nikakumbuka wakati nakua kuna mtoto wa jirani yetu yeye alikua naishi na babu yake, siku moja aliachwa nyumbani alafu akaenda kucheza....babu yake alivyorudi alichofanya ni kumchapa alafu akamweka kwenye gunia lenye yale majani yanayowasha alafu akamtundika wakati chini moto unawaka.Yule mtoto alitoka mwekundu kama nini sijui....sikumbuki kama kuna jirani aliyethubutu kumkemea yule mzee.Nyingine tuliwahi kua na msichana wa kazi ambae alikua na mtoto wa zaidi ya mwaka mmoja.....ilikua tukiwa shule yule dada anamfunga mtoto wake kwenye mguu wa kitanda ili eti asimsumbue.Yule mtoto analia na kukojoa pale pale mpaka analala...tukirudi basi tunakakuta kamelala uvunguni.Anagombezwaaa ila tukiwa hatupo tu anafanya vile vile.
  Bila kusahau wale watu wanaoishi na watoto wa wenzao pamoja na wa kwao alafu wanawatreat fofauti.Kuna baadhi ya ndugu zangu nimewahi kuishi nao wa aina hiyo.....unakuta wale watoto wasio na mtu wa kumlilia wananyanyaswa ila wale wakwao na wale wenye ndugu au wazazi wao wenye uwezo wanalelewa vizuri tu.
  Na yule aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakageuka!!

  Kusema kweli hizi hali zote zinasikitisha.Kuona mtu mzima anamnyanyasa mtoto kwa sababu yoyote ile na kwa kisingizo chochote kile haifai.Wengi wao hawana wa kumlilia na kushtaki sio kitu ambacho kinaweza kufanyika kirahisi kwasababu kitendo cha kumpeleka mzazi au ndugu anaekulea kwenye vyombo vya sheria mara nyingi itaongeza matatizo zaidi ya kupunguza..

  Naomba niwaombeni wanajamii tuwe na huruma jamani.Awe mtoto wako...wa ndugu au jirani jaribu kutokua mnyanyasaji.Kama mzazi kua na ukaribu na mwanao ili hata kama kuna mtu mwingine anaemnyanyasa iwe shuleni, mtaani au nyumbani iwe rahisi kukwambia.Na kwa wale ambao wanaishi na watu ambao sio wazazi halisi wa wanao (mama na baba wa kambo) kua na tabia ya kuongea na mwanao kujua mambo yanayoendelea nyumbani ukiwa haupo.
  Mateso ya utotoni hua yanaacha makovu mabaya sana....JALI NA KUA NA HURUMA huo ndo ubinadamu!
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Nimekosa cha kusema kabisa ngoja labda nitarudi maana nimesikia kama umetonesha kidonda
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  ehh iyo ya kuvutwa nyus mpaka majicho yakageuka kwa kweli DUU shetan anatamalaki
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kweli jamani.
  Halafu mateso kwa mtoto sio hadi umchape viboko, mi nakumbuka nilipokuwa mtoto walikuwa wananifungia ndani, hakuna kutoka nje. Tulikuwa hatuna housegirl na watu wote walikuwa na mishemishe kurudi hadi jioni.
  Dah, wapeni uhuru watoto wenu jamani.
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole mpendwa.....na samahani kama nimekukumbusha wakati mbaya!!!
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa....kitendo tu cha kumnyima mtoto kua mtoto ni mateso tosha!!Pole mwaya!
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  nishapoa ila hadi nimezeeka sijasahau. Lol!
   
 8. CPU

  CPU JF Gold Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mi napenda sana watoto
  Na ni kweli watoto wanateswa sana sanaaaaa

  Ila siku hizi sio watoto wote wanaweza kusema ukweli kwenye kila kitu
  Wapo watoto wajanja ambao wana tabia ya kuongeza chumvi kwenye maelezo yao au anatunga kabisa maelezo mapya
  Mimi nimeshuhudia mtoto wa darasa la 4 akimuweka mwalimu wake matatani aliposema kwamba sababu ya yeye kupewa adhabu ya kumwagilia bustani na kesho yake aje na mzazi wake ni kukataa kwake kukopa ubuyu aliokuwa anakopesha mwalimu.
  Mzazi alimjia juu mwalimu kesho yake akidai ananyanyasa mtoto wake. Hata mzazi alipoelezwa kwamba mtoto wake alikutwa anaandika mambo ya kimapenzi kwenye karatasi darasani mzazi alipinga kwa nguvu zote akidai mtoto wake hawezi kufanya mambo kama hayo.

