Watanzania tuwe makini sana na watu kama Dkt. Diallo. Ni watu wa maslahi zaidi

Alama zipi?umesikia huko kuwa lile somo la historia alilokuwa amelazimisha lianze kufundishwa madarasa yote kuanzia July, limetupiliwa mbali licha ya kuwa vitabu tayari vilishaandaliwa kabisa?kisa ni kuwa ni full propaganda za kumsifia tu yeye, hao marais wengine wamegusiwa kidogo tu!!hizo siasa za kishamba, ukatili, ndio legacy?kama ndio hivyo ki ukweli itachukua karne nyingi sana kumpata kiongozi wa aina hiyo, na bahati nzuri Dialo juzi ametupa angalizo zuri sana!!!MUNGU FUNDI
 
Wala rushwa ndivyo walivyo,paymaster alimwona dialo kama MTU anaye kubalika na kusikilizwa mwanza akampa mchongo amchafue magufuli naona hali ni tete uchaguzi ujao wamwandalie fungu la sivyo itakula.
 
Mambo mengine mnamuonea bure, yeye Kama Rais alitoa mwongozo kuwa somo la Historia ya nchi yetu lifundishwe kuanzia primary hadi chuo, ili watoto wetu wafahamu historia ya nchi yao.

Kazi ya utunzi wa vitabu vya historia ni kazi ya wataalamu wa somo husika, Kama wameboronga katika utunzi wao wa vitabu inakuwaje lawama zinaenda kwa JPM?!!

Alama alizoacha Magufuli ni nyingi katika nchi hii mfano:-
Ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, flyovers, Hospitali na vituo vya Afya, ujenzi wa meli mpya, upanuzi wa viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege mpya, Usambazaji maji toka ziwa Victoria, elimu bure, kuondoa wafanyakazi hewa, kupambana na ufisadi, nidhamu ya watumishi wa umma, udhibiti wa madini yetu na rasimali nyingine, kuongeza makusanyo ya kodi N.k.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Nasema hivi hoja si ukweli au uongo bali ni mambo ambayo mnapenda kuyasikia, na ndio maana imekuwa issue kubwa ya kufungua nyuzi kibao humu pamoja na kusema si jambo jipya.

Ww mwenyewe ndio nyuzi unazochangia, kwanini usifungue uzi wa kujadili vile viwanda vyake 8,000+, ili mliokuwa mnamsujudia mkutane huko mjadili?
 
Mambo mengine mnamuonea bure, yeye Kama Rais alitoa mwongozo kuwa somo la Historia ya nchi yetu lifundishwe kuanzia primary hadi chuo, ili watoto wetu wafahamu historia ya nchi yao...
Awamu ya tano kuna msomi hata mmoja alikuwa anaweza kutumia elimu yake inavyotakiwa kwa kufuata taaluma yake?!!awamu ya tano ni barabara zipi alizojenga hadi kumpa sifa hiyo?ufisadi upi huo?ni kitu gani cha kipee ambacho wengine hawakukifanya ?hayo mengine kila mtu alifanya kwa kiasi chake
 
Ww mwenyewe ndio nyuzi unazochangia, kwanini usifungue uzi wa kujadili vile viwanda vyake 8,000+, ili mliokuwa mnamsujudia mkutane huko mjadili?
Nishakwbia mimi nipo huru tofauti na nyie mnaochumkia au kumuabudu Magufuli, sina sababu ya kumchukia wala kumuabudu.
 
Nani angethubutu kuanzisha miradi mikubwa kama SGR na Bwawa la umeme la Rufiji?
JPM alithubutu kuanzisha ujenzi wa Bwawa la umeme la Stiglers gorge licha ya kelele nyingi za mabeberu kuhusu mazingira.


Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Sawa hayo alithubutu!!lakini mzigo aliouachia taifa hili kwa miradi hiyo hadi wajukuu wetu, watahangaika nao!!ingekuwa ni pesa yetu sawa, lakini kwa pesa ya kukopa tena kutoka kwenye taasisi za fedha/bank binafsi kwa miradi hiyo ambayo kuanza kurudisha fedha ni miaka mingi?

Na ndio itakayo mtesa sana SAMIA, unadhania kwanini mambo mengi yalisimama , huwezi ukawa kiongozi ukawa na vipaumbele vyako kwanza, ili kujijtengenezea sifa, huku vipaumbele vya taifa ukaachana navyo!!stahiki za wafanyakazi ikawa ni hisani sio haki!!unadania hata huo uamuzi wa kuhamia dodoma ulikuwa ni wa busara?MUNGU FUNDI
 
Uelewa wako wa mambo ni mdogo sana!

Kikwete aliondoka madarakani akiwa amekwisha kamilisha mipango yote ya ujenzi wa sgr kwa mkopo kutoka china. Kama Magufuli asingekurupuka kufuta huo mkataba leo hii sgr ingekuwa imeshafika kigoma na Mwanza.
 
Hiyo miradi ni nguzo muhimu katika uchumi, huwezi kuwa na viwanda vikubwa na huna reliable source ya umeme, Megawati 2100 zitakazozalishwa na 1500 za Sasa ni suluhisho tosha kwa changamoto ya umeme.

SGR ya umeme ni kichocheo kizuri Cha ukuaji wa uchumi, mizigo mingi itasafirishwa kwa gharama ndogo toka bandarini kwenda sehemu mbali mbali za nchi hadi nchi jirani. Hii itasaidia Sana kupunguza mfumuko wa bei na kurahisha movement ya bidhaa.

Magufuli aliona mbali Sana, hata Kama tunachukua mikopo kwa miradi itakayochochea ukuaji wa uchumi siyo tatizo tuna uhakika kuwa mikopo hiyo italipika bila tatizo lolote.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Uelewa wako wa mambo ni mdogo sana!

Kikwete aliondoka madarakani akiwa amekwisha kamilisha mipango yote ya ujenzi wa sgr kwa mkopo kutoka china. Kama Magufuli asingekurupuka kufuta huo mkataba leo hii sgr ingekuwa imeshafika kigoma na Mwanza.
Duh! Nadhani umesikia kuhusu SGR ya Kenya ambayo imejengwa na wachina, ni copyright na ile kikwete aliingia mkataba na wachina. Ile SGR ni ya kutumia diesel na gharama yake ni kubwa kuliko gharama ya SGR ya Magufuli. Wachina ni wajanja Sana, wanatoa mkopo kwa riba kubwa na ujenzi wanafanya wao.

JPM hakuweza kufuata mkataba wa wachina kwa sababu kwanza, SGR ilikuwa ni ya kutumia diesel badala ya umeme, pia gharama ya ujenzi ilikuwa kubwa mno ukilinganisha na SGR inayojengwa Sasa.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mizigo gani iliyokwama kufika popote nchini ikisubiria SGR.Sgr haiendi mikoa yote.
 
USILOLIJUA NI KWAMBA CCM WOTEEE NI WATU WA MASLAHI BINAFSI. WOTE BABA MMOJA NA MAMA MMOJA.
 
Kuna mizigo gani iliyokwama kufika popote nchini ikisubiria SGR.Sgr haiendi mikoa yote.
Aise!!! Kusafirisha mizigo kwa njia ya barabara kutumia Malori ni gharama maradufu ya kutumia SGR inayotumia umeme. Kwa kutumia SGR unasafirisha mizigo mingi kwa wakati mmoja, unatumia muda mfupi na uhakika kuhusu usalama wa mizigo. Gharama za mafuta ni kubwa na zinabadikika kila wakati ukilinganisha na gharama za umeme ambazo zitashuka baada ya ujenzi wa Bwawa la Rufiji.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…