Watoto wa vigogo BoT wasafishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watoto wa vigogo BoT wasafishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Oct 22, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Watoto vigogo BoT wasafishwa

  Na Ramadhan Semtawa

  WAKATI watumishi wengine tisa wa Benki Kuu (BoT), wakifunguliwa kesi mahakamani kwa kughushi vyeti, watumishi wengine 18, maarufu kama watoto wa vigogo waliodaiwa kuajiriwa kinyemela wamebainika kuwa na sifa stahili.

  Kukamilika kwa uchunguzi huo na matokeo, kunaondoa na kumaliza utata uliokuwepo tangu awali kuhusu ajira za watoto ambao baba zao wengine wapo serikalini na waliostaafu.

  Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alithibitishia gazeti hili jijini Dar es Salaam kuhusu watoto hao kubainika na sifa stahili.

  Watoto ambao wameonekana kuwa na sifa, majina ya koo zao ni pamoja na Lowassa, Sumaye, Kawawa, Lumbanga, Hassan Mwinyi, Muganda, Mahita, Nchimbi na Mkapa.

  Katika orodha hiyo, majina mengine ya ukoo yanayotajwa ni pamoja na Luhanjo, Kamba, Mongela na Kigoda.

  Akizungumzia mchakato huo ambao alisema uliendeshwa kwa uwazi na umakini, Profesa Ndulu alisema katika uchunguzi huo watoto wanane kati ya 18 ambao walikuwa wanafanya kazi za kitaaluma wote walikuwa na sifa.

  Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, jambo la msingi lililotumika katika uchunguzi huo ni vigezo vya ajira kwa kuanzia mwaka 2000/01 hadi 2006/07.

  Akifafanua hilo, Profesa Ndulu alisema kabla ya mwaka 2005, kulikuwa na vigezo tofauti na baada ya mwaka huo, walioajiriwa baadaye 2006/07, walipaswa kuwa na vigezo vipya tofauti na vile vya mwaka 2000 hadi 2005.

  Profesa Ndulu alisema kabla ya mwaka 2005, kazi za kitaaluma kigezo kikuu kilikuwa ni shahada ya kwanza, lakini baada ya mwaka huo kigezo kikawa ni shahada ya uzamili (MA).

  "Kwa hiyo, watoto hao wanane mnaoita wa vigogo wote walikuwa na basic entries (sifa za kujiunga), waliajiriwa kwa vigezo stahili, ambavyo kipindi hicho ilikuwa ni shahada ya kwanza, lakini pia waliendelea kusoma na kuweza kufikia shahada ya uzamili ambayo ni kigezo cha baada ya mwaka 2005," alifafanua Profesa Ndulu.

  Alisema vijana hao ambao wanafanya kazi nzuri, waliingia na sifa stahili na bado wamekuwa wakijiendeleza kwa kusoma zaidi.

  "Tena ni vijana wachapakazi tu, wamesoma vizuri, wanafanya kazi vizuri na tayari tumewapa barua za kuwataarifu kwamba wana sifa stahili," alisisitiza Profesa Ndulu.

  Profesa Ndulu alisema watoto wengine kumi ambao hawakuwa wakifanya kazi za kitaaluma, nao waliingia wakiwa na sifa.

  Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, watoto hao walikuwa na kazi ambazo ni pamoja kuhesabu fedha.

  Akizungumzia sifa zao za kujiunga, alisema kwa kazi ambazo si za kitaaluma, kigezo kikubwa kilikuwa ni kidato cha nne na kujua hesabu na Kiingereza.

  "Hawa nao 10, wote walikuwa na sifa hizo, wanafanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu na hakuna namna yoyote ya kughushi ambayo walifanya," alifafanua Profesa Ndulu, gavana ambaye amekuwa akiisafisha BoT.

  Alisema uchunguzi huo uliangalia watumishi 50 wakiwemo hao 18 watoto wa vigogo na kuongeza kwamba, wengine pia walibainika na sifa huku wale ambao walikiuka walichukuliwa hatua.

  Hata hivyo, alisema tayari BoT imetoa tangazo kwa kuwataka watumishi hao kujisomea kwa gharama zao wenyewe vinginevyo hawatapanda madaraja.

  "Kwa hiyo, kama mtu hatajiendeleza, ajue hatapanda daraja, atabaki hapo hapo na kuathiri ajira yake," alisisiza Gavana Ndulu.

  BoT ambayo ni taasisi nyeti katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 chini ya uongozi wa hayati gavana Daud Ballali, ilikumbwa na tuhuma mbalimbali.

  Miongoni mwa tuhuma hizo, ni pamoja na hizo za watoto wa vigogo kuajiriwa katika mazingira yaliyohisiwa kuwa ni tata, kashfa ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na gharama kubwa za ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.

  Hata hivyo, tangu Gavana Ndulu aingie BoT Januari mwaka huu baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, amefanikiwa katika harakati kuisafisha taasisi hiyo nyeti, kujenga uhusiano mzuri na vyombo vya habari hata umma.
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndulu don't take us for a ride? Tanzania ina watu takribani milioni 36, hivi majina hayo tu ndo yenye uwezo wa kushinda interview za kazi BOT? kwani wapo form 4 wangapi wanao jua hesabu na kingereza? kwanini wenye majina hayo tu ( the so called vigogo)

  Beno hiyo BOT ni mali ya Watanzania wote, nawewe endelea kusafisha ufisadi na uzandiki huu, lakini kumbuka watoto wa walala hoi tunazidi choka.. kama hamtaki sikia sauti zetu, subirini kuna siku hata miti na mawe vitasema.

  Hiyo richness cycle lazima ifumuke na itufikie wengine!
   
 3. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari hii ina uwalakini. Ndullu angetuambia kazi hizo zilitangazwa lini? wangapi waliomba na mchakato uliotumika kuwapata watajwa. Watu si wajinga!
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nadhani hili suala linahitaji UTAFITI YAKINIFU... Hizi ajira za watoto wa vigogo (nadhani tuseme viongozi wakuu wa serikali wastaafu na waliopo kazini) ndani ya BOT yawezekana zilifanyika on merit grounds or on "MEMO" grounds.

  Kwahiyo ili kupata tafsiri sahihi ni vyema tukapanua wigo na kutizama across public services sector as whole. Na natumaini hizo data zitatupa picha nzuri ya kujua kama ni kweli watoto wa "vigogo-kwanyuma" upata ajira kwa uhalali?

  Inawezekana tunaongelea sana BOT, perhaps kutokana na status yake lakini pia kwenye taasisi nyingine za serikali kuna waajiriwa ambao wana uhusiano na "vigogo-kwanyuma" waliongia kwenye ajira kwa stahili za "kimemo".

  Wana-JF tukumbuke kwamba collectively public service is doing very poorly interms of service delivery and it should be noted that in any insititution where nepotism is normal practice, there will be certainly poor performance.

  **********************
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani majibu ya Gavana ni sahihi, ila kwa maswali ambayo siyo. 10 linaweza kuwa jibu sahihi kwa 6+4 lakini sio 3+2 ambalo nadhani ndilo swali la msingi hapa. Nadhani kiu ya Watanzania haikuwa kuwa hao walioajiriwa BOT kuwa hawani sifa na ujuzi wa kazi hizo, ila walichotaka kujua ni utaratibu gani uliotumika kuwapa vijano wote wa vigogo hao kazi. Kulikuwa na uwanja sawa wa ajira? Je, matangazo ya kazi yalikuwepo? interview ziliendeshwa je? wajumbe wake walikuwa kina nani? kulikuwa na bias yoyote katika kuchagua hao wafanyakazi? nk. nk.

  Mimi nadhani haya ndiyo majibu aliyotakiwa KUYAJIBU Gavana, na sio kutoa taarifa kuwa wana shahada za uzamili! Mbona wengi tu wanazo, kwani wanafaya BOT, au wao hawataki kufanya BOT? Nadhani anatakiwa arudi alieleze hili!
   
 6. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Hivi huu uchunguzi uliangalia jinsi walivyoingia huko BOT au walikagua tu vyeti vyao? Kwangu mimi tatizo nililoliona sio tu la vyeti bali zaidi ni jinsi walivyoingia hapo kwenye kitovu cha EPA na karibu wote wakawa wanatokea kwenye cream ya vigogo na sio cream ya BCom (UDSM n.k.), IFM, IDM-Mzumbe n.k.

  Au ina maana hawa watoto wa vigogo pia wote ndio walikuwa vipanga kwenye vyuo vyetu au ndio wale 'waliopendelewa' kupata Scholarship za India, UK n.k.??

  Gov. Ndulu inatakiwa atufafanulie ni jinsi gani BOT ilifanikiwa kuaajiri watumishi wake, wengi wake wakiwa watoto wa vigogo.
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sijui WAANDISHI wote NCHI hii ni "REPORTERS" tu. Kwa nini hawakummuuliza maswali hayo? Uandishi wa nchi hii unachosha sana na hii imechangia usomaji magazeti kudorora sana
   
 8. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli tunachohitaji kujua
  1. Kazi zilitangazwa lini na kwenye magazeti gani au ilikuwa ile design ya kupelekewa tangazo nyumbani kuwa kuna kazi hii hebu apply mwanangu....
  2. Wangapi waliomba na sifa zao manake saa nyingine the best candidates (seen as threat) wanaweza wasiwe-shortlisted ili kurahisisha employment ya watoto wa vigogo walio kwenye list
  3. Kwenye usaili ranking ilikuwaje ----hao watoto wa vigogo ndio walikuwa the best among all applicants?

  Nadhani imefika wakati shutuma kama hizi ziwe zinachunguzwa na watu huru(ambao kwa nchi yetu ilivyo ni kazi kuwapata) kabisa sio kutupa majibu rahisi rahisi na kudhani kuwa tutaridhika tu kirahisi kama wanavyodhani.
   
 9. Francis the King

  Francis the King Member

  #9
  Oct 22, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I am sick of this country..
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sure Francins

  Unajua pia inatia hasira sana, a reputable person a professor, ambaye wengi tuliamini siasa hazija mzingira na kumuinfluence utendaji wake, kwa kipindi kifupi tu hiki ameisha badirika na kuanza na kuja mbele ya public kuleta politics za kuwapumbaza watu kisanii sanii!

  Mpaka watu kuhoji uhalali wa watoto hao si kweli kwamba hawana data, wengine wapo humu humu BOT wanajua kila kitu nawe unatoka kueleza mambo kijuu juu namna hii!

  Hizo kazi zilitangazwa wapi? waliomba wangapi? interview wakafanya wangapi kwa vigezo vipi? jopo la waamuzi je lilikuwa free ama influenced? hayo ndiyo tunayo yalalamikia.. siyo hizo bla bla zako, kwa taarifa yako hata zile data za mtoto wa kigogo mmoja aliyekuwa akipachikwa kama kiraka kwa kuto fit popote mle BOT tunazo, na huyo je? leo hii nawe unakuwa msanii??

  Beno, wewe msomi, linda heshima yako, ukiendekeza siasa kuna siku nawe utapopolewa mawe mtaani hata ukiwa kikongwe! be aware!
   
 11. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2008
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Rwabugiri,

  Ebu tupe habari kuhusu huyo Mfanyakazi Kiraka ambaye labda amesomea fanii nyingi tu ndiyo maana akawa anapachikwa kila kona BOT. Hivi BOT huwa hamna muda wa probation ili ikifikia kikomo na mwajiriwa mpya hana deliverable zilizotarajiwa anaambiwa "Asante, kazi yako hairidhishi katafute kwingine".
   
 12. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #12
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ma mdogo,
  Ka surf humuhumu JF hii topic ya watoto wa vigogo si mpya, data zote zimemwagwa humo, hata hivo naomba mod kama hawatajali waiunganishe hii mada huko, ili wasomaji wapya wapate mwendelezo murua!
   
 13. A

  August JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  sasa BOT ikiwa marorocho namna hiyo, kuna kukua kweli kwa uchumi wetu? Na tatizo ni pale mpaka wasomi wanapokuwa wajinga na kushindwa kutumia ujuzi wao katika kufanya kazi. yaani Prof mzima na akili zake anaendeshwa na Darasa la Nnne la zamani?
   
 14. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hapo BoT sikutegemea jibu tofauti na hili. Tunasubiri ya Tume ya EPA!
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  this means prof aliamua kujitungia swali mwenyewe au hajui hesabu?
   
 16. Tonga

  Tonga Senior Member

  #16
  Oct 22, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ni kweli kabisa kwasbabu kama anasema kigezo kilikuwa ni degree ya kwanza wakati huo, kwani wangapi tulikuwa nazo tena za field hiyo ila hatukuona hayo matangazo ya ajira BOT na sisi tuombe kazi! Na kwa sasa kama kigezo ni Masters basi wote wenye MA wanaqualify kwa ajira BOT mbona sioni majina ya kawaida kama Wambura,Mgaya, Chamila, Wagesi, Rajabu, etc? bado majina ni hayo hayo ya watoto wa vigogo, bwana Gavana bado majibu yako sio kamili zaidi ya vigezo vya kupata kazi tunahtaji kujua uhalali wa hao kuajiriwa kuna walakini katika hili believe me "lisemwalo lipo na kama halipo laja" tumekuwa kichwa cha mwendawazimu for so long huku wengine wakifaidi ASALI na MAZIWA....
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,559
  Likes Received: 1,917
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wadau wote hapo juu...Habari hii ni tata.
  Therefore ni wazi kutokana na kichwa cha habari ambacho kinasema "Wasafishwa" Ni wazi si kila kisafishwacho husafika.
   
