Watanzania wazuiliwa kucheza bahati nasibu ya kupata ukazi wa kudumu (Green Card) Marekani

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,293
2,000
Kwa msaada tu wale wenzangu na mimi wa enzi zile tunaandika S/M Mtakuja tukimaanisha Shule ya Msingi Mtakuja.
Carnal knowledge ni kujamiiana kwa kuingiza naniliu ya ME.
 

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
3,062
2,000
Serikali ya Marekani imepiga marufuku raia wa Tanzania kushiriki katika bahati nasibu ya kupata viza ya kuingia Marekani(US Green Card DV Lottery).

Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya serikali ya Trump kumpiga marufuku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingia nchini humo.

Bahati nasibu hiyo hutoa viza kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.

Nchi ya Sudani pia raia wake wamepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Wakati huo huo raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani.

Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan.

Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa.

Ni taifa moja tu la Belarus ambalo lilitajwa katika rasimu ya awali ambalo halijaorodheshwa katika taarifa za leo.

Afisa wa ngazi ya juu nchini Marekani amesema kuwa nchi hizo sita zimeshindwa kufikia "kiwango stahiki cha usalama na kupashana taarifa".

"Nchi hizi, kwa sehemu kubwa, zinataka kutoa msaada lakini kwa sababu mbali mbali zimefeli kufikia viwango vya chini tulivyoviweka," Naibu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Chad Wolf amewaambia wanahabari siku ya Ijumaa.

Nchi hizo mpya zinaungana na nchi nyengine saba ambazo raia wake wamepigwa marufuku kuingia Marekani toka mwaka 2017.

Nchi hizo, nyingi zikiwa na raia wengi Waislamu ni Libya, Iran, Somalia, Syria, Yemen.

Aidha nchi za Korea Kaskazini na Venezuela pia zimo kwenye marufuku hiyo.

Chanzo:BBC
 

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
22,094
2,000
Nasema hivi Laaaanakum BASHITE

Hatari yote kisa BASHITE mie nilishajiandaa ku'apply ifikapo hiyo octoba.
Bashite mwana hiyana sana
 

Asherymdudu

Member
Jul 13, 2018
19
75
Naona watu wanajadili zuio la Makonda kuingia Marekani badala ya kujadili sababu zilizopelekea hilo zuio. Wenye akili ndogo wameanza kusema "Kwani Marekani ni mbinguni? Kwani asipoenda atapungukiwa nini?" Hii ni comment ya Mbunge mmoja wa CCM kule Twitter.

Lakini hoja si Makonda kuzuiwa kuingia Marekani au kuingia Chato. Hoja ya msingi ni madai yaliyotolewa na Marekani kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Makonda.

Pamoja na mambo mengine, Pompeo amesema Marekani ina USHAHIDI kuwa Makonda ameshiriki KUDHULUMU HAKI YA KUISHI KWA WATU KADHAA. Hii ni kauli ngumu sana, inayotafakarisha sana.

Kudhulumu haki ya watu kuishi means kuamua kumuondolea mtu uhai kabla ya wakati wake. Je ni kweli Makonda amefanya hayo? Kwa akina nani? Kwa ruhusa ya nani? Kwa sababu gani? Lini? Wapi? Na kwanini?

Kumbuka taifa lenye teknolojia kubwa kama Marekani linaposema lina USHAHIDI juu ya jambo fulani bila shaka limejiridhisha vya kutosha.

Kwahiyo ili tuwe na mjadala wenye tija tuachane na kujadili zuio, tujadili sababu zilizopelekea hilo zuio. Hata kama asingezuiwa kwenda Marekani, lakini tuhuma alizotajwa nazo ni kubwa sana. Zinaogofya, zinatafakarisha, zinatisha. Kumbuka Marekani imesema ina USHAHIDI na kumbuka Pompeo alikua Mkurugenzi wa CIA kabla ya kuwa Waziri.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Lyaule Kitundu

JF-Expert Member
May 25, 2011
757
1,000
ngoja tuone watumwa wa fikra wakishabikia ujambazi wa marekani,

Marekani ikisema demokrasia, ujue kuna taifa litaumizwa kwa vita na kuondolewa katika misingi yake.

Sote ni mashahidi wa namna kete ya Demokrasia ilivyotumika vyema na marekani kuvuruga mataifa mengine.
Mbona unaweweseka? Unawashwa Nini taarifa yenyewe ya kawaida kabisa ushakimbilia kujihami..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,278
2,000
Doh mwaka uliopita nilijaza aiseee ndio tushatemwa hivo. Makosa ya wengine yanalicost Taifa zima. Kweli mchuma janga hula na wa kwao.

Sheria huanza kazi ikipitishwa kwenda mbele, hairudi nyumba. So, kama ulicheza mwaka jana haikuhusu ila ni rahisi kupigwa na radi kuliko mtanzania kushinda dv lottery.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom