Watch TBC Live!. " William Malecela na Ndoto ya CCM Kutawala Miaka 50!.

Status
Not open for further replies.
Ati ccm inatawala next 50 years! Wake up William and smell the coffee!
Atafraiii... CCM hii ambayo imeshindwa kuwapa wananchi maji safi na salama ilhali tumezungukwa na ziwa victoria,tanganyika,natron,manyara,chala,nyasa,duluti, mindu ... ongezea bahari kuanzia tanga mpaka mtwara, mito mikubwa kama Rufiji, Ruvu, Ruhuhu, Pangani, Wami,Ruvuma...plus vyanzo mbalimbali kwenye maporoko ya vilele vya mt k'jaro, meru, miinuko ya pare, usambara, uluguru, udzungwa nyanda za juu kusini..

Le Mutuz KAVIMBIWA tumbo na akili pia!!! Kwa mtu mwenye akili timamu lazima atakuwa anapatwa kichefuchefu akisikia hili lidubwana CCM linalotoa harufu mbaya ya ufisadi likitamkwa... TANZANIA kweli ni ya kuwa na SHIDA ya MAJI? SILLY MAGAMBAZ...
 
Wanabodi,

Please watch TBC-leo saa 4:00 usiku (not exactly!) Mwana JF mwenzetu, William Malecela atazungunzia kuhusu
1. Baada ya CCM kutawala kwa miaka 50, wish yake ni CCM itawale kwa miaka 50 mingine ijayo!.
2. Majukumu ya JF as Social Media!.
3. Kwa nini JF ni watu wa kulaumu tuu serikaki na sio kuisifia!.
4. William Anaamini CCM inapendwa na Watanzania na CCM kama chama hakina, matatizo na watu bali matatizo ya CCM ni personalities za baadhi ya viongozi only!.
5. Pia amefanya ukosoaji wa CCM ili iweze kutawala miaka 50 Ijayo!.

NB. Wana JF wenzangu, nawaombeni sana tujenge utamaduni wa "Political Tolerance" kwa kuvumiliana, kustahamiliana na kupingana bila kugombana kati kati ya watu wenye milengo tofauti ya kisiasa.

NB. Sio kipindi kuhusu jf bali ni "wrap up" ya 10 series zangu ziitwazo " Saba Saba na PPR" na nilipokutana na William nilim beg for his comments na akakubali!. I thank him for that!.

My Take:
Wana jf wengi ni watu wa maneno marefu na matendo mafupi!. Nilipokutana kwa mara ya kwanza na William pale Dodoma, nilimpongeza kwa kuwa ni miongoni mwa wana jf wacheche wenye "guts na waliotake that "extra step" to move toka kwenye maneno hadi kwenye vitendo kwakuingia kwenye kwenye "ground zero" ya "active politics" ndani ya uwanja wa mapambano!. Anastahili a big "Big UP!" and not a subject of ridicule!.

Please take time to watch him, listen to him in "betwen the lines", mtakubaliana na mimi kuwa huyu Mkuu William sio mtu wa kubezwa hata kidogo!. Japo I personally don't share with him comments za " Le Grand Mutus", " The Big Show!" and the like!.

" Please lets take him for "Who he is" not for "What he is"!.

Thanks.

Pascal.
Up Date 1!.
Very Unfortunately Kipindi hiki hajitakuwepo due to "un avoidable circumstances"!.

Kipindi kilirekodiwa tarehe 08/07/2012 na kilikuwa kitoke ile ile tarehe 8, kukatokea "technical problem" kipindi hakikwenda!.

Jana tarehe 9 kilikuwa kiende, lakini kukatokea " Technical problem" hakikwenda!.

Leo tena kilikuwa kiruke kuanzia saa 4:00 usiku huu lakini kumetokea tena a " technical problem" kipindi hakijarushwa!. na kwa vile the "theme" was "Vox Pop" ya " mrejesho" wa maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam!.

Kwa vile maonyesho yamenalizika toka Jumapili, ladha ya mrejesho ni sponteneity ya pale kwa pale!. Mrejesho wa 3 days after is pointless hivyo sidhani kama kipindi hicho kitakuja rushwa!.

Sorry for a all inconveniences caused!.
Update 2.
Ni kweli program ina technical problem ya ku-stuck stuck ila inarushwa na clip ya William imeruka!.
Pascal.

Bora kuangalia senema ya ma-vampire
 
- again hoja yangu nyingine ni my committment ya kuona ccm inatawala miaka 50 ijayo i have no shame on that na sina unafiki on that goal, that is my goal and mission ninaamini in 50 from now ndio ccm tutaanza kugombea kura na upinzani, kwa sababu huu wa sasa siouni as serious upinzani, ni upinzani wa ccm against ccm, sio upinzani against ccm nit yet hatujafikia huko yet, lakini naamini 50 years from now tutakuwa there; wapinzani bado sana mpaka leo hawajweza kuwa na agenda moja ya chama, kila siku agenda za binafsi na nyingi zinaanzia kwenye maadui wa ndani ya ccm yaani wenyewe kwa wenyewe meaning kwamba watoaji wa agenda always wanakuwa na control of how far the agenda will go sio the messenger aliyepewa tu ili kutumiwa kwa manufaa ya baadhi ya viongozi wa ndani ya ccm.

!!

Nianze na hapo kwenye red: Kama upinzani hawajeweza kuwa na ajenda moja ya chama inakuwaje wanawavutia wananchi? (think about it). Kwa maneno mengine CCM kimekosa mvuto kwa sababu ya agenda?

Pili, madai kwamba upinzani una hoja binafsi zinazoanzia kwenye maadui wa CCM is not quite right. Kumbuka up until 2010 CCM na madoadoa yote bado walikuwa wamoja. Na ndio maana ukiangalia mikanda au picha utaona kweli 'watu' walikuwa wamoja wakati wote wa campaign. Walisaidiana kwa hali na mali. Uadui wa CCM unaoungelea ulijitokeza baada ya uchaguzi na ulichangiwa sana na mabadiliko ya kimtazamo toka kwa wananchi juu ya upinzani. Wanachi wengi walionekana kukubali life without CCM is possible. Na kwenye mikutano ya upinzani wananchi walijitokeza kwa wingi.

Ni sawa na mwanamke anayekuwa kwenye abusive relationship, mara nyingi inakuwa vigumu sana kwake kujitoa kwenye huu mkasa kwa sababu mbalimbali i.e hofu, haamini kama anaweza kuishi bila huyo mume, au just uoga tu. Lakini ikatokea siku akapata courage na kusema to hell with this relationship/ marraige, I can do better, kwa hakika ataondoka na hakuna wa kumzuia. Na huku nyuma mwanababa aliyeachwa (mara nyingi) atakasirika sana, ataona amedharauliwa after all he had all the powers in the house. Na hata akikutana na huyo mwanamama mahakamani anaweza kuonesha hasira maana amekuwa 'challlenged' (humulited?) something he was not used to.

Hii ndio hali ya CCM, wananchi wamekuwa abused for decades, sasa wamepata courage and kusema to hell with CCM lakini CCM wenyewe wanaona no no no hawa watakuwa wamefundishwa na 'watu'! Wanafuata nini huko? Lazima ni wale watu tuliogambana nao ndio wanawapa kichwa! Ujue kweli CCM wamewa-abuse wananchi, inafikia mahali wanatoa chakula wakati wa campaign! Chakula, ubwabwa, mahindi, maharagwe!

Well, as the saying goes, 'a hungry man is an angry man'. Na ningesema be afraid, be very afraid of a hungry man. Watanzania kwa mamilioni wana njaa ya elimu, njaa ya huduma bora za afya, njaa ya malazi bora, njaa ya barabara safi, njaa ya employoment. Na njaa hii imezidi siku hadi siku. Kweli hapo unahitaji 'hasimu toka upande mashariki? Hii mambo ya sera sijui chama upinzani hauna agenda moja ya chama, I just dont buy it. Na hata hao wanaodhaniwa ku-export support wamefanya hivyo as part of the equation ya kibano cha upinzani. Kwamba public imeonekana kuwa upande wa pili na sababu za kuvuka upande wa pili wakataja, CCM wakaona bora warekebishe mambo ili wasiachwe, but again wakashikwa na kigugumizi. Na hii ime-shake foundation ya chama.

