Consigliere
Platinum Member
- Sep 9, 2010
- 12,690
- 26,567
Watanzania, tusiwe watu wa kushangilia kila kelele inayopigwa mbele yetu. Si kila anayepaza sauti anapigania mabadiliko. Wengine wanapiga kelele ili kuua kelele nyingine. Wengine ni kama mabuzi wa porini wanaolia ili simba asisikike.
Mbinu ya Kumtumia Polepole ni njia ya kuua mjadala ya kitaifa
Tuchukulie mfano wa Humphrey Polepole. Wengi wanaona ni kama ameamua kuwa upande wa wananchi, amejitokeza "kuikosoa" CCM kwa kutumia lugha kali, ya uchokozi na kejeli. Lakini mnapaswa kujiuliza: Why now? Kwa nini sasa hivi, wakati hoja kubwa zilikuwa juu ya uchaguzi, kesi ya Tundu Lissu, Katiba mpya, na uwajibikaji wa Mahakama?
Polepole si mwepesi. Anatumika kisiasa. Amepewa jukumu mahsusi, kutoa “content” mpya ya mjadala ili kuondoa watu kwenye hoja za msingi. Anafanya kazi ya delaying tactics yaani kuchelewesha mijadala halisi na kuingiza hoja zinazowavuta watu kwenye bubble za kelele zisizozaa tija. Kitaalam na kimkakati, hii huitwa shifting the narrative.
Watu walikuwa wanapanga movements zao, walikuwa na hasira ya kuanzisha mabadiliko, baada ya Polepole kujitokeza wamejik7ta wanajisemea huyu haongei bure, ana kyndi kubwa nyuma yake linakimuunga mkono, wamejikuta wanaahirisha movements zao na kusubiri hilo kundi kubwa lenye nguvu lijitokeze. Wanasubiri "uwepo wa nguvu" fulani ilhali nguvu yenyewe ipo kwao lakini hawajitambui. Hii ni mbinu ya kisiasa ya decoy, chambo kinachotumika kuhamisha mawazo yenu mbali na samaki mkubwa unayepaswa kumvua.
Ni aibu na Inasikitisha sana. Tuna watu kama Tundu Lissu, Mwabukusi, Heche, Mnyika, Jaji Warioba, Prof. Issa Shivji, Generali Ulimwengu, na wengine wengi sana waliotoa muda, maisha, akili na vipawa vyao kwa ajili ya kupambania taifa. Wamepambana wakitazamia kizazi hiki k8tathamini fikra za kina, na kugeuka na kuwa kizazi cha kupambanua na kujitolea kwa nchi. Lakini badala yake, watu hao wamekuwa kama wanaopigania kivuli cha mtu aliyechoka kutembea.
Sasa hivi Mbowe analaumiwa kutoka kila kona ya nchi. Kama kuna mtu wa kumlaumu Mbowe ni viongozi wenzake na baadhinya wanachama ambao already paid their price kwa kuuawa, k6filisiwa, kukamatwa, kufungwa, kutesa n.k, na si vinginevyo. Tuwaache akina Lissu, Lema na wengine wamlaumu sababu hawa wao pia wameyapitia aliyoyapitia. Mbowe ana haki ya kuchoka. Hata nyie mngekuwa Mbowe, ingewaumizeni kuona siku waliyotangaza maandamano akaishia kujitokeza na kukamatwa yeye, bint yake, viongozi wenzake na waandishi wa habari huku wananchi wakiwa wamej7f8cha wakichukua matukio kwa simu zao za takno.
Wananchi wengi wanasubiri mabadiliko pasipo wao kuweka misimamo wala j8tihada, akili na misimamo yao ni kama vile nguo iliyoanikwa kwenye kamba, ikisubiri upepo uiamulie upande wa kwenda. Au kama bendera kwenye ulingoni , haijui mwelekeo wake hadi upepo uje.
Wanyakyusa walijulikana kwa hekima na ushauri wa wazee wao, waliojua kwamba ukitaka kumaliza tatizo la kijiji, usikurupuke. Ukisikia ngoma imepigwa, usikimbie kucheza kabla hujajua aina ya ngoma hiyo. Huu ni mfano wa busara.
Jamii ya wawindaji ya Wahadzabe hawakimbilii porini kufuata ndege kisa wamesikia kelele za ndege tu. Wanajua kuna ndege wa onyo, wa ulaghai, na wa furaha. Wana akili ya kuchuja , na hilo ndilo tunalopaswa kuwa nalo sasa, kuchuja kila kelele inayoletwa kwenye mjadala wa taifa.
Wamang'ati wenyewe ni jamii ya wapiganaji, hawakubali kupigana kwa hasira bali kwa mkakati. Walijua ukitafuta ushindi kwa kelele, utapoteza nguvu kwa makelele badala ya mapambano.
Na ukiangalia kwa Waingereza, Wamarekani, na Wakanada, utakuta, wanajua tofauti kati ya noise na voice. Wanajua ni lini ni mjadala wa kusaidia taifa, na ni lini ni drama ya kupoteza muda.
Je, sisi Watanzania tumejifunza nini?
CCM hawana Hofu ya Kashfa, Wanahofu Kuondolewa Madarakani
Tusidanganyike, CCM si chama kinachojali kusema mabaya juu yao. Hayo matusi ya akina Polepole, hayo ni matusi waliojipangia wenyewe, wakampatie mmoja wa wenzao ambaye ni Polepole awatukane. Hawaogopi kuambiwa wako hovyo. Sababu ni simple, wapo hovyo kuliko hata matusi yanayowatamkwa na hilo wanalijua. Waite wauaji, waite wezi, waite wala rushwa waite wauaj8...na hata wakila rushwa, wakiua, wakiiba hayo hawajali.
Kitu pekee kinachowaumiza ni kuondolewa madarakani. Kwa hivyo, watatumia kila mbinu , ya kihuni, ya kitaalamu, ya kiintelijensia, ya kihistoria , kuhakikisha wanabak8 madarakani.
Mbinu wanazozitumia ni pamoja na kutumia media strategy kuhamisha mawazo ya watu.
Kuingiza mijadala ya ndani ya chama ili watu wasahau mijadala ya kitaifa.
Kutengeneza wahusika wa “uhalisia” wa kisiasa ili waonekane wako na wananchi, lakini kwa ndani ni watu wa kazi maalum.
Kuweka hoja bandia kwenye timeline za mtandao ili watu wapoteze “focus.”
CCM haikuwa ilipuuzwa, haikuwa ikijadilika, lakini Polepole amefanikiwa kuwarudisha watanzania katika kuihadili na kuifuatilia CCM.
Amefanikiwa kuikoa Serikali, Tume na Mahakama, wote mnaifuatilia na kujadili chaguzi za CCM, wote mmerudishwa kujiandaa na Uchaguzi, wote mnasubiri uchaguzi wa ndani ya CCM ufanyike, mshindi atabgazwe na huyo ndiye atakuwa Mbunge rasmi, labda na kujua vyama washirika wa CCM watagawiwa majimbo mangapi na yapi.
Ushauri wa Mwisho
Tumia Akili Yako Kama Filter, Siyo kama Sponji
Watanzania wenzangu, don't be a sponge. Usipokee kila tone la habari bila kuchuja. Ukitaka kujua umuhimu wa jambo, jiulize, hili jambo linasaidia vipi maisha ya Watanzania wa kawaida?
Ukitaka kufahamu kama mjadala ni wa kweli au wa kutengenezwa, jiulize: Kwa nini mjadala huu umeibuka sasa? Unavuruga nini kingine kilichokuwa mbele yetu?
Ukitaka kujua kama mabadiliko yanakuja, usisikilize sauti, tazama mwelekeo wa matendo.
Usikubali kuwekewa akili na wengine.
Mtu akikutengenezea akili, atakutengenezea pia maamuzi.
Usiwe sauti ya echo ya Humphrey au yeyote yule.
Kuwa sauti yako mwenyewe.
Watanzania, tuna deni la fikra.
Tulifilisika kwa matumaini, sasa tusifilisike kwa akili.
Think beyond the headlines. Fikiria kabla ya kushangilia.
Na tukumbuke, Mabadiliko si kelele , ni matendo na mikakati.