Watawala jifunzeni kitu kutoka kwa Dkt. Bashiru Ally

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Soma Unaweza jifunza Kitu...

"Dr. Mpango alienda bungeni kama Waziri wa fedha. Kufumba na kufumbua akawa VP, akaondoka na ving'ora, msafara na ulinzi mkali. Maisha ndivyo yalivyo. Nothing is permanent in life. Kila kitu unachokiona kwenye maisha ni cha kupita tu. Hivyo ishi vizuri na watu.

Jana hadi saa 8 mchana Dr. Bashiru alikua boss wa watumishi wote wa umma na Katibu wa Baraza la usalama wa taifa. Yani Rais asingeweza kutangaza vita bila kushauriana kwanza na Bashiru. Alikua raia namba 4 baada ya Rais, VP na PM.

Jana ameenda Ikulu ya Chamwino akiwa na msafara, king'ora na ulinzi mkali kwa hadhi ya raia namba 4. Lakini ametoka hana ulinzi, hana king'ora, hana gari, hana dereva. Ameanza maisha mapya leo.

Kwa miaka minne amekaa Masaki kwenye nyumba ya Katibu Mkuu wa CCM, kisha akahamia jumba la kifahari la CS Ikulu. Ghafla leo anarudi kwenye nyumba yake pale Ubungo Msewe, hana ulinzi, hana msafara, hana gari.

FUNZO;
1. Rais Mwinyi (baba) aliwahi kusema madaraka ni kama koti la kuazima. Usilivae kwa mbwembwe, ipo siku mwenye nalo atalihitaji. Bashiru aliwahi kutamba kuwa CCM itatumia DOLA kubaki madarakani. Na kweli uchaguzi mkuu 2020 tuliona jinsi walivyotumia DOLA kubaki. Lakini sasa anarudi zake Ubungo Msewe hana DOLA wala paundi.

2. Maisha ni kupanda na kushuka. Ukiwa juu usidharau walio chini kwa sababu ndio watakaokudaka siku ukianguka.

3. Bashiru alipoteuliwa kuwa CS mitandao ilijaa pongezi. Vijana wa CCM wakampamba ktk profile zao, na wengine wakadai alikua mwalimu wao UDSM. Lakini leo amebaki peke yake. Wale vijana wameshaondoa "profile picture" na kufuta yale maandiko ya pongezi. Hii inatufundisha "mchuma janga hula na wa kwao" Utapata wapambe wengi ukiwa na madaraka, pesa au umaarufu. Lakini vikiondoka utabaki peke yako.

4. Bashiru aliteuliwa GS wa CCM bila hata kuwa kiongozi wa tawi. Yani kutoka Mwanachama wa kawaida hadi GS. Then akawa CS Ikulu bila kuwa mtumishi wa umma. Yani alipanda kirahisi sana. Na leo ameporomoka kirahisi pia. Wahaya husema "Easy come, easy go"

5. Ukimtegemea mwanadamu ipo siku ataondoka na utakosa pa kuegemea. Mtegemee Mungu pekee na ishi vizuri na watu wote. Vijana wa Manzese husema "heshimu watu, sponsor hufariki"


Credits: Malisa GJ
 
Jana hadi saa 8 mchana Dr.Bashiru alikua boss wa watumishi wote wa umma na Katibu wa Baraza la usalama wa taifa. Yani Rais asingeweza kutangaza vita bila kushauriana kwanza na Bashiru. Alikua raia namba 4 baada ya Rais, VP na PM.

Jana ameenda Ikulu ya Chamwino akiwa na msafara, king'ora na ulinzi mkali kwa hadhi ya raia namba 4. Lakini ametoka hana ulinzi, hana king'ora, hana gari, hana dereva. Ameanza maisha mapya leo.
Saivi Bashiru yupo level moja na Msukuma, Kibajaji & co
 
Kitendo cha Bashiru kuondolewa ikulu moja kwa moja naamini kuna tukio baya alifanya (lile linalosemwa kuhusu kuchota pesa zetu), lakini ningependa zaidi uchunguzi wa hilo tukio ukikamilika na kukutwa na hatia watuhumiwa wote wapelekwe mahakamani ili iwe fundisho kwa wote wanaoiona Tanzania ni shamba la bibi.

Tabia ya kulindana ndio inasababisha matukio ya aina hii yaendelee kuwepo kila awamu, watu wanazidi kuamini wakipata nafasi za juu serikalini ni kama wamesogezwa mdomoni zaidi kuiba mali za umma, huu mtazamo ni vyema ukomeshwe, kuanzia sasa yeyote anaepatikana na hatia apelekwe mahakamani sheria ichukue mkondo wake.
 
My due respect mkuu. You nailed it. Akaguliwe na uraia maana kwa mateso yale kwa watanzania bila huruma huenda hana damu ya kitanzamia. You can't be such rude creature. Waliangamiza utanzania wetu wa upendo na Mshikamano. Tunaanza upya na kwa haraka Mwanga tunauona tena. Long live our President Samia Suluhu Hassan. Natabasamu.
 
Sijakuelewa unamaanisha nini kwani ulikuwa na chuki na bashiru?

Je, umeuona mwisho wa bashiru na hukumu yake unayo wewe?

Kama mpango ameweza kuwa VP unadhani bashiru muda wake umeisha?

Ukitumia akili utajua huna mandeti ya kumzungumzia bashiru, bado ana muda ambao wewe siku moja ukakasirika akiwa Raisi wa nchi hii kwa hiyo mapenzi yako ya moyo hayana tija.

Huwezi mpangia mtu mwisho wa maisha yake.

Bashiru bado anayo nafasi ya kuwa kiongozi wa nafasi ya juu sana ndani ya nchi hii.

Hizo chuki zako ndo zitakutoa roho wewe mwenyewe.
 
Kitendo cha Bashiru kuondolewa ikulu moja kwa moja naamini kuna tukio baya alifanya (lile linalosemwa kuhusu kuchota pesa zetu), lakini ningependa zaidi uchunguzi wa hilo tukio ukikamilika na kukutwa na hatia watuhumiwa wote wapelekwe mahakamani ili iwe fundisho kwa wote wanaoiona Tanzania ni shamba la bibi.
Bashiru hajachota, anarudishwa Lumumba kukiongoza chama. Wamejipanga vyema kinyume na yaliyokuwa matarajio ya adui zao.
 

Similar Discussions

49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom