Watanzania tulioko Switzerland

Watanzania tulioko Switzerland

Ingekuwa vizuri ungeweka wazi fursa zilizopo especially kwenye elimu ambazo Mtz awe za apply . Mfano aina ya masters, Ph.D. Scholarships n.k n.k
 
Fanyeni kazi nyinyi
tapatalk_1589200855995.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp kama mtu anataka kuanzia huko bachelor ya science kama vile ya nursing ama ya maabara kwa kujisomesha mwenyewe vp inawezekana ?
 
CHF2500 ni sawa na bei gani ya Tanzania?
naomba nikujibu kwa niaba.
njia itakayokufaa ni ya kutumia masomo kwa kazi itakuwa ngumu na hiyo masters yako ya vyuo vya huko nyumbani, hawa jamaa huku hawaitilii maanani elimu inayozalishwa na baadhi ya nchi za afica na hutaweza kushindana na watu toka bara la ulaya, America na asia kwenye soko la ajira la kimataifa, hii itakuwia vigumu mno na utayaona maisha ya hapa kama jehenamu, lakini ukija kwa njia ya masomo utatakiwa usome baadhi ya kozi ili kuboost elimu yako atleast uweze kutambuliwa kwenye mifumo ya ajira na utakuwa unafanya part-time job kipindi uko masomoni na kuyasoma mazingira vizuri ya nchi kabla ya kujichanganya, hii njia itakuwa nzuri na itakusaidia sana

Kwa PHD kama utapata scholarship itakuwa ni jambo jema na kama utaweza kujigharamia pia ni vizuri, nina rafiki zangu wawili wanasoma PHD tuko nao huku Switzerland mmoja raia wa Nigeria anasoma chuo cha Geneva Bussiness School hapa mjini Geneva na chuo kinamlipa CHF 30,000 kwa mwaka,na atatumia miaka 4 tu kumaliza PhD yake, mwingine ni raia wa rwanda anasoma ETH Zurich Institute of science, Technology and policy PHD pia yeye analipwa CHF 35,000+ kwa mwaka

Ada za PHD kwa huku zinaanzia CHF2500 na kuendelea kutokana na chuo husika na kwa elimu ya PHD na mifumo ya elimu ya vyuo vya hapa itakuchukua miaka 4 mpaka 7 kumaliza na tambua Switzerland ni moja ya nchi ya ulaya wanayotoa elimu bora kabisa ulimwenguni na vyuo vyake ni vya hadhi ya juu kimataifa na hutojuta kusoma huku, Karibu mkuu tuwe pamoja huku lakini tambua maisha ya hapa ni ghali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp kama mtu anataka kuanzia huko bachelor ya science kama vile ya nursing ama ya maabara kwa kujisomesha mwenyewe vp inawezekana ?
inawezekana mkuu ila uwe umejiandaa kimpunga
 
inawezekana mkuu ila uwe umejiandaa kimpunga
Sawa nimekuelewa mkuu nikuombe kama inawezekana kupata taarifa za awali kujua ni bei gan ya ada kwa mwaka hasa bachelor ya nursing na michango mingne ya awali ama ikiwa unaweza kujua ni chuo kipi kinatoa coz hiyo itakiwa poa sana. Jaribu kuuliza tafadhari mkuu.
 
Back
Top Bottom