Watanzania wazuiliwa kucheza bahati nasibu ya kupata ukazi wa kudumu (Green Card) Marekani

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa raia wa Tanzania wamepigwa marufuku kushiriki katika mchezo wa bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani.

Bahati nasibu hiyo hutoa visa kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.

Nchi ya Sudani pia imepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Kwa upande mwengine, raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani.

Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan.

Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa

BBC
 
Sababu ndio hii
Makonda
IMG_20200131_221454_845.jpeg
IMG_20200131_221618_821.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ngoja tuone watumwa wa fikra wakishabikia ujambazi wa marekani,

Marekani ikisema demokrasia, ujue kuna taifa litaumizwa kwa vita na kuondolewa katika misingi yake.

Sote ni mashahidi wa namna kete ya Demokrasia ilivyotumika vyema na marekani kuvuruga mataifa mengine.
 
Ha haaa .. kumbe ndio maana Makonda wamemshukia kwa kasi sana!

Naona hapo wamewekea alama za kunukuu kabisa kwamba Magufuli alipoingia tu madaraka mwaka 2015 kaendesha kampeni ya kukomesha "mtu yeyote kuingiliana kinyume na maumbile"
kwa kizungu "Carnal knowledge of any person against the order of nature"
 
ngoja tuone watumwa wa fikra wakishabikia ujambazi wa marekani,

Marekani ikisema demokrasia, ujue kuna taifa litaumizwa kwa vita na kuondolewa katika misingi yake.

Sote ni mashahidi wa namna kete ya Demokrasia ilivyotumika vyema na marekani kuvuruga mataifa mengine.
Kwani democracia ni nini mkuu, ebu tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom