Kule Kwetu
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 3,157
- 1,890
Hata mimi nashangaa wanawake hawatupishi sisi wanaume kwenye viti vya mabasi/ daladala.Ukitaka kuhakikisha hili, panda basi za mwendokasi.
Utawakuta bila aibu hata kidogo wamekaa kwenye viti na hawataki kuwapisha watu wazima. Yaani mtoto mdogo kabisa kakaa kwenye siti bibi yake kasimama na kuegemea mlingoti.
Sijui wanatoka katika familia zipi ambazo nidhamu ni msamiati.
Yaani mwanamke anathubutu kukaa wakati Mwanaume amesimama tu.
Kule kwetu sijawahi kushuhudia haya tangu kuzaliwa.