watch-out hizi GIRLS NIGHT OUT.Changa la macho

Mke mwema yu ndani yako kaka unayesoma hapa, tabia unazozitaka kagua kama unazo. Usidanganyike kila kitu kizuri kipo kwa wakati na mazingira sahihi, hi dunia ni pana sana achilia haka kajiji ka Dar tu kuna mambo kuna watu wengine tukisikia hata hizo habari za girls Night ni terminology mpya kabisa masikioni mwetu, si kweli kabisa wadada wote tumeharibika noo nakataa, ila ninyi wanaume hamjui mnataka nini? Mi sijui hata niseme je jamani, kwanza jitambue wewe ni nani na unataka nini, na unataka atoke wapi huyo unayemtaka.

Daaa kaka zangu mnaniuzunisha sana ujue, hivi unataka mke mwema asiye na mambo mengi ya kiduniani lakini wewe dunia unataka uibebe kichwani, kila mwanamke unaomuona umjue, baa zote maarufu unazijua, sijui club sijui nini hizo ni mteja mzuri, aina zote za pombe unazitaja kama sala ya baba yetu, halafu unataka mke asiye kuwa na hayo mambo, kweli jamani!!

Mkikutana na mwaminifu mwenye utu na kiasi katika maisha unamchakachulia hadi malengo yake unambwaga hapo. JITAMBUENI KINA KAKA. JALINI UTU.

umenena vema LD!. Satisfaction is at infinty..aka kujilisha upepo.. Mimi ni kijana na inanisikitisha,au pengine ni kutokuwa na utu na hofu ya Mungu..kwanza haya mastarehe mi i dont kno mwisho wake kama si kujuta,anyway,kp t up!
 
una busara we mwanamke balaa,vipi uko single au una dada yako?nyie ndo wanwake tunaowataka mtutulize

Kutulia unaamua wewe mwenyewe binafsi kwa kuridhika na yule uliyenaye,kujiheshimu na kumuheshimu Mungu,presence ya mwanamke mtulivu kwenye maisha yako ina uwezo mdogo sana wa kukutuliza......l.o.l:laugh::laugh:
 
kwa hiyo mnasuggest nimkataze shemeji yenu hizi girls out?

aaaaaaah acheni hizo bana hata akikaa ndani kama wa kumegwa atamegwa tu

Ndo maana nakupenda,hata akikaa ndani......atamegwa tu......:laugh::laugh:
 
Girls wana deserve nights out kwani si wote wana misbehave,mbona wanaume mnatoka sana wenyewe? Nanyi tuwa judge wote kwa matendo ya wachache wenu? Mfanyaji unapaswa ubadilike na wala usiwatumie hao mabint ku justify tabia zako mbaya.
 
Thanks for this post

My wife atakoma na hii mambo ya Girl Night.

akilazimisha namwambia aende na my sis au mdogo wake, I know she will behave
 
Nafikiri hoja yako ni maovu yanayofanywa kwenye the so called "girls night out"......nakubaliana na wewe kuna cases kama hizo kwamba watu wanaenda kutoa frustrations huko na kufanya vutu vya ajabu.....ila si kila girls night out wasichana wanafanya hivyo.....

Sidhani kama matendo ya hao wasichana wote yanakufikisha wewe kwenye point ya kuamua kuacha kuoa au kulala na wake za wanaume wenzio....hiyo ni tabia chafu na hakuna namna ya ku-justify.....kuna wanawake waliotulia ambao hawana hizo tabia,look for them...tatizo la wanaume wenye attitude ka zako mnaumiza hata wasichana waliotulia kwa fikra kuwa kila mwanamke hajatulia......
Mpashe onja onja huyo
 
kwa kweli itanibidi niishie kulipa mahari tu ndoa mh! Mh! Kitanzi.......akiwa siyo kwaheri.
 
wenye picha si ndio wahusika we vipi wewe,unaona kuna wa maana yeyote hapo?
Wenye hizo picha umewaomba kuzibandika hapa?


Tukirudi kwenye topic ,naona inategemea, kuna wengine wanao heshimu relationship zao na wasio heshimu.
 
Wenye hizo picha umewaomba kuzibandika hapa?


Tukirudi kwenye topic ,naona inategemea, kuna wengine wanao heshimu relationship zao na wasio heshimu.

