Watawala jifunzeni kitu kutoka kwa Dkt. Bashiru Ally

Nothing is permanent in life. Kila kitu unachokiona kwenye maisha ni cha kupita tu. Hivyo ishi vizuri na watu.
Bandiko lako liko sawa ila limekaa kimipasho kama maneno ya kwenye kanga... uswahili.

Kuishi vizuri na watu ni kufanyaje!?
Jambo la msingi elewa kila binadamu ana mitizamo tofauti na mwingine katika jambo lolote lile.

Unaweza kufanya jambo ukafikiri unamfurahisha mtu, yeye akukuchukulia tofauti kabisa

Ishi maisha yako upendavyo bila kuvunja sheria.
Mengine uliyozungumza yote ni hali halisi ya maisha..hakuna jipya.
 
Huyo Bashiru, kimsingi hakuwa ccm yeye alikuwa Cuf na ni Magufuli ndiye aliyemleta ccm na kumpa ukatibu mkuu kwa sababu Magufuli alikuwa muumini wa siasa za ukanda.

Ccm walilijua hilo na hawakumpenda kabisa Bashiru ila kwa ubabe wa Magufuli hawakuwa na cha kufanya ilibidi wameze tu pini.

Bashiru ambaye alikuwa ni Magufuli "Protege" alikuwa na tamaa kwamba aje awe rais wa Tanzania siku moja labda baada ya Magufuli kuondoka lakini hiyo ilikuwa ni ndoto yake tu na Mungu alikuwa na mipango yake tofauti na alivyokuwa anafikiria.

Inaonekana pia kwamba alipokuwa katibu mkuu alikuwa akiwanyanyasa wana ccm wengi kwa kiburi na jeuri huku akitegemea ulinzi wa Magufuli. Sasa ameanza safari nyingine ya kisiasa ambayo huenda haitakuwa rafiki sana kwake kwani walimtegemea mtu na wakampuuza Mungu.

In such a scenario there is always a price to pay.
 
Bashiru hakupaswa hata kupewa kazi ya kufungua mlango wa CS.

Naamini after 2025 atarudi UD kufundisha.
 
Bandiko lako liko sawa ila limekaa kimipasho kama maneno ya kwenye kanga... uswahili.

Kuishi vizuri na watu ni kufanyaje!?
Jambo la msingi elewa kila binadamu ana mitizamo tofauti na mwingine katika jambo lolote lile.

Unaweza kufanya jambo ukafikiri unamfurahisha mtu, yeye akukuchukulia tofauti kabisa

Ishi maisha yako upendavyo bila kuvunja sheria.
Mengine uliyozungumza yote ni hali halisi ya maisha..hakuna jipya.
Hivi wewe ubongo upo kichwani kweli? Au umebakiwa na MAKAMASI pekee kichwani??
 
Soma Unaweza jifunza Kitu...

"Dr. Mpango alienda bungeni kama Waziri wa fedha. Kufumba na kufumbua akawa VP, akaondoka na ving'ora, msafara na ulinzi mkali. Maisha ndivyo yalivyo. Nothing is permanent in life. Kila kitu unachokiona kwenye maisha ni cha kupita tu. Hivyo ishi vizuri na watu.

Jana hadi saa 8 mchana Dr. Bashiru alikua boss wa watumishi wote wa umma na Katibu wa Baraza la usalama wa taifa. Yani Rais asingeweza kutangaza vita bila kushauriana kwanza na Bashiru. Alikua raia namba 4 baada ya Rais, VP na PM.

Jana ameenda Ikulu ya Chamwino akiwa na msafara, king'ora na ulinzi mkali kwa hadhi ya raia namba 4. Lakini ametoka hana ulinzi, hana king'ora, hana gari, hana dereva. Ameanza maisha mapya leo.

Kwa miaka minne amekaa Masaki kwenye nyumba ya Katibu Mkuu wa CCM, kisha akahamia jumba la kifahari la CS Ikulu. Ghafla leo anarudi kwenye nyumba yake pale Ubungo Msewe, hana ulinzi, hana msafara, hana gari.

FUNZO;
1. Rais Mwinyi (baba) aliwahi kusema madaraka ni kama koti la kuazima. Usilivae kwa mbwembwe, ipo siku mwenye nalo atalihitaji. Bashiru aliwahi kutamba kuwa CCM itatumia DOLA kubaki madarakani. Na kweli uchaguzi mkuu 2020 tuliona jinsi walivyotumia DOLA kubaki. Lakini sasa anarudi zake Ubungo Msewe hana DOLA wala paundi.

2. Maisha ni kupanda na kushuka. Ukiwa juu usidharau walio chini kwa sababu ndio watakaokudaka siku ukianguka.

3. Bashiru alipoteuliwa kuwa CS mitandao ilijaa pongezi. Vijana wa CCM wakampamba ktk profile zao, na wengine wakadai alikua mwalimu wao UDSM. Lakini leo amebaki peke yake. Wale vijana wameshaondoa "profile picture" na kufuta yale maandiko ya pongezi. Hii inatufundisha "mchuma janga hula na wa kwao" Utapata wapambe wengi ukiwa na madaraka, pesa au umaarufu. Lakini vikiondoka utabaki peke yako.

4. Bashiru aliteuliwa GS wa CCM bila hata kuwa kiongozi wa tawi. Yani kutoka Mwanachama wa kawaida hadi GS. Then akawa CS Ikulu bila kuwa mtumishi wa umma. Yani alipanda kirahisi sana. Na leo ameporomoka kirahisi pia. Wahaya husema "Easy come, easy go"

5. Ukimtegemea mwanadamu ipo siku ataondoka na utakosa pa kuegemea. Mtegemee Mungu pekee na ishi vizuri na watu wote. Vijana wa Manzese husema "heshimu watu, sponsor hufariki"

Credits: Malisa GJ
Hakika mkuu 🙏
 
Are you saying huu ndiyo ushauri wa Tanganyika Law Society? Walisema tupige kura in 14 days
 
Ukimtegemea mwanadamu ipo siku ataondoka na utakosa pa kuegemea...

Mtegemee Mungu pekee na ishi vizuri na watu wote.

Vijana wa Manzese husema "heshimu watu, sponsor hufariki"
 
Bashiru hakupaswa hata kupewa kazi ya kufungua mlango wa CS.

Naamini after 2025 atarudi UD kufundisha.
Kwa hiyo sifa kianzio ya kupata kazi ya kufunga mlango wa CS: NI kusoma mpaka level ya PhD, ukafundisha miaka 20 chuo kikuu na kupata promotion na ukawa Senior lecturer na uwe mkuu wa Idara ?.

KWELI MFUNGUA MLANGO WA CS NI KAZI INAYOLIPA.
 
Sikutaja elimu yake, nimemtaja mtu. Unaweza kuwa na elimu zooote duniani, na ukawa hustahili kuwa mtendaji wa kijiji.
 
Sasa elimu nzuri na bora pamoja na uzoefu wa uongozi unafaida gani kwa sisi watanzania kama ambavyo ushauri bora kutoka kwako mheshimiwa unavyo tushauri ?

Mbona sisi ambao tunajua kusoma na kuandika tukiomba kazi serikalini ya kufangia vyoo tunambiwa elimu ya kianzio kwa ajira Serikalini ni Certificate of Secondary Education na upate ufaulu wa masomo ya angalau matatu?

Kwa hiyo wanatuonea tuu, kwa kuwa sio lazima elimu,na makinda yangu nitawataka warudi nyumbani baada ya Pasaka hii, shule haina maana.

Duuuuh dunia chungu sana, tulio kwepa umande tunapigwa dana dana.

Asante mheshimiwa kwa ushauri murua na nitakusikiliza na kufuata ushauri wako elekezi, na Mungu aku ongezee hekima.
 
Kitendo cha Bashiru kuondolewa ikulu moja kwa moja naamini kuna tukio baya alifanya (lile linalosemwa kuhusu kuchota pesa zetu), lakini ningependa zaidi uchunguzi wa hilo tukio ukikamilika na kukutwa na hatia watuhumiwa wote wapelekwe mahakamani ili iwe fundisho kwa wote wanaoiona Tanzania ni shamba la bibi.

Tabia ya kulindana ndio inasababisha matukio ya aina hii yaendelee kuwepo kila awamu, watu wanazidi kuamini wakipata nafasi za juu serikalini ni kama wamesogezwa mdomoni zaidi kuiba mali za umma, huu mtazamo ni vyema ukomeshwe, kuanzia sasa yeyote anaepatikana na hatia apelekwe mahakamani sheria ichukue mkondo wake.
Mkui nani wa kuwapeleka Mahakamani?? "Bia ni ile ile tofauti chupa"
 
Sijakuelewa unamaanisha nini kwani ulikuwa na chuki na bashiru?

Je, umeuona mwisho wa bashiru na hukumu yake unayo wewe?

Kama mpango ameweza kuwa VP unadhani bashiru muda wake umeisha?

Ukitumia akili utajua huna mandeti ya kumzungumzia bashiru, bado ana muda ambao wewe siku moja ukakasirika akiwa Raisi wa nchi hii kwa hiyo mapenzi yako ya moyo hayana tija.

Huwezi mpangia mtu mwisho wa maisha yake.

Bashiru bado anayo nafasi ya kuwa kiongozi wa nafasi ya juu sana ndani ya nchi hii.

Hizo chuki zako ndo zitakutoa roho wewe mwenyewe.
Rais yupi labda wa nchi ya Karagwe. Hivi huoni?? Bashiru kwisha habari yake kama ule uwanja wa Chato.
 
4. Bashiru aliteuliwa GS wa CCM bila hata kuwa kiongozi wa tawi. Yani kutoka Mwanachama wa kawaida hadi GS. Then akawa CS Ikulu bila kuwa mtumishi wa umma. Yani alipanda kirahisi sana. Na leo ameporomoka kirahisi pia. Wahaya husema "Easy come, easy go"

Credits: Malisa GJ
Hivi mwalimu wa Chuo Kikuu cha Umma huwa siyo mtumishi wa umma?

Kwa maoni yangu mimi ni kuwa hakuwahi kupendelewa wala hajaonewa, na wala hatawahi kuja kupendelewa wala kuonewa. System ya nchi huwa haiwezi kuonea wala kupendelea mtu. Aombe Mungu tu baada ya hapa kusije kukajitokeza chochote kisichokuwa cha kawaida mbele ya safari. Nampa hongera nyingi sana kwa kuteuliwa kuwa Mbunge
 
Sasa elimu nzuri na bora pamoja na uzoefu wa uongozi unafaida gani kwa sisi watanzania kama ambavyo ushauri bora kutoka kwako mheshimiwa unavyo tushauri ?

Mbona sisi ambao tunajua kusoma na kuandika tukiomba kazi serikalini ya kufangia vyoo tunambiwa elimu ya kianzio kwa ajira Serikalini ni Certificate of Secondary Education na upate ufaulu wa masomo ya angalau matatu?

Kwa hiyo wanatuonea tuu, kwa kuwa sio lazima elimu,na makinda yangu nitawataka warudi nyumbani baada ya Pasaka hii, shule haina maana.

Duuuuh dunia chungu sana, tulio kwepa umande tunapigwa dana dana.

Asante mheshimiwa kwa ushauri murua na nitakusikiliza na kufuata ushauri wako elekezi, na Mungu aku ongezee hekima.
Kwenye original post, lugha niliyoandika ni figurative speech. Uteuzi wa Bashiru kwenye nafasi ya KMK, pengine ndio uteuzi wa ajabu sana kufanywa na Magufuli, kama angetoka UD moja moja kwenda kuwa KMK angestahili kabisa, maana ana sifa zote. Lakini kitendo cha kumtoa kwenye mtendaji mkuu wa chama, kwenda kuwa mtendaji mkuu wa serikali ilikuwa ni big mistake, hakupaswa kabisa.

Mama amerudisha kazi kwa watu wanaotakiwa, Career Civil Servant. Haiwezekani mtu, jana alikuwa anatunga mbinu za kuua vyama vya upinzani, leo unampa kazi ya kuratibu dola. It was a big mistake.
 
I certainly understand you now. In your past contribution on this matter did not give good value to good education and experience.
That's why my expression on the subject was to be read from the reverse to get the true meaning. .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom