Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 260
- 712
Habari ya kutwa nzima wana Jamii Forums
Nayaongea haya nikiwa miongoni mwa watanzania wachache wanaochukizwa na hili swala. Watanzania wengi ni watu malalamiko. Katika kila jambo, kila mada, kila hatua ni wazee wa kulalamika bila kutafuta suluhu.
Nimefanya uchunguzi mdogo tu nikagundua hili linaanzia hasa kwenye familia zetu. Mfano mdogo tu mtoto akifeli darasani utasikia mzazi akisem "yaani mimi nalipa ada, nakupa nauli kila siku alafu unaenda kuleta haya madudu"
Ni kweli pesa ni chungu lakini kwanini usitumie nguvu kubwa kumuuliza kwanini anafeli? Ujue tatizo ni nini ulitatue kabla haijawa too late.
Ukimlalamikia mtoto ndo itakuaje? Yale matokeo yatabadilika? Hayo ndo kashayapata, tafuta njia ya kufanya asiyalete tena hayo madudu.
Achana na familia rudi mtaani:- watu wanalalamikia serikali kila kukicha, watu wanalalamikia timu za mpira, mara dini mara sijui vitu gani kedekede.
Unajua linapokuja jambo alafu ukaanza kwa kulalamika basi kufikia utatuzi itachukua miaka. Kulalamika maana yake ni unakataa kosa au unatupia kosa kwa mtu mwengine, au unakwepa jukumu, kiufupi kulalamika sawa na sifuri.
Angalia Adam alivyoulizwa na Mungu kwanini amekula tunda aliloambiwa asile, Adam alijibu vipi?....Si huyu mwanamke ulienipa ndo amenishawishi. Adam akalalamika kwa Mungu kuwa Eva/Hawa ndo chanzo.
Em waza Adam alivyoulizwa hivyo angemwambia tu Mungu naomba unisamehe, ni kweli nimekula na nimekukosea sana nakuahidi hili halitojirudia tena. Huenda yote yale malaana yasingetokea, Mungu ni mkuu hata yeye anasema ombeni nanyi mtapewa, Adam angeomba msamaha tusingefika hapa.
Kwa Adam ngoja niishie hapa, isje kuonekana na mimi namlalamikia Adam kwa hali tuliyonayo sasa.
Nachotaka kuwakumbusha ndugu zangu tujaribu kuiacha hii tabia, si nzuri na inapunguza kasi ya kuleta maendeleo. Akili yetu ijikite katika kutatua tatizo kwanza na sio kulalamika.
Iwe kwenye familia zetu, jamii zetu, makanisani, misikitini, kokote kule tutakapokuwa.
Unalalamika serikali haikupi ajira, ukilalamika itakupa? Ipe serikali sababu ya kukupa ajira. Unalalamika maisha magumu, ukialalmika yatakuwa mepesi? Pambana, hali isipokuwa nzuri leo basi tumaini kesho itakuwa poa.
Ikizidi kuwa ngumu jiulize unakosea wapi, ukijua wapi unakosea utapata utatuzi mzuri sana wa kujiinua aidha kiuchumi, kiafya na kwa jambo lolote linakusibu.
Makazini maboss wanalalamika, unarudi nyumbani mke/mume analalamika, watoto wanalalamika, unasema ufungue kiduka wateja wanalalamika. Woooooi