Mjadala: Kuna ulazima wa kuwapisha wazee kwenye siti?

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,777
24,211
Katika hiki kizazi cha digitali kumeibuka mjadala mkali kati ya vijana na watu wa makamo kuhusu suala la kuwapisha watu wazima kwenye siti za magari.

Busara: Wazee/watu wazima inatakiwa wapewe siti kwani kusimama kwenye daladala ilihali vijana wamekaa ni utovu wa nidhamu.

Hoja za vijana: Wazee wanaiona gari zimejaa lakini bado wanaingia kwenye magari ili iweje?

Pia vijana wanasema mbona hakuna umuhimu wa kuwapisha, kwani Kila mtu anapambana na hali yake [mbona wazee hawataki kutupisha kwenye ajira].

Karibu kwenye mjadala na hoja konki.

1686752926871.jpg
 
Katika hiki kizazi Cha digitali kumeibuka mjadala mkali kati ya vijana na watu wa makamo kuhusu suala la kuwapisha watu wazima kwenye seat za magari

Busara
Wazee/ watu wazima inatakiwa wapewe siti Kwani kusimama kwenye daladala ilihali vijana wamekaa ni utovu wa nidhamu

Hoja za vijana
Wazee wanaiona gari zimejaa lakini bado wanaingia kwenye magari Ili iweje

...Pia vijana wanasema mbona hakuna umuhimu wa kuwapisha Kwani Kila mtu anapambana na Hali yake [bmbona wazee hawataki kutupisha kwenye ajira]

NB karibu kwenye mjadala na hoja konki
View attachment 2657401
Vijana wana hoja ndio lkn waangalie mazingira,Kuna wakati magari yanakuwa machache na abiria unakuta ni wengi,na hao Wazee ukute wanatakiwa kuwahi sehemu wanayoenda,Sasa watafanya nini km si kuingia kwenye gari iliyokwisha kujaa?.Vijana tufikiri mara mbili ktk hili,Hutapungukiwa kitu ukimpisha mzee,zaidi sana Utabarikiwa na Mungu.
 
I
Yaap!,hapo sawa ndugu yangu.Sisi sote ni wazee watarajiwa ikiwa Mwenyezi Mungu atapenda tuishi miaka mingi.
la ni kweli usemayo sema kuna wale wazee wengine mi huwaga siwapishi kabsa unakuta ni mwanzo wa safari na ni ya kusubr daladala ijae ndo safari ianze ww umesbria gari ijaze imejaa yy kusubria gar ingne moka ijaze anaona kero sijui ndo haraka au anategemea watu wampshe wa hvo siwezi kumpisha kbSa aisee
 
Kuwapisha siyo suala la nidhamu pekee, bali ni suala la kiafya pia. Duniani kote wazee hupewa hiyo heshima. Hata katika nchi zilizoendwlwa, Subways na Mabasi kumetengwa viti/behewa maalum kwa ajili ya wazee. Huku kwetu, kwakuwa hakuna viti maalum au behewa maalum kwa ajili ya wazee/watu wazima Sana busara ni kwa wadogo kupisha watu wazima Ili kuenzi heshima yao na kutambua changamoto zao za kiafya ambazo wengine huwawia vigumu kusimama muda mrefu.
 
Binafsi inategemea na mood ya siku husika,mara nyingi katika mazingira ya kawaida nikipata seat alafu mzee akaja kusimama karibu yangu huwa nampisha.Lakini kuna zile siku nafanya kila ninaloliweza ili nipate seat,iwe kugombania,kusubiri gari ya nyuma ambayo haiko katika foleni ya kupakia au kulipa nauli mara mbili ili kuzunguka na gari nipate seat,Siku za namna hii ni ngumu ku-surrender seat yangu.
 
Back
Top Bottom