Watoto wa vigogo BoT wasafishwa

WAKATI watumishi wengine tisa wa Benki Kuu (BoT), wakifunguliwa kesi mahakamani kwa kughushi vyeti, watumishi wengine 18, maarufu kama watoto wa vigogo waliodaiwa kuajiriwa kinyemela wamebainika kuwa na sifa stahili.

Wakuu naomba kusema hivi, hapa dawa kutafuta facts against haya maneno na kuziweka hapa, yaani tutafute ukweli wa elimu zao na CV zao ziwekwe hapa ili ukweli uonekane wazi kama kuna uongo na ukweli na hii habari,

Mana katiba ya taifa letu inawaruhusu hawa watoto wa viongozi kufanya kazi katika mashirkika yetu ya umma pia, lakini pia katiba hii haiwaruhusu kupewa nafasi hizo bila ya kwua na qualifications zinaotakuwa au kuingizwa wka ujanja ujanja, lakini ni lazima uwepo ushahidi kama kumefanyika faulo,

Sasa tuutafute na tuuweke hapa!
 
Ukweli ni mchungu kwenye hili, hao watoto wa vigogo wana nafasi kubwa ya kusoma vizuri kuliko watoto wa maskini. Kuna uwezekano mkubwa kwamba wana qualifications za kutosha lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba huenda waliingia pale kwa migongo ya wazazi wao.

Kuna wananchi chungu nzima wenye qualifications kama za kwao lakini iweje karibu kila kiongozi awe na mtoto wake BOT?

Uchunguzi unakuwa halali kama unajua unachochunguza, kuchunguza qualifications bila kuangalia ni wangapi wengine waliomba na ambao walikuwa na qualifications kama za kwao ni kupoteza muda tu.

Hapo tumefungwa goli lingine na pesa kibao zimetumika.
 
Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele mkuu, hukumu tuzitoe kwa ukweli na facts, kama kuna faulo zimechezwa huko tutafute ukweli, lakini tusihukumu kwa imaginations, kwenye EPa tunawajua wezi wetu for a fact, lakini kwenye hili tunasua sua,

Hebu tutafute ukweli kama hawa watoto wa viongozi waliajiriwa kwa faulo, maana tunakuabliana kua wananzo qualifications, lakini hatuna uhakika na kuajiriwa kwao, JF huwa tunakuwa na ukweli at hand ndio tunahukumu tena kwa standars zako mwenyewe, tusichukie wananchiw enzetu bila sababu za msingi!

Siuamini uchunguzi wa ndulu lakini siwezi kutoa hukumu nzito bila facts, ninawajua watoto wengi wa masikini ambao wapo BOT, kwa mfano mshikaji mmoja Mkulu Margai wa Imma alianzia huko na baba yake hakua kiongozi wa anything, tuwe fair japo kidogo
 
Excuse me sir... hivi watu walikuwa wanalalamika kuwa hawakusoma vya kutosha au hawakuwa wanafanya kazi nzuri BoT?
 
Namna walivyoajiriwa kwa vi-memo badala ya ajira hizi kutangazwa ili WATANZANIA wote wenye sifa waombe na kufanyiwa udahili.
 
Kwa sababu jibu lililotolewa yawezekana halihusiani na swali lililoulizwa; ila kwa vile ni jibu limetolewa basi tunatakiwa kuridhika hata kama halihusiani na swali. Well, wakati mwingine swali nalo matters...
 
Kwa mfumo wa Elimu ya sasa (Shule za kata), haya malalamiko hayatakwisha. Watakao pata Elimu bora (quality education) ni wale wenye uwezo wa kusoma kwenye shule private (academy) hata kama siyo first class students.( Kwa sababu shule hizo zina Teachers wazuri wenye access to good facilities for teaching). Hawa ndiyo baadaye watapata kazi nzuri n.k.
Mfumo wa sasa wa Elimu unajenga matabaka.
 
Wakuu naomba kusema hivi, hapa dawa kutafuta facts against haya maneno na kuziweka hapa, yaani tutafute ukweli wa elimu zao na CV zao ziwekwe hapa ili ukweli uonekane wazi kama kuna uongo na ukweli na hii habari.........

Mkuu FMES,
Nakubaliana na wewe kuwa katiba yetu haimkatazi mtu yeyote kuajiriwa BoT, PPF n.k., hata kama ni mtoto wa kigogo, mkulima n.k., ili mradi tu awe na sifa.

