Mkuu Mtanzania,
Hapa ninashindwa kuamini, kwamba wewe bingwa wa kudai ukweli hapa uko radhi kushusha standards zako na kuhukumu watoto wa viongozi bila facts,
Ndulu aliombwa kuchunguza nini? Na aliombwa na nani? Kushindwa kwa Ndulu kufanya uchugnuzi unaoutaka sio kosa la hao vijana, huwezi kua right 100% wakati huna ukweli wa tofauti na uchunguzi wa Ndulu, Unasemaje unapinga udanganyifu wakati huna facts za ku-prove point yako bro?
Watoto wa vigogo wapo foreign pia, wapo kwenye mashirika mengi mapya ya private, ni haki yao kufanya kazi kisheria kama ilivyo yako na yangu, lakini huwezi kulazimisha guil;t on thier part kwa kuajiriwa BOT, unless unao ushahidi wa kutosha wkamba walipoajiriwa kulikuwa na kukiukwa kwa sheria za kazi huko bila huo uthibitisho mkuu ninaona ni wivu na chuki against wananchi wenzetu wka sababu ni watoto wa viongozi!
Mkuu FMES,
Hapo ndipo unapokosea, wapi mimi nimewalaumu hao vijana moja kwa moja? Mimi napinga uchunguzi uliofanya na BOT kwamba ulikuwa ni udanganyifu.
Kwenye research kuna kitu kinaitwa garbage in garbage out. Ukiingiza data fake unapata report fake. Sasa kama waliamua kuchunguza basi wangechunguza process nzima ya hao vijana kuajiriwa na sio qualifications tu.
Pia scenario tunayoiona BOT haiko foreign affairs tofauti na unavyodai. Foreign kuna weza kuwa na watoto wanne au watano wa vigogo lakini sio kama hiyo BOT. Kama una data tofauti mwaga hapa.
Ni private company gani ambayo imejaza hao watoto wa vigogo kama BOT? Kama una data telemsha hapa mkuu. Tuna data za BOT, kama una data zingine zinazofanana na hizo basi JF ndio mahali pake.
Mkuu lazima ujue uongozi ulioajiri hao vijana ndio huo huo uliokuwa unachota mabilioni ya Watanzania kwa kufuata vimemo vya wakubwa. Unataka kutuambia kwenye ajira hawakupata vimemo kama hivyo?
Mimi ni mtetezi wa haki na utawala bora, lakini hapa kuna malalamiko ya upendeleo. Utawala bora unataka uchunguzi kama huo ufanywe na chombo ambacho hakihusiki na hayo madai. Hapo BOT tunaona wanajichunguza wenyewe. Hao hao BOT si ndio walisema hakuna wizi wa pesa mpaka makaburu walipowaumbua?
Nitakuwa wa mwisho kuiamini report ya BOT. Kama mchangiaji mmoja alivyosema, suala sio hao vijana tu, suala ni pamoja na kazi zao, maana ikionekana vimemo vilitumika itabidi baadhi ya watu wapoteze kazi.
Namheshimu prof. Ndulu lakini kwenye hili ni kama Watanzania wengine ambao kazi yetu ni kushindwa kuchukua hatua madhubuti na kuanza kupiga blah blah kama za JK. Hata hao vigogo wa BOT waliofukuzwa kazi ni kwasababu tu ya Makaburu na pia E&Y, vinginevyo uchunguzi wa BOT ungeonya hakukuwa na makosa.
Watu dunia hii hawaajiriwi kwa basic entries, hizo basic entries zinakusaidia tu kukufikisha kwenye interviews za maana. Sawa walikuwa na basic entries, je baada ya hapo? Ina maana wote waliokuwa na basic entries waliajiriwa BOT?
Wamepoteza muda na mamilioni ya pesa za Watanzania kuchunguza kitu ambacho ni obvious.
Kwenye hii taarifa prof. Ndullu anaongelea vijana 18 wakati ukweli ni vijana 26 kwasababu wanane walishachukuliwa hatua. Hivyo namba sahihi ya watoto wa vigogo ilikuwa at least 26 na sio 18.