Watanzania matatizo yenu hayatamalizwa na Hayati Magufuli. Hatujadili tena mstakabili wa nchi yetu!

Trable

JF-Expert Member
Jan 3, 2023
1,783
3,281
Daah!

Sasa nashindwa namna ya kuelezea jinsi isivyo kawaida kwa aliyekuwa Raisi wa nchi yetu Tanzania hayati John Pombe Magufuli!

Huyu alikuwa ni kiongozi wa aina gani?

Ni miaka miwili sasa hatuna naye, lakini bado hajatoka mioyoni na midomoni mwetu, tena kila uchwao jina lake linakuwa linavutia zaidi kuwa maarufu zaidi mitandaoni na hata kwenye vijiwe vyetu kwa mijadala iwe kwa mabaya ama kwa mazuri, utadhani yupo hai bado!

Naona ni kama tumekwama na hatufanyi tena mijadala kuhusu ustawi wa nchi yetu, badala yake ni jina tunabishana kama wendawazimu kuhusu jina lake! Je, zile chanjo hazijaleta shida?

Tuna matatizo mengi kiasi cha kuzidi hata wakati wa yeye akiwa Raisi, lakini ni kama hatuoni shida hizo! kuna anguko la kifedha duniani na migogoro ya kifedha itayosababisha mgogoro mkubwa kwa nchi zenye madeni na kuanguka kwa uchumi Nani atusaidie?

Tuna matatizo ya chakula, mvua kutokunyesha kwa wakati, umeme kukatikatika na kama si kukosekana kabisa, tuna wafanya biashara wengi wameanguka kibiashara shida ikiwa ni TRA

Tunamadeni kama nchi na mengine yameiva na hatuna uwezo wa kuyalipa mpaka tukakope tena ndo tuyalipe!

Huduma mbovu kwenye sector za kiserikali, tunawatoto wako shule miaka saba lakini hawajui hata kuandika majina yao na wengine wako secondary lakini hawajui chochote

Tunaupungufu wa walimu, madaktari, manesi n.k

Kama nchi tutakabiliana vipi na njaa inayotokana na ukosefu wa mvua kwa mwaka huu, mifugo yetu itaishije kwenye ukame ujao, watu wetu vipi,

Badala ya kuongelea mambo ya mhimu, wasomi wetu ndio wanaongoza mijadala isiyo na tija

Sifahamu, labda ndio sehemu ya wao kufichia udhaifu wao?

Ni lini tutaacha mijadara ya kipuuzi na kuanza kudili na mambo mhimu ya maendeleo kwa nchi yetu?

Si wapinzani wala chama tawala! Wote tunakutanishwa hapa kumwongelea mtu asiyekuwa nasi!

Nchi za watu weusi iko siri iliyojificha ndani yetu ambapo kuijua kwake, ni hadi wazungu wahame kwenye hii sayari!
 
Tunapaswa kuendeleza misingi mizuri aliyotuwekea JPM kama tunataka kujikwamua kutoka hapa.

Tuendeleze uchapakazi, upingaji wa rushwa kwa vitendo, kuongeza nidhamu na uwajibikaji, kujenga miundombinu bora.

Tuachane na safari zisizokuwa na tija, mikopo, na kubembelezana.

Kwa kifupi tunapaswa kuwa na uongozi imara kama wa JPM kama tunataka kujikwamua kutoka kwenye mkwamo huu tulionao kama taifa.

Hatutaendelea kwa ku-copy na ku-paste kwa wazungu. Changamoto zao hazilingani na zetu, uwezo wao haulingani na wetu, na zaidi; mazingira yao hayafanani na yetu.
 
Magufuli ameharibu nchi hii tutanahitaji Ten yrs of maintenance chini ya Rais muislamu Kama Mama samiah
Umeanza kuwa mweupe kichwani!

Watanzania hatujivunii dini zetu bali utanzania wetu!

Ni utanzania tu utakofuta ujinga ujinga wa udini kichwani!

Aliyeko madarakani hawakilishi dini bali anawakilisha Watanzania!

Wewe ni Dr gani mweupe hivi mbichwa? DR HAYA LAND
 
Tunapaswa kuendeleza misingi mizuri aliyotuwekea JPM kama tunataka kujikwamua kutoka hapa.

Tuendeleze uchapakazi, upingaji wa rushwa kwa vitendo, kuongeza nidhamu na uwajibikaji, kujenga miundombinu bora...
Hapa kazi tu
 
Umeanza kuwa mweupe kichwani!

Watanzania hatujivunii dini zetu bali utanzania wetu!

Ni utanzania tu utakofuta ujinga ujinga wa udini kichwani!

Aliyeko madarakani hawakilishi dini bali anawakilisha Watanzania!

Wewe ni Dr gani mweupe hivi mbichwa? DR HAYA LAND

Nchi imeharibiwa na Magufuli kila kitu kaharibu
Ajira kaua
Wawekezaji kaua
Biashara kaua
Kilimo kaua

Sasa what the next be humble we need at-least ten years of Economic reviving.
 
Nchi imeharibiwa na Magufuli kila kitu kaharibu
Ajira kaua
Wawekezaji kaua
Biashara kaua
Kilimo kaua

Sasa what the next be humble we need at-least ten years of Economic reviving.
Ni miaka miwili sasa hayupo!
Lakini ukumbuke pia! Huyo mpaka anaondoka, nchi haikuwa na shida ya umeme kama ilivyo leo,

Nchi iliingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati tofauti kabisa na leo!

Aliondoka huku akiacha nidhamu kubwa kwa watumishi wa umma, leo kiko wapi!
Tuchukueni mazuri yake mabaya tuyatupe kule ingawa nayo ni ya kutafuuuta saana yani
 
Nchi imeharibiwa na Magufuli kila kitu kaharibu
Ajira kaua
Wawekezaji kaua
Biashara kaua
Kilimo kaua

Sasa what the next be humble we need at-least ten years of Economic reviving.
Sawa, tu-assume Magufuli ameharibu kila kitu. Tuna miaka miwili sasa tangu atutoke; je, ni kitu gani tangible mmekifanya, kuelekea hiyo miaka kumi ya kuamsha uchumi, kama hata kulipa tu madeni mnashindwa hadi mkope kwanza? 🤣
 
Ni miaka miwili sasa hayupo!
Lakini ukumbuke pia! Huyo mpaka ataondoka, nchi haikuwa na shida ya umeme kama ilivyo leo,

Nchi iliingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati tofauti kabisa na leo!

Aliondoka huku akiacha nidhamu kubwa kwa wafanya kazi wa serikali, leo kiko wapi!
Tuchukueni mazuri yake mabaya tuyatupe kule
Huyo alikuwa anafanya propaganda huwezi kujenga uchumi imara kwa kuua watu na kuteka hakuna kitu kama hicho
 
As I told you we need ten years of Economic reviving

Kufufua uchumi sio Kazi nyepesi Kama kuharibu Magufuli within his six yrs kaharibu Sehemu kubwa Sana kaua kila kitu kakata miti million mbili Hadi mvua hakuna
Ajira kaua
Biashara kaua
Wawekezaji kafukuza
Redundancy kaleta yeye vijana wengi wanapitia redundancy yeye ndo chanzo
Sawa, tu-assume Magufuli ameharibu kila kitu. Tuna miaka miwili sasa tangu atutoke; je, ni kitu gani tangible mmekifanya, kuelekea hiyo miaka kumi ya kuamsha uchumi, kama hata kulipa tu madeni mnashindwa hadi mkope kwanza? 🤣
 
Magufuli ameharibu nchi hii tutanahitaji Ten yrs of maintenance chini ya Rais muislamu Kama Mama samiah
Ten yrs kufanya nini ?
Wenzetu siku mia zinaanza kutoa matokeo wewe unawaza teni yrs na ndo maana tunaitwa vibaya na Trump.

Mwezi mmoja ulimuomdoa waziri uingereza sisi tunasubili ten yrs, naogipa tusi kwako ila tubadilishe akili ili tujue sisi tuna thamani kwenye hii nchi kuliko hao watawala.
 
Nilidhani hoja yangu itakufanya uache huu ujinga wa kujadili yasiyosaidia nchi na badala yake bado unaongeza mashambulizi

Vipi ulichanja?
Kama una Akili kichwani huwezi kulalamika kuhusu Hali ya Maisha nchi imeharibiwa Miaka sita mfululizo tunahitaji miaka 10-15 ili kurudi nchi ya Asali na maziwa

Kuhusu Umeme kukata ni yeye Magufuli kakata miti mil2 so read between the lines
 
Ten yrs kufanya nini ?
Wenzetu siku mia zinaanza kutoa matokeo wewe unawaza teni yrs na ndo maana tunaitwa vibaya na Trump.

Mwezi mmoja ulimuomdoa waziri uingereza sisi tunasubili ten yrs, naogipa tusi kwako ila tubadilishe akili ili tujue sisi tuna thamani kwenye hii nchi kuliko hao watawala.
DR HAYA LAND anauelewa mdogo sana, msamehe mkuu
 
Kama una Akili kichwani huwezi kulalamika kuhusu Hali ya Maisha nchi imeharibiwa Miaka sita mfululizo tunahitaji miaka 10-15 ili kurudi nchi ya Asali na maziwa

Kuhusu Umeme kukata ni yeye Magufuli kakata miti mil2 so read between the lines
Lete ushahidi!

Huu ni upuuzi tu ulioandika hapa!
 
Ten yrs kufanya nini ?
Wenzetu siku mia zinaanza kutoa matokeo wewe unawaza teni yrs na ndo maana tunaitwa vibaya na Trump.

Mwezi mmoja ulimuomdoa waziri uingereza sisi tunasubili ten yrs, naogipa tusi kwako ila tubadilishe akili ili tujue sisi tuna thamani kwenye hii nchi kuliko hao watawala.
This is Africa shithole country kuharibu it just simple kuliko ku-rebuild Magufuli ndo hayupo na kaacha Matatizo katika nchi yetu
 
As I told you we need ten years of Economic reviving

Kufufua uchumi sio Kazi nyepesi Kama kuharibu Magufuli within his six yrs kaharibu Sehemu kubwa Sana kaua kila kitu kakata miti million mbili Hadi mvua hakuna
Ajira kaua
Biashara kaua
Wawekezaji kafukuza
Redundancy kaleta yeye vijana wengi wanapitia redundancy yeye ndo chanzo
Ten good years start with a single beautiful day. It has been two years already. Tell us, in a nutshell; what have you guys done to lay a foundation for full economic revival at the end of the next eight years?
 
Lete ushahidi!

Huu ni upuuzi tu ulioandika hapa!

Hiyo miradi uchwara bila kutumia Akili anakata miti mil200 na nchi inakosa mvua mabwawa yanakauka umeme unakatika kuchagua watu wapumbavu wenye low IQ lazima tusote mtu mjinga Kama Magufuli alikuwa hatumii Akili katika maamuzi alikuwa anatafuta umaarufu wa kijinga ndo maana sisi watu wenye Akili tuliwaambia huyu mjinga Hana mwendo ataingiza nchi katika Matatizo ya kiuchumi .
 
Huwa huelewi ukiulizwa? Lete ushahidi ndio huu wa kulalamika?
 
Back
Top Bottom