Watanzania wazuiliwa kucheza bahati nasibu ya kupata ukazi wa kudumu (Green Card) Marekani

Ni nadra sana zaidi ya sana mtz kushinda dv lottery hivyo haina impact yoyote iwepo au lah ila wangeisitisha nchi kama Kenya nadhani jamaa wangeandamana kama sio kuuana kabisa.

Mkuu impact ipo, manake walikuwepo watu wanashinda hiyo kitu, yan ile tu kuwa denied from involvement ni problem aisee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
watu wanadhan pompeo ni kipilimba 🤣🤣🤣🤣🤣🤣, aisee me waliposema wanaushahidi ndio nimeogopa sana


Sent from my iPhone using JamiiForums

Ni kweli yule siyo Diwani wetu, matamko yao hasa wanapokuwa kule kwenye jumba la kinga wayaangalie sana. Ngoja tuone mwisho wa huu mziki nani ataomba poooo
 
ngoja tuone watumwa wa fikra wakishabikia ujambazi wa marekani,

Marekani ikisema demokrasia, ujue kuna taifa litaumizwa kwa vita na kuondolewa katika misingi yake.

Sote ni mashahidi wa namna kete ya Demokrasia ilivyotumika vyema na marekani kuvuruga mataifa mengine.
Acheni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani acheni unyama unyanyasaji kwa wapinzani
 
Unajua kwenye uhalifu wowote dhidi ya binadamu,lazima kuna mmoja atatekeleza amri huku dhamiri yake ikimsuta,na huenda ndio wanaopeleka ushahidi wakati mwingine hata wa video ya jinsi wanavyotekeleza uhalifu huo.Tecnolojia iko juu sana.

Marekani kusema ina ushahidi tena "wa kutosha!" Ni jambo linalofikirisha sana. Maana hawa jamaa hawanaga uongo uongo.

Ila najiuliza tena, iwapo wana ushahidi wa jinsi alivyodhulumu maisha ya watu, kwa nini wasifungue mashtaka the Hague?
Au hii ikoje maana isije ikawa sasa wameamua tu kumpakazia kutokana na maneno ya wanasiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asherymdudu, Muamerica ana ushahidi wa kutosha kwamba Makonda ameshiriki kudhulumu haki ya kuishi ya watu kadhaa" kumbe hawa wazungu wanajua yote ila walikaa kimya tu kuona kama wauaji watabadili tabia, halafu akitoa roho za watu ndio anazidi kunenepeana, yule atakuwa vampire!

Lissu ana bahati sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mwaka, Marekani inatoa makazi ya kudumu kwa watu 50,000 kupitia mchezo wa bahati nasibu. Mchezo huo, unachezwa kuanzia mwanzoni mwa mwezi Oktoba hadi Mwanzoni mwa mwezi Novemba. Leo hii, Serikali ya Marekani imetangaza kwamba waTanzania wote watazuiliwa kwenda Marekani kupitia bahati na sibu hiyo. Kuzuiwa huko kutaanza tarehe February 22. Kwa hio kama ulishinda mwaka jana, basi wahi ubalozini sasa hivi upate viza yako ya kukupatia makazi ya kudumu USA, kabla ya hio tarehe ambapo ndio waTZ watazuiliwa. Serikali ya Marekani haijasema sababu halisia ya kufanya hilo.

Pamoja na Tanzania, nchi ya Sudan nayo imezuiliwa viza hio ya bahati na sibu. Nchi 2 nyingine za Afrika za Eritrea na Nigeria zimepigwa nyundo kali Zaidi ambapo wamezuia aina zote za visa zinazomruhusu mtu kuishi na kufanya kazi Marekani.


IMG-20200131-WA0004.jpg
 
ngoja tuone watumwa wa fikra wakishabikia ujambazi wa marekani,

Marekani ikisema demokrasia, ujue kuna taifa litaumizwa kwa vita na kuondolewa katika misingi yake.

Sote ni mashahidi wa namna kete ya Demokrasia ilivyotumika vyema na marekani kuvuruga mataifa mengine.
Lakini na wewe utambue kuwa tatizo sio sisi raia, ni misimamo na sera za viongozi.
 
Ina maana ndoto yangu ya kuenda Marekan imefia hapo sasa, am looking forward to Canada
 
Sheria huanza kazi ikipitishwa kwenda mbele, hairudi nyumba. So, kama ulicheza mwaka jana haikuhusu ila ni rahisi kupigwa na radi kuliko mtanzania kushinda dv lottery.
😂😂😂😂😂 Hatari sana.
 
Kwanini wakenya wameachwa kwenye hili, hivi hili katazo haliwezi kubatilishwa tuwe kama zamani? Na ni hatua zipi za kufuata ili marekani watutoe kwenye list yao? Jiwe must do something.
 
Back
Top Bottom