  Angalizo hapa ni kwamba pamoja na huruma zetu kwa watoto na kusikiliza matatizo yao, pia tunapaswa kuchunguza nyendo za watoto wetu pia kubaini tabia zao zilizojificha. Watoto wa siku hizi wana mambo mengi sana, tusiwe wepesi wa kuamini kila wanachokisema.
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sipiyu tatizo sio wanachofanya au wanachosema ila ni adhabu tunazowapa!Kuna picha nimeona jana mtoto ameungua matakoni kwa kukalishwa kwenye jiko la mkaa!Hata kama huyo mtoto angekua ameua bado hastahili adhabu ya aina hiyo!Besides..mtu kama huyo aliyekutwa akiandika mambo ya kimapenzi alitakiwa kukalishwa chini akaelezwa kosa lake lilipo bila kusahau uwepo wa mzazi wake pale.Kuna mwl aliwahi kumchapa mwanafunzi mpaka mkono ukachanika..japo sikumbuki kosa lake ila nna uhakika halikua kubwa!
   
 10. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Dah,Lizzy acha tu dada yangu,mi nakumbuka utoto wangu nilikuwa napenda kweli kucheza mpira na kila ikifika muda wa ugali saa saba mi sina habari,hiyo ilikuwa mitaa ya sinza mwaka 1980,
  basi huyo mdogo wake mama aliyekuwa ameletwa kutulea alikuwa anatutembeza kwa magoti kwenye foundation ya nyumba iliyokuwa jirani mpaka magoti yanachubuka kisha unaogeshwa na kuvalishwa suruali ili usionekane ulivyochubuka na kwa sababu ya utoto unalia kimya kimya tu ukiogopa kuwa nikisema kipondo cha kesho kitazidi,jamani tuwasaidieni hawa watoto kwa kuwa baadhi yetu tumepitia huko.
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  POLE SANA MKUU. NASHUKURU KUWA ULIWEZA KUVUMILIA HADI KUKUA MKUBWA. WENGINE HUTESWA WAKAISHIA ULEMAVU WA KUDUMU AU KUPOTEZA MAISHA KABISA.

  Kila tulipo tujaribu kusaidia kuwafunza wazazi wenzetu juu la malezi bora ya mtoto. Adhabu kupindukia na mateso havimfunzi mtoto bali kumfanya awe sugu na akuchukie maisha.
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  pole sana mkuu
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  St. PM pole mpendwa!Dah...nakumbuka kaka yangu ye aliwahi kufinywa na mfanyakazi mpaka ngozi ikatoka!Akafukuzwa right away!Tatizo ni kwamba wazazi wengine ni wagumu kuongea nao kwahiyo hata mtoto kushtaki hawezi!
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  ahsante MAMMAMIA. una huruma kama jina lako.
  Juzi nilikutana na mtoto wa primary akaniomba nauli. Nikawa namdadisi kwanini amekula hadi nauli, akaniambia amepewa mia.
  Hivi jamani, hivi mzazi kama huyo anataka mwanae aende shule ila asirudi au!!
  Kweli watoto hawatendewi haki, mwingine ni wake wa kumzaa ila anavyomtreat acha tu.
   
 15. LD

  LD JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli watoto watunzwe vizuri, mi nakumbuka baba alikuwa mkali kiasi kwamba hata ukiwa mgonjwa huthubutu kusema mpaka uvizie baba hayupo ndo umwambie mama!!! Huwezi kuomba kitu chochote kwa baba hadi upitie kwa mama!!!! Hakuwa mlevi wala nini lakini ukisikia anaingia tu mnaacha kila kitu mnakimbilia ndani. Ukikosea unapewa adhabu ya kulima na unaogeshwa kwa maji ya baridi, au unachapwa hadi mama anakuja kukuamulia. Dah kuna siku alinichapa mbele ya wanafunzi wa darasa la nne na mwl wa hesabu akiwepo kisa nimepoteza daftari la hesabu, Dah nilizomewa na wanafunzi siisahau hiyo siku. Kuna wakati nilikuwa simpendi baba kabisa yani. But namshukuru Mungu baada ya kuwa na akili za kikubwa ninampenda tu vizuri.
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  dah! Mie nilijisahaulisha we umenikumbusha tena,dah! Mie utotoni ckuishi vzuri kwa kweli
   
 17. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  mmhh Lizzy,
  leo umenikumbusha mbali mpendwa.

  ni kweli inakaa na wewe milele..
  na inachangia sana na nini unafanya ukubwani..
  mara nyingi unafanya vitu ajili ya hasira au uwoga..

  mie sinta changia sana
  ni hayo tu
  bali asante sana mpenzi....
   
 18. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nikikumbuka nilivyoteswa na shangazi yangu nakosa cha kusema nimebaki na huzuni tu
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Poleee ntSamahani kwa kukumbusha bwana ila ushakua wewe kwahiwmwo jikaze kiume..fikiria wanaoteseka sasa hivi!
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole mpnz...hayo ndo maisha!Wakati mwingine inatufundisha pia ujue!
   
Loading...