Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,973
Soma Unaweza jifunza Kitu...
"Dr. Mpango alienda bungeni kama Waziri wa fedha. Kufumba na kufumbua akawa VP, akaondoka na ving'ora, msafara na ulinzi mkali. Maisha ndivyo yalivyo. Nothing is permanent in life. Kila kitu unachokiona kwenye maisha ni cha kupita tu. Hivyo ishi vizuri na watu.
Jana hadi saa 8 mchana Dr. Bashiru alikua boss wa watumishi wote wa umma na Katibu wa Baraza la usalama wa taifa. Yani Rais asingeweza kutangaza vita bila kushauriana kwanza na Bashiru. Alikua raia namba 4 baada ya Rais, VP na PM.
Jana ameenda Ikulu ya Chamwino akiwa na msafara, king'ora na ulinzi mkali kwa hadhi ya raia namba 4. Lakini ametoka hana ulinzi, hana king'ora, hana gari, hana dereva. Ameanza maisha mapya leo.
Kwa miaka minne amekaa Masaki kwenye nyumba ya Katibu Mkuu wa CCM, kisha akahamia jumba la kifahari la CS Ikulu. Ghafla leo anarudi kwenye nyumba yake pale Ubungo Msewe, hana ulinzi, hana msafara, hana gari.
FUNZO;
1. Rais Mwinyi (baba) aliwahi kusema madaraka ni kama koti la kuazima. Usilivae kwa mbwembwe, ipo siku mwenye nalo atalihitaji. Bashiru aliwahi kutamba kuwa CCM itatumia DOLA kubaki madarakani. Na kweli uchaguzi mkuu 2020 tuliona jinsi walivyotumia DOLA kubaki. Lakini sasa anarudi zake Ubungo Msewe hana DOLA wala paundi.
2. Maisha ni kupanda na kushuka. Ukiwa juu usidharau walio chini kwa sababu ndio watakaokudaka siku ukianguka.
3. Bashiru alipoteuliwa kuwa CS mitandao ilijaa pongezi. Vijana wa CCM wakampamba ktk profile zao, na wengine wakadai alikua mwalimu wao UDSM. Lakini leo amebaki peke yake. Wale vijana wameshaondoa "profile picture" na kufuta yale maandiko ya pongezi. Hii inatufundisha "mchuma janga hula na wa kwao" Utapata wapambe wengi ukiwa na madaraka, pesa au umaarufu. Lakini vikiondoka utabaki peke yako.
4. Bashiru aliteuliwa GS wa CCM bila hata kuwa kiongozi wa tawi. Yani kutoka Mwanachama wa kawaida hadi GS. Then akawa CS Ikulu bila kuwa mtumishi wa umma. Yani alipanda kirahisi sana. Na leo ameporomoka kirahisi pia. Wahaya husema "Easy come, easy go"
5. Ukimtegemea mwanadamu ipo siku ataondoka na utakosa pa kuegemea. Mtegemee Mungu pekee na ishi vizuri na watu wote. Vijana wa Manzese husema "heshimu watu, sponsor hufariki"
Credits: Malisa GJ