Hata hivyo nikiri, Dr Slaa amefanya mambo makubwa sana kwa Tanzania (sio tu chama chake) ila nchi kwa jumla. Amefanya watanzania kwa ujumla wao kuangalia matundu na michirizi kwenye governance system yetu. Bika hilo hatuwezi kuwa na mijadala yenye tija. Nchi nyingine zinesonga mbele sisi tunabakia na michakato. It is about time.

Labda una idea mpya na hizo idea zitauzika kwa umma. good luck.
 
Wanabodi, wish yake William Malecela ni CCM itawale kwa miaka 50 mingine ijayo!.
Je, alitoa sababu yoyote kwa nini anataka CCM itawale kwa miaka mingine 50? Hata hivyo nadhani anaongezea nguvu tu hoja ya Mzee John Cigwiyemisi Malecela aliyedai kuwa CCM itatawala hata kwa miaka 100 (like father like son!) ila yaonekana bado wako kwenye karne ya 17...if wishes were thrushes beggers would eat birds! (mwaka 1605)
Kwa nini JF ni watu wa kulaumu tuu serikaki na sio kuisifia!.
Pascal Mayalla huo ni uwongo, JF ni jamvi lenye watu wa itikadi mbali mbali...wako ambao huikosoa serikali inapoboronga na wapo ambao daima ni kuisifia tu serikali hata pale inapoharibu.
William Anaamini CCM inapendwa na Watanzania na CCM kama chama hakina, matatizo na watu bali matatizo ya CCM ni personalities za baadhi ya viongozi only!. Pia amefanya ukosoaji wa CCM ili iweze kutawala miaka 50 Ijayo!.Wana jf wengi ni watu wa maneno marefu na matendo mafupi!. Nilipokutana kwa mara ya kwanza na William pale Dodoma, nilimpongeza kwa kuwa ni miongoni mwa wana jf wacheche wenye "guts na waliotake that "extra step"
Ni kweli CCM inahitaji watu wenye "guts" kwani si rahisi kwa mzalendo kulimbikiza mabilioni benki za Uswisi huku wananchi wengine wakilala njaa.
to move toka kwenye maneno hadi kwenye vitendo kwa kuingia kwenye kwenye "ground zero" ya "active politics" ndani ya uwanja wa mapambano!. Anastahili a big "Big UP!" and not a subject of ridicule!.
Mwanzoni William amedai kuwa tatizo la CCM ni personalities za baadhi ya viongozi only! je kwenye huo uwanja wa mapambano alikoamua kuingia, anapambana na nani? Heri akumbuke walichosema wahenga, if you cant fight them, join them! William ameamua kujiunga rasmi na kundi lililoifikisha nchi hii hapa ilipo.
Please take time to watch him, listen to him in "betwen the lines", mtakubaliana na mimi kuwa huyu Mkuu William sio mtu wa kubezwa hata kidogo!. Japo I personally don't share with him comments za " Le Grand Mutus", " The Big Show!" and the like!.
Make up your mind Pascal, si wa kubezwa kwa lipi...comments zake za "Le Grand Mutus", "The Big Show!" and the like?...I have watched him, listened to him "betwen the lines" na sikubaliani na wewe hata chembe.
Please take him for "Who he is" not for "What he is"!.
What? So what you are saying is we should take him for who he is and not what he is? To be honest I think I agree with you here...I think you are right, take away the name and one is left with nothing, just a body!
 
Last edited by a moderator:
Pascal Mayalla nakufahamu toka enzi zileee pale juu nyuma ya msikiti wa Ngazija...enzi za akina Islem Barafaa na ALi Oki, Mzee JABIR, Meb, bila kumsahau Jov ambaye amekuwa tajiri wa kutisha

then how can I forget enzi za DVT na akina Betty Mkwasa na bila kumsahau bwana Ahmed Nzowa

hapa nazungumzia 1992-93...nilikuwa nakuamini then na naendelea kukubali mpaka leo

hivi kaka miaka yote hii pamoja na usomi wote na kutemebea kote duniani bado mnategemea TV stations ziwatushie vipindi?

Nashangaa mpaka leo hamjamfundisha huyu dogo Invisible namna ya kutake advantage of hili dude (JF)...mwishowe zimeishia kwata zile zile za miaka yote...ni aibu leo 2012 Jamii forum haina Youtube channel ambayo ingeweza kuleta vipindi vya Bunge au hata mihjadala ya kwenye TV

Nilitegemea hii Jamii Media ingekuwa isha evolve lakini cha ajabu imeishia ku print T-shirts za misiba na sasa tazama forum ilivyo...vurugu tupu...siasa zimekuwa CHADEMA vs CCM wakitake break bas ni kututakananana weee mpaka

Hivi unajua enzi za JAMBO FORUM JK inasemekana alikuwa halali bila kusoma JF?

Je JF unayoiona leo ni GAME CHANGER kama zamani?

Wewe, Mwanakijiji, Halisi, William Malecela na Maxcence mlikuwa na nafasi ya kukaa chini na watu ambao hamkubaliani nao kiitikadi na kuweza reform hili dude na mka move on lakini tazama leo. Mwanakijiji ana back up yake kivyake na analitumia kwa interests zake, nyinyi kila mmoja ana mapango wake halafu leo unatuletea habari kuwa kipindi kimeshindikana ku air kwa sababu ya TV?

You guys need to go back to the drawing board amasivyo haya mambo ya William kuna na JF ni ndoto za alinacha

Kama huamini ninayoyasema kuwa hatuko tayari kuambiana ukweli hii post itakuwa deleted bila sababu.

Kuna mtu aliwahi kuuliza...je Maxcence Melo anaweza kuwa WAEL GHONIM wa Tanzania? kama humjui wale basi mgoogle

Ukweli ni Yes lakini inabidi abadili mentality na watu waliomzunguka lazima wakubali ukweli kuwa watu wanazidi ku evolve na tactics za zamani hazina mvuto anymore

Sielewi Rashidi wa PUSH MEDIA ameweza vipi ambapo Max wa JAMII MEDIA kashindwa?
 
​Tatizo ni kuwa hamjui kuimarisha chama sisi kama wana CCM tunataka muende arusha mkafufue chama kikishakomboka kule tutajua kweli CCM itatawala miaka 50 mingine na sasa operesheni sangara inaanza in 2 weeks matawi mengine yatafungwa sasa kwa nini tusiwalaumu na william arudi newyork akabebe box hapa tuna mikokoteni inatutosha
 
Nianze na hapo kwenye red: Kama upinzani hawajeweza kuwa na ajenda moja ya chama inakuwaje wanawavutia wananchi? (think about it). Kwa maneno mengine CCM kimekosa mvuto kwa sababu ya agenda?

Pili, madai kwamba upinzani una hoja binafsi zinazoanzia kwenye maadui wa CCM is not quite right. Kumbuka up until 2010 CCM na madoadoa yote bado walikuwa wamoja. Na ndio maana ukiangalia mikanda au picha utaona kweli 'watu' walikuwa wamoja wakati wote wa campaign. Walisaidiana kwa hali na mali. Uadui wa CCM unaoungelea ulijitokeza baada ya uchaguzi na ulichangiwa sana na mabadiliko ya kimtazamo toka kwa wananchi juu ya upinzani. Wanachi wengi walionekana kukubali life without CCM is possible. Na kwenye mikutano ya upinzani wananchi walijitokeza kwa wingi....


Toka nimerudi nimeongea na Media labda hii ni mara ya 60 na Radio pia, sasa kama media wanazidi kuniiita then ina maana kuna something positive na serious ninakisema kinakubalika, leo tena nilikuwa kwenye another TV station so we are getting our message out there na tunasikika, I mean we are on the right track


- Kila mmoja ni lazima awe na goal katika maisha au katika tunayoyaamini na mimi msimamo wangu ni kuhakikisha ninaisaidia CCM kutawala another 50 years; infact I am doing it now!!

Le Mutuz!!
 
Le Mutuz unaitwa na radio pamoja na Tv station nyingi kwa sababu ni mtoto wa kigogo wa CCM na umekaa nje ya nchi kwa muda mwingi hivyo wengi wanapenda kusikia kutoka kwako nini hasa msimamo au mtazamo wako hasa kisiasa ulipojikita kwa sasa.

