Watanzania ughaibuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania ughaibuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Darwin, Sep 27, 2010.

 1. D

  Darwin JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi nashindwa kuwaelewa hawa watanzania wenzangu waishio ughaibuni.
  Hawa wako kwenye mafungu.
  Watoto wa waliokua mabalozi wa Tz nchi za nje
  Watoto wa mafisadi.
  Watoto ambao kwa njia moja au nyingine hawakufika huko kwa njia ya uhalali.

  Swali lakujiuliza nikwanini hakuna tunachoona cha maana kama kuandaa chakula au kitu kama CHANGIA MAENDELEO YA TANZANIA au kuchangia maendeleo ya sehemu wanazotoka?

  Unayoona nikuwa na vikao vyakusifia CCM,kuanzisha matawi ya CCM ugenini, Kampeni za CCM ugenini, hivi utatembea na fulana yako iliyoandikwa chagua CCM marekani nani atakayepiga kura huko? au kuna kupiga kura nje ya nchi, As far I know hakuna kitu kama hicho kwa Tanzania.
  Najua wamarekani ndio wanaoweza kupiga kura wakiwa nje ya marekani. Jengine sherehe zisizokua na kichwa na miguu.
  White party sijui nyekundu party.

  Chakushangaa zaidi ni hawa watu wanaofaidika na maendeleo ya magharibi lakini wao ndio wa kwanza kushabikia CCM izidi kuwaumiza watanzania wenzao ambao hata maji masafi ya kunywa ni shida, hapo sijaongelea mlo.

  Wengine eti wanasifia maendeleo ya magharibi lakini unashindwa kuwaelewa kwanini mtu azidi kusifia cha watu wakati chako kinadorora?
  Utakuta mtu anasema nimejifungua kwenye first class hospital, what a heck? huu ni ushamba au ninini?

  Marafiki zangu huku ughaibuni ambao wameshawahi kufika Tanzania wanasema itachukua karne watanzania kujua haki zao na majukumu yao na sio kutegemea wazungu wanaokuja Tanzania kuwafundisha namna yakujiendeleza
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  To quote Darwin himself "What a heck ?"
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Darwin, si wote waliopo ughaibuni ni watoto wa mafisadi au watoto wa mabalozi wa zamani. Wapo wengi ughaibuni walioshindwa na maisha ya shida na kandamizi ya CCM na walipopata nafasi ya kutoka nje ya nchi ndo ikawa imetoka. Ninafikiri wengi waliopo ughaibuni hutoa mchango mkubwa sana kwa ndugu zao na watu wao wa karibu. Nilipokuwa ughaibuni miaka ya huko nyuma nilitoa kila aina ya msaada nilioweza kwa wazazi wangu, kaka zangu na dada zangu.

  Sikuona sababu ya mimi kuchangia shule au hospitali ya Tanzania ili hali akina Lowasa, Rostam Azizi, Chenge, Karamagi na wengine wengi wana mabilioni ya fedha ambazo wamewaibia wananchi na kuziweka nje ya nchi, na serikali haioni sababu ya kuwawajibisha ili hiyo hela ifanye kazi ya maendeleo. Yaani mimi niache babangu anavaa viraka niichangie shule ambayo fedha yake ya kujengea anayo Rostam Aziz na serikali haitaki kuichukua? Hiyo siyo fair kabisa. Na kuwalaumu waliopo ughaibuni katika hilo ni kutowatendea haki.
   
 4. D

  Darwin JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  @ Kiranga, HERI MIMI SIJASEMA, MBONA UNAWAKANYAGA WENGINE KAMA MAJANI? mpaka wote wakaisha kuuliwa.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  vipi kuhusu wale waliopata scholarship wakaenda ughaibuni jumla ingawa si watoto wa mabalozi wala mafisDI?
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Wenzetu walio nje wako kama sisi tulio huku. Kuna wanaojitahidi kusaidia nyumbani na kuna wasiojali.
  Miongoni mwetu hapa nyumbani kuna wanaothubutu kupambana na maovu yanayotukabili, lakini kuna wasiojali kabisa- hata kupiga kura hawaendi.
   
 7. k

  kommen Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Usiwashangae hao ulioainisha, utawapima kwa matendo yao, maana kama mwamko ni kwenye mambo ya kujigamba kama hizo party nk, basi bado wanahitaji kuelimika na hicho nadhani ni kigezo kimojawapo kinachoweza kuonyesha si migrants wote wana faida kwa home countries zao!!
   
 8. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Master Darwin! umekosea!! Sio wote tuliuo ugaibuni ni Mafisadi au watoto au jamaa wa wakubwa! wengine sisi ni watanzania wa kawaida toka familia masikini zinazoangaika usiku na mchana ktk maisha yetu haya ya kawaida kwa hiyo Mkuu sio wote kama unavyotufikiria! tcare!
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  @Darwin

  the only problem i see hapa ni wewe kuhukumu wote walio nje ya nchi bila kujua walifikaje huko majuu

  you might be grossly misinformed
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Watu wana frustration zao bora wazimalizie Jf where we dare talk openly. Ooops they said .... ..... khe khe khe kazi kweli kweli.
   
 11. D

  Darwin JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa kuwaomba samahani wale wote ambao walienda kihalali.
  Pili labda nibadilishe nakuandika WENGI WAO, kwani katika ya hao wachache waliokwenda kihalali mimi ni mmoja wao. Jirani zetu Kenya kuanzia nyumbani kwao wana mambo ya HARAMBEE. Mtanzania kijijini kwenu Mkata unajisifia eti unavaa viatu vya manolo. Huko Mkata watavitambua kwamba ni viatu vya bei ghali?
   
 12. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Darwin ninafuatilia postings zako sielewi unataka kusema nini, mbona unachanganya mada? wakenya wanatafuta nini hapa?

  Haya leta ujumbe unataka kusema nini? Tukusikie?
   
 13. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Next time wakikualika kwa chakula katikati ya sherehe omba kwamba unataka kutoa ushauri, nina imani watakusikiliza. Waambie jamani eeeeeeehe haya mambo yakualikana tuache. Au anza wewe andaa sherehe na uwaambie ni kwa ajili yakuchangia shule ya kule kijijini kwako, ukiona hawajachangia basi njoo useme hapa.

  Anzisha wewe, nina imani wengine watafuata!

  Positive thinker!

  NN
   
 14. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sijui hii ''shuntama'' ya CCM ita''éxpire'' lini! Ila hao unaowaona ni sehemu ndogo sana ya wa TZ waishio nje .
   
 15. M

  Mkora JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwanza hakuna asiyekwenda kihalali na kila mtu anaishi kwa mujibu wa sheria
  Maisha yenyewe mafupi ? Kama nchi imewashinda si bora muwarudishie waingereza kila kitu uongo tuu
  Waziri anakwambia uchumi umekuwa 8% wakati mshahara unaongezeka 70%
  Hatu ukichanga haisaidii zaidi ya kupunguza siku zako za kuishi tuu
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  ..
  Mkuu wangu mimi nadhani ungezungumzia kuhusu Watanzania waishio Tanzania badala ya hao wa nje kwa sababu hawana impact yoyote ktk uchaguzi kama unavyoitaka, hivyo ni hoja isiyokuwa na majibu mepesi. Lakini hao watoto wa viongozi waliopo Tanzania mkuu wangu ungeweka hoja zote hizi kuwalenga wao, ingetujenga zaidi kwani ndio wao wasiochangia lolote zaidi ya kutumia majina ya baba zao kujinadi mjini...Wakiitwa pia WAHESHIMIWA.

  Haya tazama jinsi wananchi wanavyovaa nguo za CCM, tazama kampeni zote za CCM utashindwa kuelewa hawa watu wanafaidika kipi na CCM kuvaa nguo hizo zaidi ya kushabikia chama kama vile ni timu ya mpira..Cha kushangaza ni kwamba wanashabikia CCM kwa kila hali wakati hawana hata maji ya kunywa wala ajira ya kuweka chakula mezani wakisha rudi nyumbani toka ktk mikutano hiyo..

  Halafu basi wanavyoyajua ya Marekani utadhani wanaishi huko wakimsifia Obama na maendeleo ya Marekani kama vile yanahusiana lolote na Tanzania. Na sidhani kama kumwagia sifa Obama kunawapa ruksa ya kupiga kura Marekani ama kumjua vizuri Obama na chama chake, ukweli ni kwamba hawajui kitu..Wao ndio kwanza kuanzisha sijui Valentine, Spoilforchoices, Haloween, White Party sijui red huku wakiazima suti na nguo toka drycleaner, haya yote makubwa ya nini ikiwa watu hamna uwezo?

  Ni mila ya Mtanzania kusifia cha mwenzake yaani utawasikia wezi wote nchini ndio wanaopewa sifa uwezo wa kimaisha. Rostam Aziz, Lowassa, Chenge, Mramba, Mkapa. Dewji, na mafisadi wengine wakubwa wakubwa wanaitwa Mipapa ndio wenye kusifika kwani mtu kama Dr.Slaa ambaye wazazi wake hawana nyumba ya fahari ndiye mbovu kati ya wabovu na hafai kuongoza nchi. Leo hii Lowassa, Chenge, Rostam, Mramba nasikia ati hawana upinzani, ni swala la wakati tuu kutangazwa kwao ushindi. Hii ni kweli akili jamani?

  Na hakika pasipo mtu kujifungua ktk hospital ya first class huwezi kuifahamu huduma bora ni kitu gani. Na kuhakikishia kwamba huduma anayopata mwananchi Moi pale Muhumbili ni sawa na zahanati ya Community health centre ya mtaani tu ktk nchi hizi za Ulaya, hivyo sidhani kama Mtaznania wa kawaida anaweza kujua nini hasa maana ya first class ktk nchi hizi za Ulaya. Labda nikwambie tu ya kwamba hiyo Moi ingekuwa nchi hizi ingefungiwa na kutopewa kibali cha kuendesha huduma za Afya kwa wananchi.. sasa hapo Pima mwenyewe.

  Mengine mkuu wangu ni mazungumzo tu baada ya habari lakini nachoweza kusema ni kwamba Watanzania waishio nje ndio kwa kipimo kikubwa wanapinga Utawala wa CCM kuliko Watanzania walioko nyumbani. Angalia hapa JF ni mfano mmoja pekee unaweza kukuonyesha jinsi vijana waishio nje wanavyopinga, lakini wengi tanzania wanashindwa kuwaelewa kabisa..

  Na pengine nikwambie tu kwamba wengi wamejiunga na CCM nadhani kwa sababu jumuiya za Kitanzania zimeshindwa kusimama huku majuu kutokana na Majungu na pengine kubwa zaidi UNAFIKI wetu..
  UNAFIKI ni moja ya tamaduni (culture) za Mtanzania.
   
 17. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona mnafanya upumbavu pumbavu wa kuchangisha feza huko. hamuoni ni ujinga watz wanalia na umasikini harafu ninyi ndiyo mnajifagilia eti tumechangiwa na waziri mkuu!!!!!!!, nawashangaa sana! badala ninyi mchangie tz kwa sababu mnapata japo kipato cha kueleweka ndiyo mnageuka ombaomba! Mrudi sasa kama maisha yamewashinda! mje muone makali ya umasikini na foleni ilivyo Dar!
   
 18. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Si unajua tena WaTZ kwa kujikomba hapo wanafukuzia u DC
   
 19. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Aaa,wasikuumize kichwa hao,wengine huko ughaibuni nanga zimeshapaa kitambo wanakosa hata nauli ya kurudi kwao,walichoambulia ni lugha za kigeni na mother fucker nyingiiiii,plus kupiga picha kwenye mali za watu.Kwakifupi wamekwama!!
   
 20. c

  chama JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hasira za maisha zitatufikisha wapi?Tuangalie zaidi maendeleo duni ya Tanzania yanatokana na nini? Je jibu la matatizo yetu yatatuliwa na misingi ya kisiasa iliyopo? Si rahisi kujua impact ya watu waliopo ughaibuni wanasaidiaje maendeleo ya Tanzania, nadhani familia ndiyo rahisi kujua aliyepo ughaibuni anasaidiaje ndugu zake. Ndugu yangu mchajikobe sidhani kama utapata nafasi ya kwenda ulaya ama America utaikataa, kama ulidunda visa jaribu tena !
   
Loading...