Utofauti ya watu wa dar na watu wa mkoani ni huu

idifu10

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
329
233
UTOFAUTI YA WATU WA DAR NA WATU WA MKOANI NI HUU
Umeenda semina Njombe, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Ramadhani shukia kwa Sanga. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".

Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.

Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Baada ya muda mke wa mdogo wako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani, anakuja kukunawisha mikono huku akisema "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo.." Unakula unashiba.

Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry na Irene. Ukija tena uje nao" Unaondoka kwa heshima zote.

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu Mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha Mbezi, lina waya za umeme juu".

Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti" Housegirl anaenda kufungua. Ndugu yako anaingia sebleni anawakuta. Anawasalimu unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia yake.

Wanao wanacheza game kwenye computer hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unawaambia, nyie msalimieni baba yenu mdogo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!

Mnazungumza kigogo, unamuuliza habari ya Dodoma. Kabla hajakujibu unashika simu unaanza kuchat, mke wako naye anachat! Sitting room imejaa watu, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula"

Unamgeukia mdogo wako unamwambia "aisee we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake.!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza peke yake. Maji ya kunawa hakuna! Bahati nzuri dada wa kazi anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye "Hw basin" maji yanatoka!

Anaenda kunawa kinyonge. Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting room. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unampa, unamwambia chukua hii utalipa hiyo bodaboda.

Boda inafika, ndugu yako anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka. Mama bado yupo busy na simu anachat. Watoto game limekolea, hawataki kutoa macho kwenye computer. Ndugu yako anawaaga hata hawamuangalii usoni. Wanatupia kwa mbaali "kwa heri ba mdogo" wanaendelea na game. Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.

Wengi tunaoishi mijini tuna maisha ya aina hii, na tunaona ni sawa. Tunajifanya tupo busy kwenye mambo yasiyo na msingi na kupuuza utu wa wengine. Hata watoto wetu tunawalea ktk mazingira ya kuthamini zaidi vitu kuliko utu. Hii si sawa hata kidogo. Tuwatendee wengine kama tunavyotaka kutendewa.
 
Tabu sana hii.Na wa "Daisiramu"(tamka kwa sauti ya Maxence Melo katokea Kamagombe) wakienda kutembea vijijini huenda na mikate.Nayo ikizidi ni minne.

Ila wao wakitaka kurudi makwao wanataka wafungashiwe maharage,unga,mchele,samaki wakavu,mikungu ya matoke na hata kuku.Watu wa mjini uhuni mwingi sana.Wenyewe wanaita "unyama mwingi"!😂😂😂😂
 
Ni kweli ni kweli kabisa. Semaa pia bado tupo tunaoenda kuwasubiri wageni stand
 
We umesema ivo wana wa dsm anakwambia aah siku ukija town fresh tu uncheki

Siku unatoka zako mkoa mshikaji wako nae ndo anakua mkoani🤣🤣

Watu wa daslam aisee sema safi xmas 13 dsm zmenifanya niwajue vizuri
 
  • Kicheko
Reactions: rr3
Hamna kitu sipendi kama kufika ugenini na kuanza kutoa simu nichat.
Mi nakuaga kama sina simu vile 😂😂😂
Naweza kaa kutwa sijaishika kabisa.
Hata meeting pia
Huu ujinga upo kila mahala mnaweza mseme mkutane marafiki, kitachofata hapo ni mmekaa kila mtu anachat
Huu ulimbukeni utaisha lini sijui
 
Huu ujinga upo kwa sister angu, na kila siku analalamika mbona hupendi kuja kwangu mpaka nikuite kufata kitu.

Siji kwakua ukienda unakua kama mvamizi mtu pekee utaongea nae ni housegirl nae anakusemesha kwa woga woga tu.

Watoto kila siku wakumbushwe kwamba ww ni nani! Sister mwenyewe saa zote anachat

Unajikuta unaangalia tv na nilivyosipendi Tv ndo kabisaa.

Kuna majumba yanachefua sana
 
Ila kijijini raha mimi na ukubwa huu nasalimia wakubwa zangu kwa kupiga magoti mpaka chini. Nikiwa nyumbani hii ni lazima.

Nikiwa huku njini nasalimia ile tu ya kuinama kidogo, bado watu wanakushangaa hasa nikiwaga dar wachaga mnavituko😀 mtu anasalimia shaam mama alishafika kule hiyo ndo shikamoo mama😊

Wasukuma pamoja na ushamba wao mnavyowasema bado wana heshima hili ndo kabila pekee lenye heshima nililoliona huku mjini.

Ila mimi siwalaumu watoto mleta mada anao wazungumizia maana hawajafundishwa tangu wakiwa wadogo.wako sahihi.

Sisi tulifundishwa ni lazima kumpokea mgeni na kumsalimia ukiwa umepiga magoti, lakini muda wa kula unamnawisha mikono ukiwa umepiga magoti etc.

Pamoja na kuishi mjini na uzee huu kuna vitu kwangu viko automatic mfano mtu akija kwangu wakati wa kula najikuta nishapiga magoti kumnawisha afu unakuta wakati mwingine namzidi umri basi tu najisahau.

Tusiwaseme vibaya watoto walozaliwa mjini shida ni wazazi wao.
 
Back
Top Bottom