Kuna shida kubwa sana kwenye ofisi ya NHIF mkoa wa Mwanza

Zero 2 Hero

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
351
575
Kuna shida kubwa sana kwenye ofisi ya NHIF kwenye mkoa wa mwanza.
1. Ofisi iko moja mkoa mzima, hivyo wateja wanalazimika kusafiri umbali mrefu kutoka wilaya zote za mwanza na visiwani kufika ofisi zao zilizopo Buzuruga kwenye jengo la TMDA

2. kuna foleni kubwa sana inayosababishwa na wingi wa wateja (mkoa mzima) na uchache wa wahudumu. Ukiingia chumba namba 74 ambamo ndimo wanamosikilizia mahitaji ya wateja, kuna watoa huduma wawili tu na kompyta 2 tu. Hata hao wahudumu wawili muda mwingi anayesikiliza wateja ni mmoja tu. Mwingine kazi yake ni kuzunguka zunguka kutoka ofisi moja kwenda nyingine na kinachotafutwa hakijulikani.

3. Ofisi inashida kubwa ya shida kubwa ya mtandao sijui wataalamu wao wa mtandao wanafanyakazi gani. Kuna muda huduma hulazimika kusimama zaidi ya saa nzima kusubiria mtandao ukae sawa.

4. Ofisi hiyo inaongoza kwa kupoteza mafaili ya wateja hasa wanaopeleka maombi ya kujiunga na mfuko kwa mara ya kwanza ama wanaoongeza wategemezi. Hii inasababisha usumbufu kwa wateja kulazimika kupeleka documents mpya mara kwa mara.

5. Kulingana na sera ya NHIF toka mteja awasilishe maombi ya kujiunga na mfuko na kuwasilisha nyaraka zinazohitajika ndani ya wiki 2 (siku 10 za kazi) kadi zake zinapaswa kuwa tayari. Lakini mambo ni tofauti kabisa. wateja waliowasilisha maombi mwezi wa 9, 10, 11 na 12 wote hakuna aliyepatiwa kadi mpaka sasa wakati watu wameshalipia ama wanakatwa michango kila mwezi.
AJIRA MPYA wa serikali ndio kabisaa hawajapata huduma toka mwezi wa 7.

6. Ofisi yao inadai kuwa mashine ya ya kuprint kadi imeharibika na hawajui itapona lini. Hivi hili ni jibu la kuwapa wateja? Kama mashine imeharibika kwanini wasitafute njia mbadala wa kuhakikisha wateja wanaendelea kupata huduma bila shida? Mfano wangeweza kutuma details za wateja wanaohitaji kadi kwenye ofisi yao iliyopo geita ama mkoa mwingine jirani ili ziprintiwe huko kisha zisafirishwe kwenda mwanza.

N.B
Changamoto ya NHIF mkoa wa MWANZA pia ipo mikoa ya TABORA na KAGERA.
 
Back
Top Bottom