SoC01 Watanzania wengi tumeshindwa kufanya mambo kwa sababu tumekuwa walalamikaji

Stories of Change - 2021 Competition

Gwanxoo

Member
Jan 24, 2021
9
3
Kama ilivyo ada Leo nakuja na hizi tafakuri alafu ujitafakari...watanzania wengi tumeshindwa kufanya mambo kwa sababu tumekuwa walalamikaji sana.

Hahaha kuna jamaaa nilikutana nae analalamika mpaka analaumu kwanini kazaliwa kwenye ukoo alioko...daaah laana hii..lakini Leo tutafakari je kulalamika sana ndio kutatua changamoto. Kwa kawaida kulalamika ni njia ya kueleza tatizo unaloliona ila sio njia ya kutatua tatizo unaloliona..mfano mtu anashikilia bango huku anaimba au analia na lile bango Lina ujumbe kinachofanyika ni kwamba anaesoma anaona tatizo lakini kama hana akili ya kutatua tatizo basi ataumia au atapuuzia maisha yataendelea....

Watanzania tumekuwa tunalalamika mpaka basi yani mtu analalamika kuanzia Babu, Baba, familia, majamaa na marafiki, mkoa, kabila, mpaka anafikia analalamikia nchi, anatamani angezaliwa...dah nimekutana na watu wa aina hii...okay sio mbaya..

Sasa basi kulalamika sana hakuleti mabadiliko ya aina yoyote zaidi ya maumivu na kama ilivyo ada maskini hasikilizwi, sasa tufanye nini ili mtu abadilike au abadilishe tu mfumo bila watu kulalamika wala nini....

Okay njia ziko nyingi lakini kwa kuanza ni muhimu kuanza na wachache kubadilisha wengi. Hivyo tukaanza ndani ya familia kwanza kuleta mabadiliko, ili watu wasilalamikie familia, tukaenda ngazi ya mkoa yani kwa kila mkoa watu wa huo mkoa wao binafsi kuwa na vipaumbele wanavyotaka kwa viongozi wa mikoa, na kama hafanyi tuwe na uwezo wa kumbadilisha, sio mpaka Rais, kisha itakuwa rahisi kufika ngazi ya taifa...na pia siasa.....ifanyiwe namna Fulani hivi...taizungumzia wakati ujao
 
Back
Top Bottom