Nafikiri hilo sio tatizo ingawa ndio tunaloweza kulihakikisha kwa kuangalia tu CV zao.



Lakini yapo masuala makubwa zaidi ya CVs zao kama Mtanzania alivyodokeza;
  1. Kwa nini iwe kuwa watoto wengi wa vigogo wamekimbilia huko BoT na waliingiaje huko, uchaguzi wao uliendeshwaje?
  2. Kutokana na madhambi yaliyokwishatokea BoT, je kwa wao kupangwa huko haikuwa plani ya kufanikisha EPA nyingine, hii ni kwa vile tunaelewa kuwa baadhi ya vigogo ndio waliohusika na EPA?
  3. Je Ndulu wameangalia upya jinsi ajira zitakavyotolewa hapo BoT? Utaratibu gani utakuwa unafuatwa ili kutofanya baadhi ya wenye majina makubwa kupendelewa zaidi ya watoto wa wakulima?
Prof. Ndulu amechemsha maana sidhani kama hakuelewa kuwa hili suala sio la CVs tu. Inawezekana hakutaka kugusa kiini hasa cha manung'uniko ambacho ni kuwa kwa nini watoto wa walio na majina makubwa ndio yamejaa hapo BoT? Wameingia-ingiaje hapo BoT maana sio wao tu wenye hizo sifa?
 
Wakuu naomba kusema hivi, hapa dawa kutafuta facts against haya maneno na kuziweka hapa, yaani tutafute ukweli wa elimu zao na CV zao ziwekwe hapa ili ukweli uonekane wazi kama kuna uongo na ukweli na hii habari,

Mana katiba ya taifa letu inawaruhusu hawa watoto wa viongozi kufanya kazi katika mashirkika yetu ya umma pia, lakini pia katiba hii haiwaruhusu kupewa nafasi hizo bila ya kwua na qualifications zinaotakuwa au kuingizwa wka ujanja ujanja, lakini ni lazima uwepo ushahidi kama kumefanyika faulo,

Sasa tuutafute na tuuweke hapa!

Tatizo hapa mkuu siyo CV. Suala kubwa ni kutaka kujua kama BoT ni "equal opportunity employer". Kama kuajiriwa kwa watu hao kulitokana na ushindani wa wazi na wa haki na hatimaye watu hao wakashinda nafasi hizo, basi hakutakuwa na maswali zaidi. Hilo ndilo ambalo gavana Ndulu hajajibu, badala yake kaishia tu kutuambia wanazo sifa zinazostahili! Je ni wao tu wenye sifa hizo? Walishindanishwa na wengine wenye sifa, kwa utaratibu gani, na matokeo yakawa vipi, na was it a just or fair process nk? Hayo gavana ameyakwepa makusudi! Nami nikasema nilijua angejibu hivyohivyo aste aste, maana hata mchuzi uwe mtamu vipi huwezi kujisahau ukatafuna vidole vyako badala ya tonge! Jamaa ni mwangalifu sana, anapajua aliposimama!
 
Mkuu Mtanzania,

Heshima mbele mkuu, hukumu tuzitoe kwa ukweli na facts, kama kuna faulo zimechezwa huko tutafute ukweli, lakini tusihukumu kwa imaginations, kwenye EPa tunawajua wezi wetu for a fact, lakini kwenye hili tunasua sua,

Hebu tutafute ukweli kama hawa watoto wa viongozi waliajiriwa kwa faulo, maana tunakuabliana kua wananzo qualifications, lakini hatuna uhakika na kuajiriwa kwao, JF huwa tunakuwa na ukweli at hand ndio tunahukumu tena kwa standars zako mwenyewe, tusichukie wananchiw enzetu bila sababu za msingi!

Siuamini uchunguzi wa ndulu lakini siwezi kutoa hukumu nzito bila facts, ninawajua watoto wengi wa masikini ambao wapo BOT, kwa mfano mshikaji mmoja Mkulu Margai wa Imma alianzia huko na baba yake hakua kiongozi wa anything, tuwe fair japo kidogo

Unajua huyo unayemsema aliingia vipi hapo? Unamjua somebody Msirikali? Unajua Mke wa Marehemu Rutihinda?na the key issue si-wote waliingia hapo kwa migongo ya watu, ili kinacho zungumziwa ni hiyo orodha
 
1.
Unajua huyo unayemsema aliingia vipi hapo?

Margai amesoma mlimani, alipomaliza akapelekwa BOT kitu ambacho zamani alipomaliza shule ilikuwa kawaida, akaenda NY akiwa Mtanzania wa kwanza kusomea namna Financial markets zinavyotakiwa ku-function, na kurudi bongo na kuanzisha ile market yetu mbuzi, hakuingia kwa anything jamaa ni mtoto wa masikini na hakuwa any connection na kiongozi yoyote, tuache majungu hapo!

