Mama Mdogo
JF-Expert Member
- Nov 21, 2007
- 2,961
- 2,138
Mdau mmoja mkereketwa wa haki za watoto katika pitapita zake maeneo ya Friends Corner Manzese aliweza kuwaona watoto Nyambuli Mganga (5) na Gosbert Bwire (3); wale watoto walionyesha umahiri wa kupiga ngoma na kucheza wakati wa sherehe ya miaka 51 ya Uhuru. Aliwakuta watoto hawa wakiwa na Kiongozi wa msafara Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara, Mpalala Mwendwa. Kilichomsikitisha mdau huyu ni kuwa, watoto hao wameletwa Dar bila kuandamana na wazazi wao walioachwa huko Mara; na mbaya zaidi kiongozi huyo wa Serikali alikuwa ameshika pombe kali ya Value, na akawa anawanywesha watoto hao kwa kutumia kifuniko cha pombe hiyo. Mtoto Bwire alikuwa anakunja uso kila anaponyweshwa hiyo pombe na huyo Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara. Huu ni ukiukwaji wa haki za watoo, na udhalilishaji wa watoto. Viongozi kama Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara, Mpalala Mwendwa, wanatakiwa wakemewe na jamii. Kwa maelezo zaidi, soma taarifa hii ya mkereketwa kwenye blog ya Michuzi (MICHUZI). Picha hizi hapa chini zinatukumbusha kuhusu watoto hawa walivyokuwa wanatuzwa na Mh Nnauye na Mh Mwigulu; na nyingine ni ya kuonyesha watoto wakiwa na Afisa Utamaduni ameshika pombe ya Value akifanya vitu vyake huku mtoto Bwire akiwa amezidiwa na ukali wa pombe amekunja uso!!! Maswali ya kujiuliza: Kwa nini wazazi waliachwa huko Mara wakati watoto hawa ni wadogo sana kusafiri bila wazazi, na hasa mama? Kwa nini Afisa wa Serikali anawanyweshwa watoto hawa pombe, je ni siku hiyo tu, au hata siku walipoburudisha walikuwa wameleweshwa Value? Nani analala chumba kimoja na watoto hawa huko walikofikia?? Nina hasira na huyu Afisa, we acha tu, uchungu wa mwana aujua mzazi!!!