Watendaji Chuo cha Muhimbili watakiwa kujitathimini, wapewa miezi mitatu ya uangalizi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ameutaka Uongozi wa Chuo cha kati Elimu ya Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUCOHAS) kujitathimini katika uwajibikaji wao na namna ya Uongozi unavyoendesha mambo yake.

Prof. Makubi ameyasema hayo Oktoba 30, 2022 wakati alipokitembelea chuo hicho kufuatia malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa Wizarani.

Mara baada ya kuongea na watumishi hao Katibu Mkuu huyo akiwataka Viongozi wa chuo pamoja na watumishi wote kujitathimini na kuhakikisha chuo hicho kinaboresha ufundishaji kwa vitendo pamoja na uwajibikaji wa Menejiment hiyo kwa kuwa karibu na watumishi na wanafunzi

Hata hivyo Prof. Makubi alisema amekiweka chini ya uangalizi wa karibu kwa miezi mitatu chuo hicho ambacho ili kuweza kubadilika na kuwajibika ipasavyo ili kuzalisha wanafunzi bora katika kuhudumia afya za Wananchi. Uongozi umetakiwa unatakiwa kuwashirikisha watumishi katika maamuzi yao, madai na kuwasikiliza kwa karibu sana.

Chanzo: EATV
 
marupu rupu madogoo, inakuwa vigumu kukaa na kutulia ofisini kuanda masomo, kuelekeza wanafunzi, kufanya tafiti .... twakimbizana vijiweni na vishughuli vya kawaida ili maisha yasogee.
 
Chuo hakina hospitali ya kufunfishia unategemea hao wahitimu watakuwa na viwango kweli.Rudisha Mloganzila MUHAS ueleweke.
 
Back
Top Bottom