 18. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  kuna jambo tunasahau hapa, ubaguzi unaanza tangu kwenye elimu, hawa watoto wamesoma ulaya na marekani ambapo wakina yahe wamesoma kule kwenye shule za kata za lupa tinga tinga ambazo hazina walimu wa hisabati! hata tufanye nini huyu wa lupa hataweza kuja kufanya kazi pale bot kwa kuwa na ukipanga wake ameishia kuzubaishwa kwenye shule ya kata isoyo na mwalimu wa hisabati, pamela lowasa yeye kasoma ulaya au marekani wakato lowasa akihubiri kujenga shule za kata kule lupa!

  tunabidi tuwe makini, wakati mwalimu nyerere akileta wanafunzi kila kona ya nchi na kuwajaza kule tosamaganga, mkwawa na kwingine, na hakuishia hapo akaenda kuwaleta walimu urusi, ulaya na kwingine wa kwetu tumewaacha huko vijiini kwa kisingizio cha shule zenye viwango vya kufikirika
   
 19. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Gavana abanwa

  2008-10-22 18:34:37
  Na Mwandishi Wetu, Jijini


  Ahsante.
  Leo vyombo vya habari vimemkariri gavana Ndulu akisema kuwa uchunguzi uliofanywa kuhusiana na ajira katika taasisi hiyo, umeonyesha kuwa watoto 18 wanaotajwa kuwa na uhusiano na vigogo wameajiriwa kutokana na sifa zinazostahili.

  SOURCE: Alasiri
   
 20. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tatizo sisi watanzania tumelelewa hivi na CCM (Mtoto leo akizaliwa hajui ametoka wapi yupo wapi na anaelekea wapi. Shule za majengo tu. QUANTITY WITHOUT QUALITY?)Tusipojifikiria ktk 3D basi ujue taifa hili sijui linaenda wapi, BORA NIISHI PEKE YANGU MANA I CANT SEE THE FUTURE IN MY EYES. Nchi imekuwa ya wale wale tu kila siku.

  Kuna baadhi ya makampuni ambayo hayahitaji hata vimemo but OLE wenu wale ambao mmpeta VIMEMO hata kwenda huko mnakoishi, kupata nafasi ya kusoma, kufanya kazi, kupata kiwanja, kupata wachumba na kadhalika ambayo imamjenga mtu kimaisha. Afadhali kama unajua fulani amekusaidia na iwe siri yako but peleka jeuri hio kwa wengine. Hapa ndo ninapokasirika kwa kuwa tumejenga matabaka hapa Tanzania. Kuna wengine huku kanda ya ziwa wanajiona miungu watu na wengine na wanahasira na wenzao huku wanakimbia kivuli vyao mfano Mama Kilango na wengine. Mbona walisema kuwa patachimbia mpaka leo papo flat? wengine ooh mahakamani mpk leo kimya!!! KWA NINI?

  Leo hii tumesahau kuwa Mwl Nyerere ni mtu kama wewe ila tumeshau kwa kuwa dhambi hii tumeshailishwa. Nilishangaa siku moja mtu ananiomba msaada ETI awe mwalimu. Was soo easy kumwambia apeleke wizarani kwa kweli akapata tena mjini, akaniletea mshahara wake wa kwanza. Nikamfukuzia mbali mpaka leo hatuelewani. Eti ASANTE, mimi!!! Mungu wake si akamfuate huko anakoaminia!!!!.

  Wale walio BOT watakuwa kama wale watoto wa mama Lucy Nkya walioitwa mafisadi kwa kuwa waliona sifa kusema mama yake ni waziri nao wakamalizia FISADI MTOTO mama akaona hasira ni kumalizia HAKI ELIMU.

  MAX de Melo, kabla hujafikiria kufyatua jaribu kuweka JAMBO ACCOUNT ile nae mtoto wako akasomee pale OXFORD UNIVERISTY. Bila shaka wakati huo utampa elimu bora sio bora elimu ila asije ajiriwa kwa kimemo cha..................

  Asante
   
Loading...