Watoto wa vigogo na ajira BoT

Watoto wa vigogo na ajira BoT

Ni kigezo hiko na "kimemo cha mzazi wake" na kuonesha kadi ya rangi ya kijani ya Chama.

NIMEIPENDA IYO YA KADI YA KIJANI,
MI MTU MINAFIKI KM MARCOPOLO, RITZ, NA MENGINE YENYE KUSHABIKIA CCM ITAFURAI ATA KM WAJUKUU WA HAWA WATAKUWA WATAFANYA PIA BOT, CHEZEA MAPANDIKIZI WEWe
 
Aisee pole sana mlaumu mzazi wako kwa kuacha kuingia kwenye system mapema. Hata hivyo nakushauri uachane na mawazo ya kufikiria BOT wakati siku hizi kuna hadi saccos za kaya ambazo unaweza kupata kazi hapo.

Ni kitu ambacho hakiwezekani wote muwe kwenye system,,,kwahiyo wengine wasipate kazi sehem nyeti? Unanipa Wasiwasi kama ni Great Thinker au kila.za kama Nchimbi
 
Iko fresh tu, nan alimkataza mdingi wako asiingie kwenye system enzi hizo wenzie wanapigwa umande kwenda skonga yeye anajifanya mjasiriamali wa kuchoma mkaa jion anatesa kijijin kwa vijisent kutesa kwa Zamu, janga alochuma mdingi wako ndo hilo linakupanikisha mpaka unaanza umbeya wa kibwege! Onesha hawana vigezo sio kuleta bla bla, wewe na ki advance chako cha CBE au kidiploma cha Zoom unategemea upigwe na kipupwe cha Twin towers, Peleka CV yako Finca ndo levo zako!

Acheni kubwabwaja pumb*v zenu nie mnabebwa na baba zenu halafu mnajifanya mmesoma wavuta bangi hamna lolote wekeni CV zenu tuone kama zinawaruhusu kuwa BOT na vyeti vya kufoji! Watu wanawaangalieni tu, subirini 2015 mtanyea debe! We unakaa kumkashifu mzazi wa mwenzio unamjua? Acheni usng!
 
ile kesi ya watoto wa vigogo kugushi vyeti bot imeishia wapi mtoa mada yuko sahihi Tanzania ina watu zaidi ya milioni 45 haiwezekani watoto wa viongozi tu ndio wana uwezo wa kupata kazi sehemu nyeti hii nchi ni mali yetu sote
 
Wasubirie 2015,wataanza kuona watoto wa Slaa,Mbowe,zitto,Manyika na kuendelea.Maana inaonekana ukisha pata nafasi unaweka watoto kwenye position zenye afya.
Kwanini wasisimamie kampuni za babazao?
 
Ni kitu ambacho hakiwezekani wote muwe kwenye system,,,kwahiyo wengine wasipate kazi sehem nyeti? Unanipa Wasiwasi kama ni Great Thinker au kila.za kama Nchimbi

Mkuu nadhani umekurupuka tu kujibu haraka. Ungeupa ubongo nafasi ya kufikiri walau dakika mbili ungepeta idea ya ujumbe gani nataka kuufikisha mkuu. Sentensi yangu haipo direct kama ulivyoitafsiri.
 
Mitoto ya mafisadi!

Naam, wakitoka hapo wanapewa support ya kwenda kugombea ubunge kwenye majimbo ambayo wazee wao wametokea, wanapata ubunge ikiwezekana hata kwa kura za thermos. Baada ya kuukwaa ubunge wanateuliwa kuwa mawaziri, wanakuwa decision na policy makers. Kwa kuwa wengi wao ni vilaza, decisions na policies watakazotengeneza ni zile zisizo na vision ya kitaifa/kizalendo. Badala yake wanaendeleza cycle ya ufisadi na rushwa zilizowafikisha kwenye nafasi hizo. Matokeo ya haya yote ni poverty visious cycle kuendelea hapa Tanzania na hii ndo maana Tanzania ni maskini hadi leo mbali na utajiri wa mali asili ziliyopo. Decision making positions za nchi zimeshikwa na vilaza unategemea watapanga mipango gani ya maana kitaifa? Tusitarajie neema yoyote Tanzania kwa mfumo tunaoenenda nao sasa. Tafakari, chukua hatua.
 
Iko fresh tu, nan alimkataza mdingi wako asiingie kwenye system enzi hizo wenzie wanapigwa umande kwenda skonga yeye anajifanya mjasiriamali wa kuchoma mkaa jion anatesa kijijin kwa vijisent kutesa kwa Zamu, janga alochuma mdingi wako ndo hilo linakupanikisha mpaka unaanza umbeya wa kibwege! Onesha hawana vigezo sio kuleta bla bla, wewe na ki advance chako cha CBE au kidiploma cha Zoom unategemea upigwe na kipupwe cha Twin towers, Peleka CV yako Finca ndo levo zako!

Mkuu kwenye hiyo orodha wewe ni namba ngapi? Maana ulivyo react sina shaka kabisa kuwa nawe wahusika.
 
Wasubirie 2015,wataanza kuona watoto wa Slaa,Mbowe,zitto,Manyika na kuendelea.Maana inaonekana ukisha pata nafasi unaweka watoto kwenye position zenye afya.
Kwanini wasisimamie kampuni za babazao?

Badala ya kusimamia kampuni za baba zao wanasimamia kampeni za kisiasa za baba/mama zao wakati wa uchaguzi. Tanzania kazi ipo!
 
Kwanini mtumwa anadiriki kuhoji mambo yanayo mhusu bwana wake?
Jamani hao ndo wenye Tanganyika! Na ndio waliokua watawala wetu wa jadi katika maeneo yetu. Mwalimu alichokifanya Tabora pale sokoni palipojengwa mnara ni kuwaelezea namna mpya ya kutumia katika kuwatawala waTanganyika. Kwamba tutawapeleka watoto wetu shule na kulitawala koloni hili kisasa zaidi. Wewe mtoto wa mtumwa koma kuhoji mambo yamhusuyo bwana wako!!
 
Inamaana BOT nzima umewaona hao tu? Kuna wafanyakazi zaid ya 500 tanzania nzima ila hao 13 wamekupanikisha? Rudi class ukapate elimu.

Tatizo la JF huwa wana m-judge mtu bila kumjua....Wewe umejuaje kwamba jamaa hajasoma?
Ngoja nikufundishe:
Unasoma UDSM B.Com unapata lower second unaona haikufai ku-compete na labour market maana wanataka uwe na upper second au first class. Sasa kwa kuwa unaupeo mzuri kielimu unaamua kusoma degree nyingine ya uchumi. Unaamua kutafuta chuo chenye hadhi kubwa sawa na hao wakubwa wanavyosoma(ga). Unaanza kupambana na jinsi gani utapata hela ya kukusomesha Ulaya. Unapata pesa baada ya miaka mitatu. Unapata Oxford University UK. Unasoma miaka mitatu pale kujumlisha na practical inakuwa minne. Unapata merit (sawa na second class ya hapa bongo). Unaamua kuendelea na masomo kwa kufanya vibarua na dhiki kubwa sana ili tu urudi bongo na elimu nzuri. Unafanya Masters ya Public Finance inayokuchukua miaka miwili kuipata. Unafaulu vizuri. Kisha unarudi bongo kuitumikia nchi. Unaanza kutafuta kazi hapa bongo. Kwanza utaratibu wa kutafuta kazi bongo haueleweki.....Hakuna job centres ama recruitment agencies. Na zilizopo ni matapeli ama wanyonyaji. Unasubiri nafasi zitangazwe kwenye magazeti. Ndo siku moja (baada ya mwaka mmoja) unakuta nafasi za kazi zimetangazwa Benki Kuu. Mojawapo ya masharti yanakutaka uwe na umri wa miaka 30 tu. Sasa kutokana na wewe kuwa mtoto wa mkulima hukuweza kuanza darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka mitano. Ulianza ukiwa na miaka kumi!!! Sasa ukipiga mahesabu mpaka unamaliza masters yako huko UK (ingawa kutoka kwenye chuo maarufu sawa na wanaposoma watoto wa vigogo) wewe unakuwa "time barred". Yaani unakuwa umezidi umri!!!!! Sasa huyo mtu unayemshauri akasome tena ili iweje???? Akirudi si atakuwa na umri wa miaka 40? Ndo watamwambia "we need young and energetic personnel.....". Think critically!!!!!!
 
Sababu ni benki kuu, je mishahara yao ni tofauti na wafanyakazi wa mabenki mengine?
Nataka tu kujua kwanini wengi wanalalamikaga as nadhani nimeshaiona humu.
 
Mkuu kwenye hiyo orodha wewe ni namba ngapi? Maana ulivyo react sina shaka kabisa kuwa nawe wahusika.

Ame-react ili kuficha upande wa pili wa shilingi.....Maana tukitoka kwa watoto na wake wa vigogo wengine waliobaki tunahoji wanatokea mkoa gani. Asilimia 80 ya wafanyakazi wanatoka mkoa mmoja huko kwenye nyuzi fulani za joto lakini kama unaruka na ndege kwenda Ulaya ndo utapaona kwao.......
 
Kumbe mpaka usome Ulaya au America ndo upate ajira kwenye EPA?

Hakika Ndiyo!Unaweza kuweka mtu kama yule aliyesema pesa ya Tanzania haina thamani eti kwa vile haina picha ya Rais?Si ndo hawa waliosoma hapa Tz?Wengi Wana roho mbaya na majigambo tungekomaje?Aliyepewa kapewa tuacheni roho za kwa nini ili mradi wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni.Tunapaswa kukomaa na wabunge wetu tunaowatuma kutetea maslahi yetu halafu wao wanashirikiana na wanaotunyonya na kutukandamiza kwa kila hali!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
I DN THINK KAMA KUNA LOGIC SASA HAO WA VIGOGO ULITAKA WASPATE AJIRA...BoT Mbona ni ofsi ya kawaida sana mbona mleta mada anaikuza kuna mashrka kama TANAPA, TRA, NGORONGORO Mbona ata yanawafunika wa BoT baadhi ya vtengo...
 
ile kesi ya watoto wa vigogo kugushi vyeti bot imeishia wapi mtoa mada yuko sahihi Tanzania ina watu zaidi ya milioni 45 haiwezekani watoto wa viongozi tu ndio wana uwezo wa kupata kazi sehemu nyeti hii nchi ni mali yetu sote

Kama kawaida mkuu kesi ilishazimwa siku nyingi pale Kisutu na bado wapo kazini,,,akitoka hapo anahamishiwa Tanapa
 
I DN THINK KAMA KUNA LOGIC SASA HAO WA VIGOGO ULITAKA WASPATE AJIRA...BoT Mbona ni ofsi ya kawaida sana mbona mleta mada anaikuza kuna mashrka kama TANAPA, TRA, NGORONGORO Mbona ata yanawafunika wa BoT baadhi ya vtengo...

Hii ni baadhi tu hiyo sehem zippo nyingi sana mkuu hata mizani,,kuna jamaa nipo nae yupo Mizani Mikese ni mtoto wa kigogo ana miaka miwili kazini lakini ana nyumba 3 mbili za kawaida na 1 ni ghorofa ipo Mbezi Luguruni,kifupi humwangalii Mara mbili anavyong'aa kwa Rushwa.
 
Back
Top Bottom