CDM inabebwa na vijana ambao wanonekana kuwa ni wazalendo ambao wapo tayari kukusoa na kuisema CCM na serikali wazi wazi tofauti na ilivyo kwa vijana wa CCM. Mimi nilidhani ungeliona hilo na kujitahidi kuliziba kwa kuanzia kwako lakini naona unaendeleza siasa za akina Nape.

Jambo la mwisho kila unapoonge huweki point zako wako na unaandika kama mhuni vile hebu jaribu kulirekebisha hilo, hebu mcheki mtu kama FJM anavyoandika na kueleweka wazi. Nimekufuatilia hili nimeona ni tatizo lako na ikiwa na kuongea hueleweki kama kwenye kuandika basi siasa hutaiweza.
 
W.J. Malecela,

Mkuu wangu wala sintokubishia kwa kazi unayoifanya isipokuwa kazi yako itazaa nini ndio hapo tunaweza tofautiana kwa sababu unajaribu kupanda juu ya mwaba ama shamba lenye magugu.. Tatizo kubwa ambalo hujaliona ni kwamba mmeshindwa kupalilia magugu kwanza kabla ya kupanda miche au mbegu zenu na kama ujuavyo weeds zinaua mimea haijalishi utaweka mbolea kiasi gani..

Siasa unazozifanya zaweza kuwa na malengo mazuri sana kwa wananchi na wanachama wa CCM kama kilimo kwanza lakini unachoshindwa kuelewa ni kwamba sisi wengine tumejitenga na CCM kwa sababu tunaelewa malengo hayatafikiwa na sababu kubwa ni Uongozi mbaya na utekelezaji mbaya. Hakuna kitu kinaweza kufanyika leo pasipo kubadilisha kabisa mfumo mzima wa uongozi kwa sababu sisi tulopitia kidogo Socialogy kuna kitu kinaitwa Culture of Deviance kimejikita ndani ya chama. Huu ni Utamaduni ulotokana na sisi kuingia Ubepari bila mahesabu wala kuelewa kwamba Ubepari unatanguliwa na MTAJI, huwezi kuwa bepari wakati ni handsome boy on the road nothing in the pocket!.

Na ndio sababu ya kuzaliwa Azimio la Zanzibar ili viongozi watupige bao, kwa makusudi kabisa mnashindwa kutazama behaviours za viongozi wetu wakikiuka sheria wazi wazi kisha mnasema CCM haina mapungufu isipokuwa baadhi ya watu! who are these people?..come on bro these aren't norms - Unapoona the ruling class wanatumia policy na criminal justice system kufanikisha economic & social purposes zao basi bila shaka ndio deviance zenyewe hizo. Crime imekuwa political concept ili kulinda power na position za viongozi at our expense (The poor).

How in the hell can you ask for 50 years of CCM leadership wakati unajua fika kwamba tatizo sio Chama bali watu waliomo na hata siku moja CCM haiwezi kutawala bila watu hawa unless this thing CCM is somekind of computed machine inajiendesha.. Lakini nakuomba sana unapotembea mitaani angalia sana na kujifunza kwamba sasa hivi tuna conflict kubwa sana ya kijamiii.. Crimes zimehalalishwa hadi kwa mfagia barabara, muosha magari na hutakiwi kumuamini mtu ukimwamini utaachwa mataani.. Trust has gone down 80% na ukikosea kidogo tu kumuamini mtu utazikwa, utaibiwa na huna pa kwenda kushtaki. Crime imeshakuwa utamaduni wetu na hivyo ktk elimu ya Criminology sign zote za kuharibikiwa zinajionyesha kitaifa, ebu pitia kipande hiki halafu unambie wapi hatujafika

- Crime becomes a function of the conflict between the goals people have and the means they can use to legally obtain them. While goals are the same for all the ability to obtain these goals is class dependant. Consequently, lower classes feel anger, frustration and resentment which is referred to as strain. These people can either accept their condition and live out their days as socially responsible but un-rewarded citizens, or they can choose an alternative means of achieving success, such as theft, corruptions, violence or drug trafficking.

Kuna la kuongezea mkuu wangu!.. think again.
 
William Malecella- na kauli-tata ya umiliki wa JF.