Unamjua somebody Msirikali? Unajua Mke wa Marehemu Rutihinda?

Hapo ndio kabisaa umekosea mkuu, Margai has nothing to na hao watu ambao wote ni washikajiw angu wa karibu, Josephine nimecheza naye Halaiki akiwa anasoma Jangwani, Jeska, Tony, Jane wote ninawajua wka akribu sana, Mzee Msirikali hakuwa na ubavu wowote wa kumuajiri mtu serikalini, Rutihinda asingewaacha kina marehemu Alex na kumsaidia mtu baki asiyemjua, Rutihinda anatoka Bukoba, Margai anatoka Musoma, na besides ninawajua wote kwa karibu no connection bro nothing!

na the key issue si-wote waliingia hapo kwa migongo ya watu, ili kinacho zungumziwa ni hiyo orodha

what orodha has to do na faulo inayosemwa? Yaani ilitakiwa wawe watoto wa masikini tu ndio katiba inavyosema? Wakuu tutafute ukweli kama hawa watoto waliajiriwa kwa faulo ukweli usemwe wazi kama tunao, lakini hukumu bila facts au hata dataz, tutaonekana mbele ya jamii tun tatizo na watoto wa viongozi, that is wrong by any standard za civilizations!
 
Field marshal Rutihinda alikuwa muhangaza kutoka Ngara..just to put record straight!
 
Field marshal Rutihinda alikuwa muhangaza kutoka Ngara..just to put record straight!

Sasa mkuu Koba, heshima mbele huko Ngara sio ndio huko Biharamulo huko ma-Bukoba mpaka Bunazi? Huko ma-Bunazi nilishaishi sana huko, si ndio Bukoba yenyewe hiyo au?
 
Mkuu FMES,

Vodacom na mashirika mengine ya private hasa ya simu yanalipa vizuri kuliko BOT, mbona hatuoni watoto wa vigogo wakiwa wamerundikana huko?

Labda hao watoto wa vigogo wanaipenda sana BOT yetu.
 
Mkuu FMES,

Vodacom na mashirika mengine ya private hasa ya simu yanalipa vizuri kuliko BOT, mbona hatuoni watoto wa vigogo wakiwa wamerundikana huko?

Labda hao watoto wa vigogo wanaipenda sana BOT yetu.

Mkuu Mtanzania,

BOT ilikuwepo kabla ya hao wengine na infact huko pia wapo sana, besides huko BOT watoto hawa wa vigogo kuna walioingia huko in the last two years?

Mara ya mwisho nilipowauliza wengi wao huko BOT, waliniambia kua wamekuwa huko for the last 10 to 20 years, Freeman amefanya huko, ndani ya hii forum kuna watu kibao wamewahi kuwepo huko na sio watoto wa vigogo, wote hawa waliacha baada ya kuona hapana mpango, sasa baadhi ya hao watoto wa vigogo walivumilia na kubaki,

Kuna wakati BOT haikuwa na lolote wananchi wengi hata watoto wa masikini walikimbia huko, wao walibaki sasa leo wanakula matunda ya uvumilivu wao imekua taabu vipi tena? Siasa za namna hii zitatufikisha pabaya sana, tunatakiwa tukubali matatizo yetu yaliyo wazi na kuya-deal nayo bila visingizio na lame excuses,

I do not like uchunguzI wa Ndulu, lakini pia sipendi majungu bila ukweli wala dataz, hivi wananchi wamefika Urope kama wewe? Ina maana ulimuhonga mtu kwenda huko? Maana tukishamaliza na watoto wa wakubwa kujaa BOT, then ni lazima tuhamie pengine guess what tutasema wananchi wote walioenda majuu waliendaje, sasa wapi tuta-draw the line na hay majungu?

