Wateja wa Mabenki chukueni tahadhari kubwa, kuna wizi kwenye tozo na commission zao

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,082
Ndugu wana-JF, kumbe tulipoambiwa kuwa eti Serikali imesikia kilio cha wananchi kuhusu tozo, na hivyo kuamua kupunguza, inaelekea ilikuwa ni hadaa kubwa. Sikuwa na kawaida ya kuomba bank statement kama hakuna sababu ya msingi. Safari hii, kuna account yangu moja iliyopo CRDB Bank ambayo huwa naitumia kwa matumizi yangu yangu binafsi, nikaamua niombe bank statement. Nilichokutana nacho, nimeshangaa sana.

Kuna wizi au unafanywa kwa makusudi au system zao zimefeli, na hivyo zinawaibia wateja. Japo kwa kweli kufeli kwa system siamini sana kwa sababu sehemu zote imekuwa ni kuibiwa kwa mteja, hakuna ambapo ama mteja amekosa kukatwa tozo au fees.

Kwa mfano, siku 1 ambapo nilitoa sh 400,000 kwenye ATM, nilikatwa cash withdraw commission mara 1, TMS government levy mara 3, VAT mara 5, kwa muamala huo huo mmoja wa laki 4.

Hizi pesa kwa sababu zinakuwa ni kiasi kidogo, unaweza kuwa unakatwa bila ya wewe kutambua. Nina imani siyo mimi pekee, kuna uwezekano mkubwa wengi wanafanyiwa mambo haya.
 
Jana nimetoka kuomba bank statement wamekata buku na bank statement hawajatuma.
Crdb mnaugua nini? Yaani Wametuma message hewa
 
Back
Top Bottom