Hadithi; The girls in island -03

chiqutitta

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
1,160
3,124
SEHEMU YA TATU
THE GIRLS IN ISLAND 03

Kwakua alitambua kuwa malikia huyo hutumia muda mwingi katika hilo tendo. Walipoingia tu uwanjani, aliyatumia masaa matatu kumchezea malikia huyo ambaye alikua akihangaika huku miguno ya mahaba ikipamba tukio hilo.

Zoezi lake lilionekana kuanza kufanikiwa baada ya kumuona malikia akiwa amebadilisha mihenmo yake na kuhema bila mpangilio.

Kabla hajaanza kuingia dimbani, alijikuta amevutwa uwanjani huku muhsika mkuu akiwa malikia mwenyewe. Nusu saa baadae, alishangaa kuona ameng`ang`aniwa kwa nguvu na baadae ukulele mkali ukasikika mpaka nje ya kisiwa.

SONGA NAYO……………………

Ukulele huo ulifika mpaka chini ya bahari ambapo jini Kadash alikua ameweka makazi yake. Ilikua ni mara ya kwanza kwa Kadash kusikia sauti hiyo ya malikia. Alitoka na kuamua kwenda kuangalia nini kimetokea katika kisiwa chake. Alipofika alimuona malikia akiwa amechoka huku akiwa uchi wa mnyama. Alipotupa macho pembeni, alimuona pia mwanasayamsi akiwa hoi taabani. Pia nae alikua uchi.

Harufu ya janaba ilimshinda kadash kukaa mle ndani, alichoamua ni kuondoka huku akiwa amejawa na hasira.

Yalipita masaa matatu bila malikia kupata nguvu. Mpaka wapambe wake walipomchukua na kwenda kumuogesha ndipo nguvu ziliporejea. Aliamuru mwanasayansi Mac Donald aletwe mbele yake. Amri hiyo ilifuatwa na wapambe wake na kumfuata Mac Donald chumbani kwake na kumfikishia ujumbe kuwa anahitajika. Mac Donsld alifika kwa malikia na kukaa kwenye kiti alichoelekezwa akae.

“hivi unaja kuwa kuazia sasa unaweza kutawazwa kuwa mfalme wa kisiwa hiki cha wanawake?... maana mambo uliyoyafanya umefanya mpaka milima imetikisika. Yaani mpaka hivi sasa najiona mpya kabisa.” Aliongea malikia na kumtazama mwanasayansi kwa macho malegevu.

“yaani najisikia uchovu wa maana. Umewezeje kufanikiwa kunifikisha mahala ambapo sikuwahi kuota kama nitafika?” aliuliza malikia huku akiendelea kumuangalia Mac Donald.

“hata mimi mwenyewe sijui, labda kwakua hatujafanya mapenzi muda mrefu.” Aliongea Mac Donald ili ajipe nafasi ya kupumzika badala ya kufululiza kufanya mapenzi na malikia huyo aliyekuwa anamuhitaji kila usiku.

“kumbe!.. sasa tukipumzika kwa siku ngapi tunaweza kurudia mchezo kama huu?” aliuliza malikia na kumkazia macho yake ambayo hayakutisha, zaidi yaliongeza uzuri wa sura yake.

“japo siku tatu au nne, lakini chini ya hapo hatuwezi kufikia kiwango kama cha leo.”aliongea Mac Donald na kumfanya malikia atabasamu.

“basi sawa, unaweza kwenda kupumzika.” Aliongea malikia na Mack Donald akrudishwa kwenye chumba chake.

Usiku wa siku siku ya pili yake, jini Kadash alimtokea malikia na kumuamrisha kumtoa sadaka Mac Donald siku inayofuata. Taarifa hizo zilimuumiza kichwa malikia ambaye alishaanza kuona utamu halisi wa mwanasayansi huyo.

Hakuamini kuwa ile ndoto yake ilikua na ukweli ndani yake. Ingawaje jini Kadash mara zote humtokea kwenye ndoto na kumpa taarifa mbali mbali katika utawala wake.

Malikia akaamua kwenda kwenye chumba chake na kuwasha vitu vyake vya kijini na kumuita Jini Kadash. Baada ya muda, jini Kadash alifika huku sura yake ikiwa inaonyesha wazi kua alikua amekasirika.

“hata siku moja hujawahi kuniita na kuhakikisha niliyokuamrisha ufanye.. iweje katika hili unaniita na kuhitaji uhakika?” aliuliza Kadash kwa Hasira.

“nilikua na mawazo sana. Hivyo hata ulipokuja wewe nilihisi ni ndoto tu ya kawaida iliyonitokea.” Aliongea malikia kwa unyenyekevu.

“basi ndio hivyo, ukae ukijua kuwa usiku wa siku ya leo unahitajika utoe sadaka ya huyo mgeni aliyebakia.” Aliongea Kadash na kuondoka bila kusubiri jibu lolote kutoka kwa malikia.

Malikia alirudi kwenye kiti chake cha enzi na kuanza kufikiria. Hakua na uwezo wa kukataa amri ya Kadash kwakua yeye ndiye mmiliki mkuu wa kisiwa na ndio alikua analeta chakula na kila kitu wanachomiliki vipo chini yake.

Mawazo yalimrudisha mpaka siku ya jana yake alipokua mchezoni na kijana huyo aliyeikonga nafsi yake kisawasawa.

“hastahili kufa huyu kijana.”

Aliongea malikia huku akiwa anaisumbua akili yake kutafakari ni jinsi gani anaweza kumsaidia.

Masaa yalizidi kukatika kwa kasi huku kiza kwa mbali kilianza kulisogolea wingu na kubadilisha muonekano wa mchana uliokuwa umetawala kwa masaa kadhaa.

Malikia alitoka na kwenda kwenye chumba cha Mack Donald na kumgongea. Mac Donald alipofungua tu, malikia alimvuta na kumuanyeshea ishara iliyoashiria kuwa anyamaze.

Alimshika mkono na kuanza kutoka nae huku akitoa amri walinzi wasogee upande mwengine ili wasimuone Mac Donald akiwa anamtorosha.

“fanya haraka, maana kiza kikitawala zaidi uhai wako utakuwa matatani.” Aliongea Malikia huku akizidi kukimbia huku akiwa ameushika mkono wa Mac Donald.

“si bora ungesubiri kukuche ndio uniachie kama kutoroka usiku kunaweza kusababisa nikapoteza uhai?” aliongea Mac Donald huku akiendelea kukimbia.

“jini kadash amekasirika na sijui kwanini amekasirika hivyo. Amesema nikutoe kafara usiku wa leo. Kwangu mimi naona hustahili kufa.” Aliongea malikia na kuzidi kumkimbiza Mc Donald.

“ahsante sana.” Alishukuru Mac Donald na kumfuata malikia ambaye wakati huo walishafika kwenye pango.

Malikia alisimama na kumchukulia madini katika mkoba aliobeba na kumkabidhi Mac Donald. Alipo beba tu yale madini, lile jiwe kubwa la dhahabu lika funga njia ya kutokea. Malikia alifika pale na kulishika lile jiwe na kuongea maneno yasiyeleweka na lile jiwe likajifungua.

Malikia na Mac Donald wakaongeza mwendo japokuwa wamechoka ili mradi tu wawahi kabla giza halijatawala kabisa.

Walifanikiwa kufika baharini lakini hakukua na usafiri wowote wakati huo.

“sasa tutafanyaje?” aliuliza Mack Donald baada ya kuona hata ile helkopta yao waliyoenda nayo haikuwepo eneo hilo.

“unaniamini?” aliuliza malikia na kumshika mkono kwa nguvu Mac Donald.

“mpaka sasa nimeshakuamini vya kutosha.” Alijibu Mack Donald.

“basi fumba macho yako.”

Aliongea malikia na muda huo huo bila kuuliza kuwa alikua anataka afanywe nini, Mac Donald alifumba macho yake na kusubiri kitakachotokea kutoka kwa malikia. Ghafla Mac Donald akajikuta amebebwa huku upepo mkali ukimpuliza kama mtu aliyepanda boda boda iendayo kasi kwenye bara bara iliyonyooka.

Aliambiwa kama anaweza kufumbua macho basi anaruhusiwa. Mac Donald alifumbua macho ili apate kujionea mwenywe.

Alijikuta yupo mgongoni mwa yule malikia huku akiwa amelala juu yake na malikia akionekana akiwa yupo spidi kama roketi angani umbali mdogo kutoka usawa wa bahari. Wakiwa wapo angani, malikia aliona jeshi kubwa la Jini kadash likiwa nyuma yao linawafuata huku na wao wakiwa wanapaa kwa spidi kama yeye.

“safari njema mgeni, acha nipambane nao hawa vibaraka wa Kdash.” Aliongea Malikia na kumshusha Mac Donald kwenye maji na yeye akageuka na kuanza kurudi nyuma ambapo kulikua na jeshi la majini ya Kadash.

Malikia alianza kupambana nao kwa upanga maalumu aliokua katika mgongo wake na kuanza kuwashambulia kwa mbali kutokana na urefu wa panga hilo.

Alijitahidi kuwapukutisha mpaka akawamaliza wote na kutua salama katika ardhi ya kisiwa chao. Kabla hajafanya lolote, Kadash mwenyewe alishafika pale na kukutana uso kwa uso na malikia .

“kwa hiyo umejifanya mjuaji sana mpaka umeamua kukataa amri yangu na kuamua kumtorosha yule mgeni eeh?” aliuliza Kadash kwa hasira.

“huwezi kumchukua yule kijana kwakua hakukukosea kitu chochote.” Aliongea malikia huku akitweta kutokana na kazi nzito aliyoifanya ya kupambana na jeshi la majini ya Kadash.

“kwani wale uliowatoa sadaka walikua na makosa gani?” aliuliza Kadash kwaa hasira.

“hilo swali nikikuuliza wewe itakuwa sahihi sana, ilikuaje ukamuacha yule mgeni wakati tulitoa sadaka wote watatu?” aliuliza malikia na kumfanya Kadash anyamaze.

“hizo nguvu nilizokupa ndio zinakutia kiburi, sasa nitakuonyesha kuwa mimi ni bora zaidi yako.” Alioongea kadash na kutoa kitu kama chupa hivi ya kupimia mizani ambayo ndani yake ilikua na maji ya bluu.

Alimwagia malikia yale maji na hapo hapo malikia akaanza kulia kwa uchungu na nguvu zake zikaanza kupungua huku mwili wake ukipata majeraha makubwa.

Baada ya sekunde kadhaa, malikia alidondoka chini na kupoteza fahamu. Jini kadash alikirudisha kile kichupa kimazingara maeneo alipokitoa na kumshika mkono malikia aliyekua amelala pale chini na kuanza kumburuza mpaka kwenye uwanja wa wanawake hao.

Jini Kadash alipiga ukulele mkubwa uliowashtua wakazi wote wa kisiwa hicho na kukusanyika uwanjani kushuhudia yaliyojiri usiku huo.

Kwakua wote walikua wanazijua nafasi zao, walikaa kulingana na matabaka yao na kumyamaza ili kusikiliza wito huo wa mmiliki wa kisiwa chao.

“kuanzia leo, nimevunja utawala wa malikia SUBBI kutokana na utovu wake wa nidhamu kwa kukaidi kuniletea sadaka. Hivyo nimemnyang`anya uwezo wake wote wa kutawala na nimeuchukua mwenyewe. Kuanzia leo hii kisiwa kitaanza kutawaliwa na majini kamili na mimi ndio nitakua malikia mkuu wa kisiwa hiki. Hivyo natangaza kuvunja uongozi wote kuanzia juu mpaka chini na nitawapa majini kamili kwakua wananitii na hawajawahi kunisaliti.” Aliongea Kadash na kuwatawanya wakazi wote wa kisiwa hicho.

*******************

Baada ya Mac Donald kushushwa kwenye maji, kwa bahati nzuri alikua anaweza kuogelea. Alipiga mbizi taratibu huku akiomba mungu aweze kupata msaada wa boti au meli itakayopita karibu na maeneo hayo.

Haukupita muda mrefu, ikatokea boti na kumuokoa Mac Donald na kumfikisha salama katika bandari ya salama katika jiji la Dar-es-salaam.

Mac Donald hakuamini kuwa angeweza kufika salama kutoka katika kisiwa hicho cha wanawake.

Hakumruhusu mtu yeyote kulishika begi lake ambalo lilikua na utajiri wa maana ambao hakuna mtu yeyote aliyekua anajua siri iliyokuwemo katika kile kibegi kidogo alichopewa na malikia Subbi zaidi yake yeye mwenyewe..

Kwakua walifika alfajiri, mwanasayansi huyo hakuona haja ya kupoteza muda kule bandarini. Aliamua kutembea huku akiulizia mahala ambapo panachongwa pete na mikufu ya dhahabu.

Baada ya kufanikiwa kufika sonara, aliingia na kutoa kipande kimoja cha dhahabu kilichokuwa na thamani ya dola tano ambayo ilikua kubwa sana kwa kipindi hiko.

Mwenye sonara alikosa kiasi hicho cha fedha. Kwakua Mac Donal alikua anashida sana na kurudi kwao marekani. Aliamua kuchukua kiasi cha dola mbili alizokuwa nazo sonara na kuwenda uwanja wa ndege na kutumia dola moja tu mpaka kukamilisha safari ya marekani.

Alifika kwao na kupokelewa na waandishi wa habari walikua wanafahamu safari ya watafiti hao wa kimarekani waliondoka na kwenda bara la Afrika kwenda kuhakikisha uwepo wa kisiwa kilichoibuka ghafla ili waweze kuirekebisha ramani ya dunia na kukingiza kisiwa hicho.

Taarifa za vifo vya watafiti nane kati ya tisa waliokwenda kwenye kisiwa hicho cha maajabu, kiliwahuzunisha sana wanafamilia na wanasayansi wengine waliobakia kule marekani.

Majibu ya maswali ya waandishi wa habari yalikua kwa vitendo baada ya mwanasayansi Mac Donald kuwaonyesha madini ya aina mbali mbali ambayo hata mengine hawakuwahi kuyaona.

Ndani ya mwezi mmoja tu, ulitosha kabisa kumpa umaarufu Mac Donald kutokana na utajiri aliokuwa nao na kuvumbua madini ya aina mbali mbali ambayo aliyapa majina yeye mwenyewe.

Haikuishia hapo, kitabu chake cha THE GIRLS IN ISLAND kilimpa umaarufu sana katika pande zote za dunia kutokana na watu wengi sana kuwa na kiu ya kukifahamu kisiwa hicho cha maajabu kilichokuwa katika bara la Afrika katikati ya nchi ya Tanzania na Comoro.
 
asante,naona unatutendea haki,lete utamu
 
Back
Top Bottom