Watanzania tuwe makini sana na watu kama Dkt. Diallo. Ni watu wa maslahi zaidi

Mama anaupiga mwingi sana 😂😂😂😂sasa hivi Diallo anaupiga mwingi. Uchaguzi ungekuwa unafanyika mwaka huu Diallo angeteuliwa na wapinzani uchwara kugombea kama rais.
Hakuna cha kuupiga mwingi. Haya ni matokeo ya alichokipanda Magufuli alizuia habari na kufungia na kuwatisha waandishi sababu akifanya ushezi usisikike kwa watu. Sasa aliyoyafanya yanamfuata nyuma na ndiyo asili ya jambo lolote unalolifanya Leo kesho litakufuata nyuma liwe jema au baya
 
Ni swala la muda tu magu ataoata na kupewa heshima anayo stahili hadi na upinzani
Mimi kwangu kashaota kabla ajafa toka siku ile alipotaka kumuuwa Lisu na Mungu kumkatalia lakini akashupaza shingo za kumuandama Lisu. Ndiyo siku aliota na kujulikana Ni mtu wa aina gani. Ana kigeni kwangu maana nilishajua ana nini moyoni mwake
 
Inawezekana kwa kuwa tuna ugomvi na chuki na Magufuli kila ambaye atakuja msema vibaya tutamwona ni shujaa. Lakini tujiulize "Dr. Diallo alikwii?"

Je Dr. Diallo kweli ana moral authority ya kumsema vibaya Magufuli? Huyu Diallo ukiangalia anacholalamika si kwamba watanzania wamefanyiwa hivi au vile. analalamika kwa kuwa kampuni zake zilitakiwa kulipa kodi ambayo zilikuwa hazilipi...
Hakuna mtu duniani asiyekuwa na maslahi. Hata wewe una maslahi. Cha muhimu ni kujiuliza je ujumbe wake ni wa kweli au la. Je lile file alilosema lipo kweli?
 
Mtu mchafu aache uchafu wake na kuenda kueleza uchafu wa mwenzie!! Ndio maana mimi nasema kinachowasumbua wengi ni chuki si kingine, yani mtu ambaye kama asingeguswa na Magufuli katika mambo yake binafsi basi asingeona au kuzungumzia ubaya wa Magufuli.

Alichokifanya ni kusema ukweli, suala la usafi wake ni mjadala mwingine boss.
 
Alichokifanya ni kusema ukweli, suala la usafi wake ni mjadala mwingine boss.
Alichokifanya sio kusema ukweli(sina ushahidi na alichokisema) bali kuonesha hasira zake kwa Magufuli kutokana mambo yake binafsi.
Hilo lazima liwekwe sawa, kama mambo yake binafsi yangeenda sawa basi asingekuwa na sababu ya kuja kueleza hayo.
 
Tatizo la wengi ni kwamba wana hasira zao binafsi kwa Meko kwa sababu zao binafsi.
Hilo ni sawa ukiwa kiongozi lazima tu watu kama hao, watakuwepo, lakini kwanini kwa kila mtu anayemsema MEKO, anachukuliwa hivyo hivyo kuwa alikuwa na chuki binafsi, ina maana hakuna watu kweli utawala wake uliwaonea?!!na ukiona kiongozi aliyekuwa madarakani baada ya kufariki tu ndio mabaya yake mengi yanasemwa, ujue kuwa alikuwa hapendi kusikia akikosolewa, na hilo liko wazi kwake.
 
Unaposema kuna mtu alikuwa na faili milembe unakuwa unalenga maslahi gani hasa?
 
Hilo ni sawa ukiwa kiongozi lazima tu watu kama hao, watakuwepo, lakini kwanini kwa kila mtu anayemsema MEKO, anachukuliwa hivyo hivyo kuwa alikuwa na chuki binafsi, ina maana hakuna watu kweli utawala wake uliwaonea?!!na ukiona kiongozi aliyekuwa madarakani baada ya kufariki tu ndio mabaya yake mengi yanasemwa, ujue kuwa alikuwa hapendi kusikia akikosolewa, na hilo liko wazi kwake.
Unajua mkuu hata JF nikikwambia unitajie watu wanaokosoa pale kwenye kosa na hupongeza pale palipostahili kupongezwa ni wachache utawapata, yani tuna makundi mawili tu kuponda au kusifia, kuna watu wao hawaoni mazuri kwa mtu wao huona mabaya tu na wengine wao hawaoni mabaya wao kutwa kusifia tu. Sasa hapo ndipo penye tatizo ndio maana zinaibuka hoja za kuonekana una chuki binafsi au una faidika kwa masilahi yako binafsi.
 
Inawezekana kwa kuwa tuna ugomvi na chuki na Magufuli kila ambaye atakuja msema vibaya tutamwona ni shujaa. Lakini tujiulize "Dr. Diallo alikwii?"

Je Dr. Diallo kweli ana moral authority ya kumsema vibaya Magufuli? Huyu Diallo ukiangalia anacholalamika si kwamba watanzania wamefanyiwa hivi au vile. analalamika kwa kuwa kampuni zake zilitakiwa kulipa kodi ambayo zilikuwa hazilipi.

Hiyo ndiyo chuki yake. Analalamika kwa kuwa alimpigia Kampeni Magufuli lakini hakuja pewa Upendeleo. Utaona ni mbinafsi mwanzo mwisho.

Lakini alikuwa wapi? "Alikwii?" Hawa wanafiki wasiwaaimbishe mapambio mapya kipindi hiki wakitengeneza mazingira ya kukumbukwa na rais aliyepo. Ni wanafiki tu hawa.

View attachment 1850089
Yote sawa khs Diallo, lkn pia yote yaliyosemwa na Diallo khs Mwendazake yako wazi na ni ukweli mtupu.
 
Unajua mkuu hata JF nikikwambia unitajie watu wanaokosoa pale kwenye kosa na hupongeza pale palipostahili kupongezwa ni wachache utawapata, yani tuna makundi mawili tu kuponda au kusifia, kuna watu wao hawaoni mazuri kwa mtu wao huona mabaya tu na wengine wao hawaoni mabaya wao kutwa kusifia tu. Sasa hapo ndipo penye tatizo ndio maana zinaibuka hoja za kuonekana una chuki binafsi au una faidika kwa masilahi yako binafsi.
na hili ndo tatizo kubwa lililopo kwa watanzania wengi kwa sasa hakunw wenye akili wengi wameshajitoa akili na kubaki na mihemko. MAGUFULI HAKUWA MUNGU. HAKUWA MTAKATIFU. ALIKUWA NA MEMA NA MABAYA YAKE. WATU wameamua KUSIFIA KILA KITU na wengine wameamua KUPONDA KILA KITU. huu ndo wendawazimu.
 
Inawezekana kwa kuwa tuna ugomvi na chuki na Magufuli kila ambaye atakuja msema vibaya tutamwona ni shujaa. Lakini tujiulize "Dr. Diallo alikwii?"....
He is the first suspect for accelerating the extermination substantially after coming out publicly in a televised interview undermining his previous party chairperson and the former United Republic of Tanzania.

Mwenye macho an masikio asikie huyo ni mtu wa aina gain an alitumikaje kufanikisha ajenda binafsi.
 
Team Msoga katika harakati zao za kujifaragua.... hawa wahuni wanakuja kwa kasi sana kwa sasa
 
Inawezekana kwa kuwa tuna ugomvi na chuki na Magufuli kila ambaye atakuja msema vibaya tutamwona ni shujaa. Lakini tujiulize "Dr. Diallo alikwii?"....
Kama tulishindwa kuwa makini Watanzania milioni 60 mpaka tunaongozwa na kichaa,sidhani kuna haja ya kuwa na umakini wowote kwa wasema ukweli kama Diallo.
 
Hakuna cha kuupiga mwingi. Haya ni matokeo ya alichokipanda Magufuli alizuia habari na kufungia na kuwatisha waandishi sababu akifanya ushezi usisikike kwa watu. Sasa aliyoyafanya yanamfuata nyuma na ndiyo asili ya jambo lolote unalolifanya Leo kesho litakufuata nyuma liwe jema au baya
MAMA ANAUPIGA MWINGI SANA....
 
Alichokifanya sio kusema ukweli(sina ushahidi na alichokisema) bali kuonesha hasira zake kwa Magufuli kutokana mambo yake binafsi.
Hilo lazima liwekwe sawa, kama mambo yake binafsi yangeenda sawa basi asingekuwa na sababu ya kuja kueleza hayo.

Ni kweli kilichomsukuma kuusema huo ukweli ni kwakuwa amekuwa muhanga wa madaraka ya Magufuli. Kwa haya hatuangalii kilichomsukuma kusema ukweli, bali tunaangalia ukweli wa alichosema. Kwa maneno marahisi, hatuangalii mtoa hoja, tunaangalia ukweli wa hoja yake.
 
Hapo sio issue ya ukweli wa hoja bali ni issue ya hoja yenye kuwapendeza bila kujali ukweli au uwongo wa hiyo hoja, alichoongea kimewapendeza kama si hivyo basi sasa mngekuwa mnamuangalia yeye badala alichokisema hata kama ni ukweli.

Mifano tunayo, tunaona Zitto kuna wakati akiongea mnachopenda kisikia huwa mnamsapoti ila asipoongea chenye kuwafurahisha ndio mnaanza kukumbushia usaliti wake na kusema haaminiki huyo ni msaliti tu, hata kwa Lipumba ni hivyo hivyo.

Kwenu nyie ukweli ni lile lenye kuwapendeza tu kinyume na hivyo ni upuuzi tu. Diallo angeongea ukweli kuhusu Mbowe au Lissu na likawa jambo lisilowafurahisha japo ni ukweli unadhani mgekubali huo ukweli? Jiulize mwenyewe katika nafsi yako.
 
Natoa rai kwa wana CCM wote tuisusie Sahara media ya Antony Dialo kwa sababu ya uasi wake.

Fisadi Dialo hapaswi kuchekewa na yeyote mpenda haki na asiye mnufaika wa magenge ya kihuni ndani ya CCM.

Kidumu chama cha mapinduzi.
 
Hapo sio issue ya ukweli wa hoja bali ni issue ya hoja yenye kuwapendeza bila kujali ukweli au uwongo wa hiyo hoja, alichoongea kimewapendeza kama si hivyo basi sasa mngekuwa mnamuangalia yeye badala alichokisema hata kama ni ukweli...
Narudia tena, alichosema Diallo ni ukweli, na ukweli huo huwa tunausema humu jukwaani mara Kibao. Alichokifanya huyo Diallo ni kwenda kinyume na wanaccm wengi kuficha ukweli unaokidhuru chama chao.

Hiyo mifano ya kina Zito na Lipumba subiri kwenye mada hizo ili tuuone huo ukweli, ama wapigie simu waseme ukweli ili uone tukiukataa. Na kwa kukusaidia tu, hata kama Diallo asingejitokeza hadharani na kuukiri huo ukweli, bado ukweli huo uko wazi.
 
Back
Top Bottom