Mie mgeni humu lakini nimeona kama sio sahihi kubandika hiyo picha hapa kwa sheria za JF nilizosoma kama nimezielewa vizuri au sijui nakosea
 
Mungu atusaidie wamama na dada mcharuko siku hizi ni wengi kuliko walio tulia! Ongezeko la uvutaji bangi kwa warembo limekuwa jambo la kawaida.........sijui tunakoelekea
 
tena micharuko iliyochakachuliwa,watu hawataki kukubali kuwa mwanamke na mwanaume wakiwa vicheche anayeonekana kicheche zaidi ni mwanamke
Mungu atusaidie wamama na dada mcharuko siku hizi ni wengi kuliko walio tulia! Ongezeko la uvutaji bangi kwa warembo limekuwa jambo la kawaida.........sijui tunakoelekea
 
Naomba hiizo picha alizoweka muanzisha mada ziondolewe au thread nzima ifutwe maana hamna uhusiano uliothibitishwa kati ya walio kwenye picha na shutuma zinazotolewa. Huku ni kuwachafulia sifa watu wasio na hatia. Hapa si Zeutamu ingawa inaelekea kuna wengine wangependa iwe hivyo!

Amandla......
 
Naomba hiizo picha alizoweka muanzisha mada ziondolewe au thread nzima ifutwe maana hamna uhusiano uliothibitishwa kati ya walio kwenye picha na shutuma zinazotolewa. Huku ni kuwachafulia sifa watu wasio na hatia. Hapa si Zeutamu ingawa inaelekea kuna wengine wangependa iwe hivyo!

Amandla......

Nami nimepata hofu hiyo, coz mmoja wapo namfahamu ni mke wa mwenzetu mmoja, sasa nashindwa kuelewa the outcome, manake mmh!
 
zinahusu sana tu tena ndo wahusika wakuu
Naomba hiizo picha alizoweka muanzisha mada ziondolewe au thread nzima ifutwe maana hamna uhusiano uliothibitishwa kati ya walio kwenye picha na shutuma zinazotolewa. Huku ni kuwachafulia sifa watu wasio na hatia. Hapa si Zeutamu ingawa inaelekea kuna wengine wangependa iwe hivyo!

Amandla......
 
kweli mamii halafu hawa watu wengi wao huwa wanapata wake wazuri waliotulia matokeo yake ni mateso tu kwa mwanamke.
Nimewahi kuona baadhi ya ndoa yaani mwanamke ametulia lakini mwanaume hashikiki utafikiri amechanjiwa.

Vice versa is also true.
 
Nafikiri hoja yako ni maovu yanayofanywa kwenye the so called "girls night out"......nakubaliana na wewe kuna cases kama hizo kwamba watu wanaenda kutoa frustrations huko na kufanya vutu vya ajabu.....ila si kila girls night out wasichana wanafanya hivyo.....

Sidhani kama matendo ya hao wasichana wote yanakufikisha wewe kwenye point ya kuamua kuacha kuoa au kulala na wake za wanaume wenzio....hiyo ni tabia chafu na hakuna namna ya ku-justify.....kuna wanawake waliotulia ambao hawana hizo tabia,look for them...tatizo la wanaume wenye attitude ka zako mnaumiza hata wasichana waliotulia kwa fikra kuwa kila mwanamke hajatulia......

Mmmh MCHELE??????!!!!.......mbona unaitetea mada ya MFANYWAJI?......
 
Bajeti ya Serikali yapigwa panga Send to a friend Sunday, 13 February 2011 09:21 digg

NI KWA AJILI YA KUFIDIA NAKSI YA BILIONI 640
Mwandishi Wetu
HALI mbaya ya uchumi imeilazimisha Serikali kufumua bajeti yake ya mwaka wa fedha 2010/11 kwa kupunguza matumizi ya Wizara ili kufidia upungufu wa Sh670.4 bilioni zilizotegemewa kupatikana kutokana na makusanyo ya kodi katika mwaka huu wa fedha.

Uamuzi huu ambao umetokana na kupungua mapato ya ndani ya mwaka huu wa fedha, umesababisha Serikali kupiga panga fedha za miradi ya maendeleo na za matumizi ya wizara zote.

Taarifa za kuaminika ambazo Mwananchi Jumapili imezipata, zinaeleza kuwa fedha hizo zinapunguzwa kutoka katika kila wizara kwa viwango tofauti kulingana na bajeti ya wizara husika, ili kufidia makusanyo ya kodi yaliyokusudiwa na kulipia mahitaji ya fedha za mishahara na kuwalipa makandarasi wa Barabara.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustaffa Mkullo, alipoulizwa kuihusina na hali hiyo alisema taarifa ya hali ya uchumi wa nchi alishaitoa hivi karibuni kwenye chombo kimoja nchini, hivyo hahitaji kuitoa tena.

"Nilitoa taarifa kwa wenzenu wa gazeti (sio Mwananchi) sasa siwezi tena kuirudia," alisema.

Habari hii inakuja wakati Serikali imeelezwa kuwa imetuma barua kwa nchi wafadhili kuziomba ziweze kuchangia miradi ya maendeleo katika bajeti yake.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Wizara ya Fedha na Uchumi (Hazina), imekuwa ikifanya vikao mbalimbali vya kujadili tathmini ya hali ya uchumi na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti tangu Desemba mwaka jana.

Katika vikao hivyo vilivyofanyika Januari11 hadi 24 mwaka huu ilibainika kuwa kuwepo kwa upungufu wa mapato kwa mwaka huu wa fedha unafikia Sh670.4 bilioni.

Kutokana na hali hiyo, Serikali imelazimika kupunguza fedha za matumizi kwa wizara zake, kiasi cha Sh480.51 bilioni ili kufidia upungufu huo.

Vile vile, itapunguza fedha za matumizi, kiasi cha Sh153 bilioni ili kuziba pengo la gharama za mishahara.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Serikali inahitaji kiasi cha Sh258 bilioni kulipa madai ya wakandarasi wa barabara na mkandarasi aliyekarabati Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku fedha hizo zikielezwa kuwa mikataba yake ilifanyika nje ya bajeti ya mwaka 2010/11.

Kwa mujibu wa chanzochetu cha habari, katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara, uliofanyika hivi karibuni kuliibuka mjadala juu ya kwanini malipo ya kandarasi ya barabara yaonekane kuwa ni ya dharura wakati kuna wizara ambazo pia zinadaiwa na wakandarasi.

Mvutano mwingine ulihusu kiwango cha fedha za matumizi ya wizara zilizopendekezwa kupunguzwa, kuwa ni kikubwa na kuwa hali hiyo itazifanya wizara kushindwa kuendesha shughuli zake kwa kipindi kilichobaki cha mwaka wa fedha.

“Kulitolewa mapendekezo kuwa badala ya serikali kupunguza kiwango hicho cha fedha kutoka katika kila wizara, inatakiwa iibane Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kuziba mianya inayosababisha kushindwa kufikia malengo ya makusanyo ya mapato,” kilisema chanzo hicho.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa mwezi huu alisema hali ya uchumi wa nchi ni nzuri na kwamba Serikali ina hazina ya kutosha ya fedha.

Hata hivyo, pamoja na mjadala huo mkali, Mwananchi Jumapili imebaini kuwa Wizara ya Fedha imesema Serikali haina budi kulipa deni hilo la kandarasi ya barabara linalofikia Sh250 bilioni ili kuendelea na kazi ya ujenzi wa barabara kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua.

Pia wizara hiyo imesema hali ya uchumi imeathiriwa na mgao wa umeme unaoendelea, na hivyo kuathiri mwelekeo wa kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.

Wachambuzi wa uchumi, Serikali kulazimika kupunguza bajeti yake kunatokana na kuwepo kwa matumizi mabaya na utoaji holela wa misamaha ya kodi iliyosababisha kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato.

Habari zilizopatikana kutoka mkutano wa wahisani na watendaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011, ulifanyika hivi karibuni zinaeleza kuwa Serikali ina upungufu wa Sh600 bilioni kutoka kwenye bajeti ya Sh11 trilioni, iliyopitishwa na Bunge mwaka jana.

Kati ya Sh11trilioni, Sh6 trilioni zilitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya mapato na kiasi kilichobaki kingetokana na fedha za wafadhili.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, John Haule, hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiwatoa hofu wananchi kwamba Serikali haina mpango wa kuwa na bajeti ndogo kukabiliana na hali hiyo.


Alisema Serikali inatarajia kuwa na mkutano wa kutathmini utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/11 ambao utatoa picha ya hali halisi ya uchumi wa taifa nchini.
 
Mnataka mtoke nyie tu wenyewe wakitoka wanawake ishu. lol girls night out kama kawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom