Watoto wa sherehe ya miaka 51 ya Uhuru wanyweshwa pombe kali ya 'Value'!

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,962
2,138
Mdau mmoja mkereketwa wa haki za watoto katika pitapita zake maeneo ya Friends Corner Manzese aliweza kuwaona watoto Nyambuli Mganga (5) na Gosbert Bwire (3); wale watoto walionyesha umahiri wa kupiga ngoma na kucheza wakati wa sherehe ya miaka 51 ya Uhuru. Aliwakuta watoto hawa wakiwa na Kiongozi wa msafara Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara, Mpalala Mwendwa. Kilichomsikitisha mdau huyu ni kuwa, watoto hao wameletwa Dar bila kuandamana na wazazi wao walioachwa huko Mara; na mbaya zaidi kiongozi huyo wa Serikali alikuwa ameshika pombe kali ya Value, na akawa anawanywesha watoto hao kwa kutumia kifuniko cha pombe hiyo. Mtoto Bwire alikuwa anakunja uso kila anaponyweshwa hiyo pombe na huyo Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara. Huu ni ukiukwaji wa haki za watoo, na udhalilishaji wa watoto. Viongozi kama Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mara, Mpalala Mwendwa, wanatakiwa wakemewe na jamii. Kwa maelezo zaidi, soma taarifa hii ya mkereketwa kwenye blog ya Michuzi (MICHUZI). Picha hizi hapa chini zinatukumbusha kuhusu watoto hawa walivyokuwa wanatuzwa na Mh Nnauye na Mh Mwigulu; na nyingine ni ya kuonyesha watoto wakiwa na Afisa Utamaduni ameshika pombe ya Value akifanya vitu vyake huku mtoto Bwire akiwa amezidiwa na ukali wa pombe amekunja uso!!! Maswali ya kujiuliza: Kwa nini wazazi waliachwa huko Mara wakati watoto hawa ni wadogo sana kusafiri bila wazazi, na hasa mama? Kwa nini Afisa wa Serikali anawanyweshwa watoto hawa pombe, je ni siku hiyo tu, au hata siku walipoburudisha walikuwa wameleweshwa Value? Nani analala chumba kimoja na watoto hawa huko walikofikia?? Nina hasira na huyu Afisa, we acha tu, uchungu wa mwana aujua mzazi!!!


Watoto 2_Nyambuli Mganga 5 na Gosbert Bwire 3.jpg Watoto 1_Nyambuli Mganga 5 na Gosbert Bwire 3.jpg
 
Tumshukuru Mungu kama iliishia tu katika kuwanywesha pombe na akawaacha salama.
 
Mama Mdogo;

Kwa kuna tofauti gani ya watoto wa miaka 4 wa wenye pesa wanaopelekwa shule za boarding zilizopo Uganda na Kenya bila kuwa na uangalizi wa wazazi wao na hawa wanaopelekwa shule ya mwalimu Nape?
 
Hii kali ..ungetoa report polisi mamamdogo ujue
sio fair kabisa
 
'Shame' kubwa. Iwe kweli au isiwe kweli mama yake aambiwe ili siku nyingine na yeye awemo kwenye msafara.
 
hakuna ushahidi hakuna picha inayooneshwa anafanya ivyo,hii ni njama ya kumchafua Mh:, ila kama angewanyweshwa ingekuwa poa maana valuu inachangamsha
 
hakuna ushahidi hakuna picha inayooneshwa anafanya ivyo,hii ni njama ya kumchafua Mh:, ila kama angewanyweshwa ingekuwa poa maana valuu inachangamsha na ukiwa mpga ngoma na mcheza ngoma lazima uchangamke ila natania tu
 
Kama ni kweli, hii siyo habari ya kuishia kui-post humu tu, shuhuda unatakiwa ukairipoti kwenye vyombo husika!
 
hakika hizi ni nyakati za mwisho!! katoto kamekunja sura maskini yarabi kusikilizia ule ukakasi! halafu wana umri gani kuwa mbali na mama zao?? mbona ni kama under 5, au naona vibaya?? LORD HAVE MERCY ON MY COUNTRY TANZANIA!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom