Utofauti kati ya watu wa Dar (Mijini) na watu wa Mkoani ndio huu

Styx Charon

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
503
1,000
Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.

Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo..." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata ka trip ka Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti." Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kidogo, unamuuliza habari ya Njombe. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza ku chat, mke wako naye ana chat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kila mtu anakula kwa wakati wake!" Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Handwash basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu ana chat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
____
Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea katika mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.
 
Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,221
2,000
Hiyo nyumba ya ba mdogo kule Njombe nayo kuna TV yenye game? Ingekuwepo madogo lazima nao wangekonsentreti tu.

Siungi mkono walichofanya familia ya baba mkubwa Dar ila nachosema baada ya miaka 7 au 8 hata kule Njombe itakuwa hivyo hivyo tu.

Kwanza ingekuwa zamani ba mkubwa angelala lazima pale home kwa mdogo wake ila si umeona kala kaaga kaondoka na wakamsindikiza hawajamlazimisha alale wala nini.
 
0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
1,800
2,000
Shangazi anatoka Bukoba, anakuja na maboga, hapokelewi mizigo mpaka ndani.

Kesho asubuhi dada wa kazi anayapika maboga, muda wa chai watu hawana habari nayo.

Shangazi anayala tena maboga yake peke yake wengine wakitafuna mikate, maboga yanabaki baadae yanatupwa.

Kumbuka kutoka Bukoba mpaka Dar alikuwa anayalipia nauli kila anapobadilisha usafiri.
 
Styx Charon

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
503
1,000
Shangaz anatoka bukoba,anakuja na maboga,hapokelew mizigo mpaka ndani,kesho asubuh dada wa kaz anayapka maboga,muda wa chai watu hawana habari nayo,shangaz anayala tena maboga yake peke yale wengine waktafuna mikate,maboga yanabaki baadae yanatupwa,kumbuka kutoka bukoba mpaka dar alkuwa anayalipia nauli kila anapobadilisha usafiri
Hahaha kazi kweli kweli
 
Eliclassic

JF-Expert Member
Aug 15, 2019
3,394
2,000
Shangaz anatoka bukoba,anakuja na maboga,hapokelew mizigo mpaka ndani,kesho asubuh dada wa kaz anayapka maboga,muda wa chai watu hawana habari nayo,shangaz anayala tena maboga yake peke yale wengine waktafuna mikate,maboga yanabaki baadae yanatupwa,kumbuka kutoka bukoba mpaka dar alkuwa anayalipia nauli kila anapobadilisha usafiri
Kwan sis tulimuagza aje na maboga?😂😂 Just jokin
 
May 11, 2021
53
125
Shangazi anatoka Bukoba, anakuja na maboga, hapokelewi mizigo mpaka ndani.

Kesho asubuhi dada wa kazi anayapika maboga, muda wa chai watu hawana habari nayo.

Shangazi anayala tena maboga yake peke yake wengine wakitafuna mikate, maboga yanabaki baadae yanatupwa.

Kumbuka kutoka Bukoba mpaka Dar alikuwa anayalipia nauli kila anapobadilisha usafiri.
Mambo ya kujipendekeza niliacha aisee, kabla ya kusafiri kwenda Dar kwa ishu yoyote unawaza na kuwazua uwapelekee nini,unajikongoja kwa tabu unakipata cha kuwapelekea kuepuka aibu ya kwenda mikono mitupu. Baada ya siku kadhaa unagundua ulichowapelea kimwagwa kwa kuozea ndani.

Hii ilishanitokea,nilikupata kibarua Lushoto sasa mkataba ulipoisha nikasema ngoja niwabebee nyanya na apple zile za Lushoto,Mungu wangu baada ya siku tatu niligundua nyanya zimeoza hazkuwekwa hata kwenye friji zile apple alikula anko kwa kuondoa aibu huku akisifia hizi ndo nzuri huku watoto na mama hakuna aliyegusa. Nilijisikia vibaya sana mpaka mambo ya kicahwi labda lakini niligundua tu ni mambo ya kibaguzi kwakuwa mimi ni mtu wa chini. Umasikini ni mbaya sana.

Kwa uzoefu wangu ni kwamba hao watu wa Dar wanafanya hivyo vituko kwa ndugu zao wanaotoka mikoani ambao ni maskini lakini kwenye uwezo kama wao shughuli zote zinasimama mapaka kwenda kupokelewa hata ingekuwa mtu anafika saa nane usiku.
 
Matindi94

Member
Oct 12, 2016
36
125
Mbona stori ya kweli kabisa hiyo

Umenikumbusha mbali sana mitaa ya Ramadhani kigamboni nimewahi ishi huko

Ila maisha ya sasa watu wapo bize sana na town mambo ni mengi kwahyo kama mtu sio muelewa atadhan anadharauliwa kumbe hapana
 
Hank_31

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
502
1,000
Mambo ya kujipendekeza niliacha aisee, kabla ya kusafiri kwenda Dar kwa ishu yoyote unawaza na kuwazua uwapelekee nini,unajikongoja kwa tabu unakipata cha kuwapelekea kuepuka aibu ya kwenda mikono mitupu. Baada ya siku kadhaa unagundua ulichowapelea kimwagwa kwa kuozea ndani.

Hii ilishanitokea,nilikupata kibarua Lushoto sasa mkataba ulipoisha nikasema ngoja niwabebee nyanya na apple zile za Lushoto,Mungu wangu baada ya siku tatu niligundua nyanya zimeoza hazkuwekwa hata kwenye friji zile apple alikula anko kwa kuondoa aibu huku akisifia hizi ndo nzuri huku watoto na mama hakuna aliyegusa. Nilijisikia vibaya sana mpaka mambo ya kicahwi labda lakini niligundua tu ni mambo ya kibaguzi kwakuwa mimi ni mtu wa chini. Umasikini ni mbaya sana.

Kwa uzoefu wangu ni kwamba hao watu wa Dar wanafanya hivyo vituko kwa ndugu zao wanaotoka mikoani ambao ni maskini lakini kwenye uwezo kama wao shughuli zote zinasimama mapaka kwenda kupokelewa hata ingekuwa mtu anafika saa nane usiku.
Mkuu umasikini ni mbaya sana, tena unanuka, wala sio kitu cha kujisifia mbele za watu kabisa,

Masikini hana maamuzi ya kuchagua yaani, yaani kama kuna uwezekano mkuu ni bora mtu apambane na umasikini kwanza kabla ya yote.

Kurudi kwa mada hapo juu hayo ndo maisha ya kina junior huko mjini Dar.
 
T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,260
2,000
Mwaka jana wakati nimeenda field mkoani kwa baba mdogo nilishangaa kupokelewa na watoto wake wawili wadogo ambao hawanijui. Akiwa nao kwenye gari, walinisubiri tangu saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku.

Home tulifika walikuwa wanachangamka sana, wanauliza mimi ni nani na natokea wapi, maswali mengine wanamuuliza baba yao. Kumbe hata kunipokea kote hawakuwa wanajua ninatokea wapi na ninahusiana nao kivipi wao waliambiwa kuna mgeni anakuja wakawa excited kunipokea. Niliishi nao poa sana walikuwa wananiita ndugu yangu badala ya kaka
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,594
2,000
Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".
Hii niliisoma kama zamani sana zaidi ya miaka mi5 iliyopita ,Thanks kwa kuileta tena.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom