Hayati Magufuli alituonesha kazi ya Urais si nyepesi na si kila mtu anaweza kuwa Rais

Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
5,295
6,342
Nikumbukumbu ya siku mbaya sana hii kwenye maisha yangu na kwa waTanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao na sitaisahau.

Mtanzania yoyote mwenye akili na mzalendo anaelewa maumivu ya kumpoteza shujaa Magufuli jinsi yalivyo kuwa tarehe 17 march.

Nilipata faraja sana kuona Nchi yangu inapata dira ya mwelekeo wa taifa letu kimaendeleo. Nilikuwa na amani ya moyo kuona tuna mtu mwenye maamuzi ya mwisho ambae kwamaneno yake na vitendo vyake, angalau unaweza kuona mipango ya maendeleo ya nchi inavyo pangwa na kusimamiwa kikamilifu.

Sifa za kiongozi mkuu wa nchi ni kupokea taarifa kwa watendajiwake na kwaakilizake mwenyewe awe na uwezo wa kuchunguza na kugundua uzuri na ubaya wa kila taarifa anzopewa.

Awe na uwezo wa kwenda site na kugundua matatizo yanayo sababishwa na watendaji wake ama mazingira ya kazi.

Pia awe na uwezo wa kusikiliza wananchi live na kutatua kerozao hapohapo. Na asiwemuoga muoga kwa watu anao waongoza hatakama walikuwa viongozi zamani.

Magufuli alikuwa na sifa hizo. Wabongo tunahitaji kiongozi wa aina ya Magufuli ama hata zaidi yake. Viongozi waoga wanao waogopa wezi na mafisadi ndio wanao turudisha nyuma kimaendeleo na kutufanya tuwe ombaomba kila mwaka.

Mungu akupe pumziko la milele hayati Rais, John Pombe Joseph Magufuli.
 
Wote tunahitaji kubadilika na kuwa na nchi inayoweza kufuata sheria.
Aliyaongelea mengi sana kwa mda wake lakini je tumebadilika?

Wakati anampa Uwaziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, alikuwa na kijikaratasi akiwa ameorodhesha madudu kibao ya Mambo ya Ndani

Ameongelea mengi sana ukimsikiliza na Mambo ya Ndani inabeba mengi kuhusu nchi yetu maana ndio Usalama wote uko huko

Je kuna hata moja limefuatwa?
Sio kuwa tunataka mtu kama magufuli hapana bali wote tubadilike

Ajali bado zinauwa na wakuu wa polisi bado wapo tu na kazi zao ni kutangaza vifo tu utafikiri wamekuwa Hospitali
 
Mimi nachojua mtaani tunampenda sana,kelele za huku mtandaoni hazinisumbui.
Humu mtandaoni wengi wanamkubali kiaina ila wanajitoa akilitu.
Kumtukana Magufuli inabidi uwe fyatu kidogo kwasababu hakuwa na baya kwa watuwema wachapa kazi na waaminifu.
 
Back
Top Bottom