Rais Samia usihangaike na maridhiano, hawa hawakutaki tu kwa sababu zao

Rais Samia usihangaike na maridhiano, hawa hawakutaki tu kwa sababu zao

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,665
Reaction score
17,139
Walikukataa hata kabla hujawa Rais. Hawakutaka uapishwe kuwa Rais baada ya kifo cha Rais Magufuli, hawakutaka ugombee nafasi ya urais, hawakutata uchaguzi ufanyike. hata baada ya uchaguzi hawakutaka uapishwe na hata baada ya kuapishwa hawataki uongoze nchi na nchi isitawalike.

Maridhiano nao hayana maana yoyote kwako na kwao, ni heri ufanye kile unachokiweza kuwahudumia wananchi. Kama ningekuwa mimi hata Katiba nisingeiandika kama wengine wakiwemo Mwl Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM walivyoacha kuiandika. Kilichowafanya wasiiandike upya usikipuuze hata kidogo.

Sio kwamba unatuongoza vibaya bali kwasababu zao wanazozificha nyuma ya demokrasia hawataki wewe uwe Rais wa nchi hii, ingawa sio wengi hivyo lakini wapo na wana mahusiano makubwa na wakoloni wetu, walikuja wote na wakaondoka wakawaacha, wapo na tunao.

Nadhani focus yako iwe kutumia kila senti yetu kwaajili ya watanzania, Katiba mpya haileti malisho kwa wafugaji wala mbegu kwa wakulima. Kwanza inatumia fedha nyingi sana kuiandika ambazo hatuna. Nafahamu wako watu ndani ya serikali wanakushauri uandike Katiba, changanya na zako. Kama ni rahisi hivyo Kwanini Mh. KIKWETE alishindwa kuiandika ikakamilika?. Sasa hivi lipo kundi kubwa sana la watanzania ambao wakati ule wa Tume ya Warioba walikuwa watoto, hivyo maoni yao hayakuwemo kwenye rasimu ile na sasa ni watu wazima ambao maoni yao pia lazima yajumuishwe kwenye Katiba ya 2030. HIVYO mchakato lazima uanze upya, na sio swala la kuanzia pale tulipoishia kama wanavyotaka wengine.

Usiyumbe na kuyumbishwa na kelele za ndani na nje za huyoo huyoo mchinje, mchinje, stay focused.

Hata huyu Lissu amejikuta tu ametumika baba wa watu. Nae ni mhanga wa wale ambao hawakutaka uwe Rais, Walimdanganya ili wamtumie kwa maslahi yao bahati mbaya amenasa tu hapo. Ndiyo maana wanahangaika mno ili atoke, they feel guilty. Muonee huruma hajui alilotenda. The actual bad people wako nje wanadunda.

Ni maoni yangu tu.
 
UMesema ukweli mabisa kuwa watanganyika zaidi ya99%hatumtaki kabisa.kwanza allijiteua kihuni pasipokufuata utaratibu wa chama.Tarehe nane mwezi wa nane tunakinukisha tena ili tumlazimishe ajiuzulu.katusababisha Tanganyika yetu kukimbiwa na uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha kuchakata mafuta cha dangote ambacho kimepelekwa kenya sababu sa100 hatakiwi na watanganyika kwa matendo yake maovu
 
Walikukataa hata kabla hujawa Rais. Hawakutaka uapishwe kuwa Rais baada ya kifo cha Rais Magufuli, hawakutaka ugombee nafasi ya urais, hawakuata uchaguzi ufanyike. hata baada ya uchaguzi hawakutaka uapishwe na hata baada ya ana wanahangaika mno ili atoke, they feel guilty. Muonee huruma hajui alilotenda. The actual bad people wako nje wanadunda.

Ni maoni yangu tu.
Sio hao tuu na hata wanaomzunguka baadhi,hawamwambii ukweli!
 
na Common Wealth pia hawamtaki kwa sababu zao?....basi ana Roho ya kukataliwa .Afanyiwe Deliverance
Jumuiya ya madola ndio nani kwetu? Kama wanaweza siwamalize vita yao ya Ukraine na Urusi? Wamalize vita ya Sudani, DRC na Iran watu wasife?
 
Walikukataa hata kabla hujawa Rais. Hawakutaka uapishwe kuwa Rais baada ya kifo cha Rais Magufuli, hawakutaka ugombee nafasi ya urais, hawakuata uchaguzi ufanyike. hata baada ya uchaguzi hawakutaka uapishwe na hata baada ya kuapishwa hawataki uongoze nchi na nchi itawalike.

Maridhiano nao haya maana yoyote kwako na kwao, ni heri ufanye kile unachokiweza kuwahudumia wananchi. Kama ningekuwa mimi hata Katiba nisingeiandika kama wengine wakiwemo Mwl Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na JPM walivyoacha kuiandika. Kilichowafanya wasiiandike upya usikipuuze hata kidogo.

Sio kwamba unatuongoza vibaya bali kwasababu zao wanazozificha nyuma ya demokrasia hawataki wewe uwe Rais wa nchi hii, ingawa sio wengi hivyo lakini wapo na wana mahusiano makubwa na wakoloni wetu, walikuja wote na wakaondoka wakawaacha, wapo na tunao.

Nadhani focus yako iwe kutumia kila senti yetu kwaajili ya watanzania, Katiba mpya haileti malisho kwa wafugaji wala mbegu kwa wakulima. Kwanza inatumia fedha nyingi sana kuiandika ambazo hatuna. Nafahamu wako watu ndani ya serikali wanakushauri uandike Katiba, changanya na zako. Kama ni rahisi hivyo Kwanini Mh. KIKWETE alishindwa kuiandika ikakamilika?.

Usiyumbe na kuyumbishwa na kelele za ndani na nje za huyoo huyoo mchinje, mchinje, stay focused.

Hata huyu Lissu amejikuta tu ametumika baba wa watu. Nae ni mhanga, Walimdanganya ili wamtumie kwa maslahi yao bahati mbaya amenasa tu hapo. Ndiyo maana wanahangaika mno ili atoke, they feel guilty. Muonee huruma hajui alilotenda. The actual bad people wako nje wanadunda.

Ni maoni yangu tu.
Ni aibu kwa taifa kuwa na mtu mwenye akili duni kama wewe.
 
Hata huyu Lissu amejikuta tu ametumika baba wa watu. Nae ni mhanga, Walimdanganya ili wamtumie kwa maslahi yao bahati mbaya amenasa tu hapo. Ndiyo maana wanahangaika mno ili atoke, they feel guilty. Muonee huruma hajui alilotenda. The actual bad people wako nje wanadunda.

Ni maoni yangu tu.
Na kama ilivyo kawaida kutoka kwako, ni maoni ya kipuuzi.
Andiko zima halina chochote cha maana kinachoelezwa.

Kama hawampendi, wewe unataka abaki kwa sababu zipi na kwa njia zipi?
 
nakubaliana na wewe kwa 100%, ndiyo, hatumtaki …
Mko wachache sana, hamsumbui serikali.

RAIS awe ngangali, Afrika hakuna demokrasia hiyo wanayoitaka wao. Hata chama kingine kikiwa madarakani watayafanya hayahaya waendelee kusalia madarakani. Kaza buti sawa na Kagame na Museveni. Borrow a leaf from Kagame and Museveni.
 
Sema mambo mengine kajitakia mwenyewe tu maana angesoma upepo tu
Mambo yapi hayo kaka? Rais Magufuli alikufa, katiba ikamtaka Makamu wake ndiyo awe Rais. Na makamu wake alikuwa Samia Suluhu, kosa lake ni lipi hadi hapo? Wakora walitaka kuipindisha Katiba ili Makamu asiwe Rais kwa sababu zao. HAKUNA HAJA YA MARIDHIANO HAPO. Maridhiano kuhusu nini? Yaani maridhiano na watu walioshindwa kukupindua, sijawahi kusikia kitu kama hiko duniani.

Ndani ya wasioitaka serikali yapo makundi 3 makubwa ya watu wasiompenda Samia tu watu wasioipenda CCM na watu wasiompenda Samia na CCM pamoja. Hapo unafanya maridhiano na kundi lipi?
 
Mko wachache sana, hamsumbui serikali.

RAIS awe ngangali, Afrika hakuna demokrasia hiyo wanayoitaka wao. Hata chama kingine kikiwa madarakani watayafanya hayahaya waendelee kusalia madarakani. Kaza buti sawa na Kagame na Museveni. Borrow a leaf from Kagame and Museveni.

unachanganya mambo, raisi wenu hata level ya afrika hamtoshi, hivyo hao madikteta wote uliowataja bado wana afadhali ya mara 10, thats how bad it is ...
 
Back
Top Bottom