Waacheni vijana walifanyie kazi taifa letu, kuna facts of life ambazo sometimes hatuwezi kuzizuia, lakini tuheshimu sheria zinazolinda haki za wananchi wote taifa ni letu sio la masikini tu!
 
tuacheni mambo ya kishamba...huwezi kumuadhibu mtu kwa kosa la baba yake ..au ukoo,hawa watooto wa vigogo wengi waliotajwa kwenye ile list wote wana qualifications zao...na wana haki ya msingi kufanya kazi kama yeyote.....i know most of those guys they have gone to school.....ndio maana hata baada ya pekua pekua ..wameshikwa wengine lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyeshikwa....

tatizo ninalolijua pale benki kuu lililokuwa likisababisha watu kuajiriwa kwa kufahamiana [hata wakiwemo watoto wa walala hoi wenzetu...i know some of them]...ni kwa sababu BOT hawakuwa na utaratibu wa kutangaza nafasi za kazi magazetini....sasa wameanza kutangaza ...itaondoa hii hali..

lakini pia nataka muelewe pamoja na kuwa BOT wengi wameajiriwa kwa connections nyingi miongoni mwa wafanyakazi kuwaita wenzao waliosoma nao universities....bado kabisa haifuti ukweli kuwa BOT ni moja ya taasisi iliyosheheni wasomi kuliko taasisi nyingi tanzania...na zaidi ya hapo ni taasisi yenye ushindani wa wafanyakazi wao kupenda kujiendeleza kimasomo........

HIVI WATANZANIA TUNAONA RAHA GANI HAWA WATOTO WA VIGOGO ....WALIOSOMESHWA KWA KODI ZETU NA PESA ZA KUDOKOA ZA BAADHI WAZAZI WAO WAAJIRIWE MANHATTAN.....BADALA YA KUJA NYUMBANI KAWA WENGINE KURUDISHA UJUZI WALIOSOMEA HUKO MAJUU......MBONA WATOTO WA VIGOGO ENGNEERS NA MADAKTARI ..WANAOTIBU ...HAMUWALALAMIKII....WATANZANIA TUNA DHANA POTOFU YA KUABUDU KAZI ZA FINANCE!
 
Hii discussion naona haina mwelekeo wala momentum kwa sasa...

Tuache kuwa bitter kwa kila kitu. Tunachanganya important things and trivial things under the same Jukwaa la Siasa. Mwishowe JF itaonekana ni kijiwe cha lamenters tu.

Sasa gavana amewakuta hawa watu ndani ya BoT, walipoajiriwa hakuwepo. Kawatizama kawakuta wanasifa na ujuzi, utaifa wao Tanzania. Na kazi(pengine) wanaperform vizuri. Taasisi ina watu zaidi ya 1500, hawa wanaotajwa 10. sasa wakuu mlitaka gavana afanyaje? awatimue kazi leo? jiulizeni ataanzia wapi? Jiulize ungekua wewe ungefanyaje?

Hata huko private sector wamejaa haohao kwenye makampuni yanayolipa vizuri, kina makamba, mwapachu, mramba, mungai n.k lakini tusisahau wana ujuzi hawa. Na chanzo cha tatizo kama wengi mlivyosema ni mfumo wa elimu. Unaweza hata kuwapa sijui KPMG, au PWC wawe ndio wanachuja watu pale BoT, chances are, kukuta tena watoto wa vigogo 10 kati ya staff 1500 haitakuwa news, coz hawa watoto wamepewa silaha bora zaidi za kwenye uwanja wa kutafuta kazi. Bitter to swallow lakini ndio fact zilivyo for the most part.

Lakini hata hivyo, hii ipo duniani kote. Uliza Chelsea Clinton anafanya wapi? Si ajabu atakua kwenye prominent firm/institution ya New York, au DC au Chicago. Na usiulize alishindanishwa na nani?.... Kama wangekua hawana sifa, au wababaishaji au Ndulu ndio angekua amewaajiri kinyume cha taratibu, pengine kungekua na grounds za kumshabulia.

Tuache kulialia kwenye kila jambo, tutashusha credibility ya Forum hata kwenye serious issues. There are more burning issues for this country, mnaikumbuka date ya rais ya Oct 31st lakini?..... Let the COUNT DOWN BEGIN.
 
Mkuu FMES mambo yote yaliyotokea huko BOT kama EPA nk.
Halafu na hayo majina bado tu hakuna maswali?
BOT ni benki ya serikali jamani....Ni chombo muhimu sana...Na hatuwezi kusema wako huko kwasababu eti ya uvumilivu...Jamani uvumilivu ndio kubakia BOT?
AMA KWELI TUKO MATAWI YA TOFAUTI SANA TU.
 
Back
Top Bottom