Akiongelea Jamii Forrums (JF), kupitia TBC (recorded episode) na PPR ya Pascal Mayalla, William Malecella ametamka,
"…in fact I'm one of the shareholders wa JF"



Malecella, Je, JF kuna shareholders? Ni akina nani hao na share zake zinauzwa soko gani la hisa kama ni public? Na hata kama si public, pia tuelezwe muundo wa hiyo 'kampuni JF' ya akina WM ili tufahamu tusichokifahamu sisi ambao ni wanachama humu bila kujua kuwa hii ni kampuni ya watu fulani.
Mimi najua kuwa kuna raia wema wanaojitolea fedha kuisaidia kuendesha JF kama michango yao ya hiyari na sio hisa, wala sijawahi kuelewa kuwa kuna watu wana status ya shareholders humu JF hata kama wangeitwa premium members.



Au ni msamiati ulimpiga mweleka, akitaka kusema 'stakeholders'?
Mod; tafadhali sana nisahihishwe kama nimekosea na thread hii ni nyeti maana hapa naongea suala la mwanachama mmoja kuibuka na mwenzake kumrusha kwenye media ya umma (TBC) akidai kuwa yeye ni sehemu ya wamiliki wa JF!:A S cry:
 
Si kosa lako, hata Babako siku moja baada ya kupata mlo mtamu wa mchana,aliwahi bwabwaja kuwa Cca itatawala miaka 100 toka 2007. Mbuzi huzaa mbuzi daima, na mtoto wa mhunzi asiposana huvukuta. Umri mdogo, lakini mawazo yako yamezeeka kama una miaka 115 vile. Pole sana kijana, subira yavuta kheri!
 
Le Mutuz unaitwa na radio pamoja na Tv station nyingi kwa sababu ni mtoto wa kigogo wa CCM na umekaa nje ya nchi kwa muda mwingi hivyo wengi wanapenda kusikia kutoka kwako nini hasa msimamo au mtazamo wako hasa kisiasa ulipojikita kwa sasa.

CDM inabebwa na vijana ambao wanonekana kuwa ni wazalendo ambao wapo tayari kukusoa na kuisema CCM na serikali wazi wazi tofauti na ilivyo kwa vijana wa CCM. Mimi nilidhani ungeliona hilo na kujitahidi kuliziba kwa kuanzia kwako lakini naona unaendeleza siasa za akina Nape.

Jambo la mwisho kila unapoonge huweki point zako wako na unaandika kama mhuni vile hebu jaribu kulirekebisha hilo, hebu mcheki mtu kama FJM anavyoandika na kueleweka wazi. Nimekufuatilia hili nimeona ni tatizo lako na ikiwa na kuongea hueleweki kama kwenye kuandika basi siasa hutaiweza.

- Siamini kwamba Tanzania nzima ni mimi tu peke yangu mwenye hiyo status unayoisema, najua wapo wengi lakini bado hawajitwa na Station hata moja ya Media, mambo ya CDM ni mawazo yako mwenyewe na ni haki yako kuwa nayo; style yangu ya uandikaji na kuongea ndio inanifanya niitwe sana hizo media so tumia yako watakapokuita mkuu wangu!!

REspect!1

Le Mutuz @ KATA KIVUKONI:DSMCITY.
 
Mkuu personally siwezi kuwa na 'political tolerance' kwa mtu sampuli ya W. J. Malecela. I am pretty sure there is some thing in his brain that makes him to impair. Pia na wewe Pascal unajishushia adhi kwa kuwa karibu na mtu huyo...

Political tolerance exists ONLY when the ideology of the other has some resemblance to yours but spurs on execution style, timing etc. I stand to be corrected, WJ behaves like a failed Paris Hilton who has tried to be a top singer, a top model, a top celebrity and could not make the cut!!!

When ya see a person climbing up and down the ladder, they need help. Even pupils whose academic trends go like that, deserve more help. Kutoka kugombea Ubunge wa EAP na kuangukia Ujumbe wa Kata, na kwenda NEC hiyo ni W trend! Kwann hakuanza na Ujumbe wa kata. Opportunist?? Just like poor Paris Hilton.

Paschal, believe me ya - he was the happier person when you two met!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom