Watanzania tuna matatizo mengi zaidi ya kebehi kwa Hayati Magufuli, Wanasiasa wanaotumia kichaka hichi Tuwakatae hadharani

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari JF,

Hivi mbona watanzania tunakuwa wajinga kiasi hiki? Maisha mtaani magumu ,ufisadi na Huduma bado duni za kijamii lakini bado mtu badala waje watusemee matatizo yetu, kila siku kumsema mtu ambae hayupo.

Kibaya zaidi huyo mtu hawezi jibu hizo tuhuma na hawezi shitakiwa na hakuna hata Mmoja Mwenye ushahidi ni kelele na tuhuma tu.

Nadhani imefika mahali mwanasiasi yoyote ataejificha kwenye kichaka hichi tumkatae kwa nguvu tena hadharani, tuna matatizo mengi kuliko huo mjadala wa MTU ambae hayupo.
 
Ni wajinga na wehu wenye mtindio wa ubongo achana nao. Muda ukifika majibu yatakuja kujulikana. Usidhani wale aliowafia mkononi wanafurahia, hii kitu iko pazuri sana tena sana.

Kumbuka waliomuu Sankara walishtakiwa na kufungwa. Kesi ya Tanzania ni rahisi sana. Maana kila aliyeshiriki keshajitambulisha waziwazi bila kificho. Kukosa hekima kwa wahusika au nadhani ni laana imewaumbua sana.
 
Maandamano ni haki yetu, Bora tuandamane kuuondoa huu uongozi uliopo
Hapana haja ya kuandamana. Maana yakotokea hayo maandamano kuna familia zitakimbilia burundi. Tushindane tu kwa hoja, haya mambo yatafika mwisho wake na amini nchi yetu ipo mikono salama kabisa na kila jambo lipo under control, hawa wapiga kelele very soon watapata majibu yao.
 
Ni wajinga na wehu wenye mtindio wa ubongo achana nao. Muda ukifika majibu yatakuja kujulikana. Usishani wale aliowafia mkononi wanafurahia, hii kitu iko pazuri sana tena sana. Kumbuka waliomuu Sankara walishtakiwa na kufungwa. Kesi ya Tanzania ni rahisi sana. Maana kila aliyeshiriki keshajitambulisha waziwazi bila kificho. Kukosa hekima kwa wahusika au nadhani ni laana imewaumbua sana.
Uko sahihi
 
Wewe hofu au shida yako ni nini "maliyemu" akisimangwa? Huwezi jua. Labda wakimsimanga wanapata afua ya maisha na kuongeza siku za kuishi. Kwani marehemu amelalamika? Kwa nini umsemee?
 
Kila siku mnaanzisha mada ya huyu Jiwe wenyewe mkielezwa mnakuwa wakali kama mbogo, unampa utukufu mtu asiye staili ndiyo maana mnateseka.

Kweli hali ni ngumu lakini haiondoi kusema huyu bwana alikuwa muovu kwa kiwango kikubwa sana.
 
Hakika nchi yetu imegubikwa na ujinga na upuuzi mwingi sana na kinachouma zaidi wananchi tupo kama mazombi, tunapelekwa tu.

Embu angalia nchi haina umeme, maji shida, hali ya maisha ni ngumu kwenye maofisi ya serikali ukiritimba umejaa alafu kuna wapumbavu wananyanyua midomo yao na kumkashifu marehemu....!!

Nchi ina wapuuzi wengi sana hii, Mungu pekee ndio wakutusaidia!!
 
Hakika nchi yetu imegubikwa na ujinga na upuuzi mwingi sana na kinachouma zaidi wananchi tupo kama mazombi, tunapelekwa tu.

Embu angalia nchi haina umeme, maji shida, hali ya maisha ni ngumu kwenye maofisi ya serikali ukiritimba umejaa alafu kuna wapumbavu wananyanyua midomo yao na kumkashifu marehemu....!!

Nchi ina wapuuzi wengi sana hii, Mungu pekee ndio wakutusaidia!!
Nchi imekuwa na ujinga mwingi
 
Wanasiasa waache kumuongelea marehemu, bali watatue shida zinazowakabili wananchi, kama marehemu alifanya mabaya, basi wafanye mema kwa vitendo tuyaone kwa macho, sio maneno tu tuone barabara za lami mitaani zaidi ya zile za marehemu,tuone madaraja,vyakula vishuke bei, umeme, maji vipatine wakati wote, petrol ishuke bei nk.
 
Back
Top Bottom