Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Watanzania, Kuukimbia ukweli hakutatusaidia

Viongozi gani walihudhuria mazishi ya Nkurunzinza? May be hofu ya Corona ndiyo sababu.

Kenya nilisikia walituma sijui gavana wa kaunti gani sijui ndege yao ikageuzia angani
 
Huelewi kuna lockdown katika nchi nyingi?

Ulipaona hapa mkuu:

"Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi."

Ukizingatia sisi Corona hakuna.

Mengine ni kujidanganya na kujilisha upepo tu ambako hakutatusaidia.
 
Viongozi gani walihudhuria mazishi ya Nkurunzinza? May be hofu ya Corona ndiyo sababu.

Kenya nilisikia walituma sijui gavana wa kaunti gani sijui ndege yao ikageuzia angani

Kwani ni kwenye msiba huo tu? Pia umesahau kuwa sisi Corona haipo. Wataogopa vipi kuja kusiko na Corona hata kama kwao ipo?

Kwenye Kuukimbia ukweli, mambo iko huku:

"Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi."

Hakutatusaidia.
 
Muhimu mtu azikwe sio nani kafika , kuchukiwa ni changamoto nzuri inakupa nguvu , acha mawazo mgando
 
Muhimu mtu azikwe sio nani kafika , kuchukiwa ni changamoto nzuri inakupa nguvu , acha mawazo mgando

Mhhh! Muhimu kuzikwa tu?

Kuchukiwa na wote ni changamoto nzuri? Mfano ya achukiwaye na wote ni shetani peke yake.

Gandua mawazo yako. Acha kujidanganya.
 
Umeandika mavi matupu,uchafu mtupu,unachokitaka hautakipata,muda si mrefu threads zako za corona watu watazijua kuwa huna content wala points bali maneno yasiyo na maana tu;

niliwahi kuuliza unataka nchi hii ifanye nini kuhusu corona ukasema taarifa ziwepo,nikauliza tena taarifa zitakusaidia nini zaidi ya kuwa mwoga na kujificha hukujibu jibu la maana tofauti na porojo;

usipende kuiga anachofanya mtu,hao waliofata taratibu na kutoa taarifa za ugonjwa wamefanikiwa katika nini na sisi sema mafanikio yetu;

yaani umeshindwa kuona hata kama hatutoi taarifa utakazo bado hatuna vifo kama wao?,hilo huoni?,

kwanini husemi upande chanya unaangalia hasi tu tena yale ya wewe kuwaza mwenyewe hali hakuna ukweli wowote?,

toka uanzishe hizi threads za corona nini kimetuzidi watanzania hadi kusema sasa tulikosea?,

kwanini unajaribu kuaminisha ummakuwa hatuko salama?,

ndugu,acha unafiki,haufaidiki kwa lolote,simama na ukweli;

acha siasa za kijinga;
 
ukitaka kujua korona ipo na nchi iko pabaya,soma threads za jamaa;
jitahidi kuwa na mawazo chanya,hasi ukiiwaza hakika itakujia muda si mrefu ;
 
Kwamba kujikombakomba kwa mataifa mengine ndiko kutatuweka pazuri!?

Hii nchi ni huru na ina misimamo yake tangu zamani. Tumeonyesha upendo kwa mataifa mengine pengine kuliko nchi yoyote.
Tumeshiriki ukombozi wa nchi zao dhidi ya ukoloni, tumewahifadhi wapigania uhuru wao hapa kwetu, tumesaidia kulinda amani, tumewapa misaada ya vyakula, kijeshi n.K, tumehani na kushiriki misiba ya viongozi wao kwa heshima kubwa.

KAma yote hayo hawayaoni na mnaendelea kutaka tuwanyenyekee basi tambueni ya kuwa IMETOSHA.

Ni wakati sasa wa Tz kujali mambo yake na maslahi ya watu wake baaaas.
 
Muwe wazalendo basi. Au mmetumwa na mabeberu? Hii ni vita ya kiuchumi. Bro Magu chapa kazi. Usisikilize kelele za chura. Hongera sana kwa kulijengea taifa heshima
Naamini hii umeandika kejeri,Ile budget ya 33t akikusanya hata nusu yake kweli atakuwa jembe.
 
Mhhh! Muhimu kuzikwa tu?

Kuchukiwa na wote ni changamoto nzuri? Mfano ya achukiwaye na wote ni shetani peke yake.

Gandua mawazo yako. Acha kujidanganya.
Ndio muhimi ni kustiri mwili wa Mtanzania mwenzetu hao wengine waje au wasije hakuna umuhimu wowote , halafu Nani kakwambia shetani anachukiwa na wote ? ndio maana nikakwambia acha mawazo mgando kijana
 
Mkuu asante kwa bandiko lako,limenifikirisha !! Swali lanngu ni kuwa km tulishirikiana nao wakati walipopotwa na shida kwa nini sisi wametuachia msiba! Ingekuwa hatukushirikiana nao ningeelewa,mf mkapa alihudhuria misiba ya viongozi mbalimbali,kwa nini wao nao wasije hata kwa heshima ya mkapa?
Au tunachukiwa na nchi zote!? Kwani tumewakosea nini?au tunatakiwa tufanye nini? Na hao burundi wao wanatupendea nini? Na je nchi zingine zinaichukuliaje burundi? QUOTE="brazaj, post: 36217652, member: 377684"]
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada.

Siyo siri tena zama zimebadilika na matukio yanakwenda kwa kasi sana. Taifa letu likipita katika kipindi kigumu ambapo kwa bahati mbaya kumezuka hata makundi katika jamii ambayo yamelenga kupiga makelele tu yakijaribu kulazimisha kuufanya uongo kuonekana kuwa ukweli au ukweli kuwa uongo. Mithili ya kujidanganya mchana kuwa ni usiku au usiku kuwa ni mchana.

Mifano iko mingi mno na katika nyanja nyingi.

Ikumbukwe kuwa ukweli ni ukweli na uongo ni uongo na utabakia kuwa hivyo bila ya kujali nani kasema nini au nani atasema nini.

Ukweli mchungu hulka mpya hii haikuwahi kushuhudiwa katika awamu yoyote ya uongozi kabla ya awamu ya hii.

Hivi karibuni tumeondokewa na mzee wetu rais mstaafu mzee Mkapa (rip). Pamoja na sisi kushiriki sana katika shughuli zote za wenzetu, ni Burundi peke yake ndiyo walioweza kutuma ujumbe wao rasmi kuja kutuhani kwenye msiba huu mkubwa kutoka nyumbani kwao.

Si Malawi tulikokwenda kwenye kuapishwa kwa rais Chakwera. Si Zimbabwe tulikokwenda kumhani raisi wao Mugabe (rip). Si Afrika kusini tulikokwenda kumhani Mandela (rip) wala Winnie (rip). Wote hawa, hawakutuma wawakilishi wao rasmi tokea makwao kuja msibani sisi yalipotukuta.

Si Kenya tulikotuma ujumbe wetu mzito kabisa wakiwamo marais Kikwete na Mkapa (rip) kwa pamoja kuwahani kwenye msiba wa rais Moi (rip), kuwa walikuja kutuhani sisi yalipotusibu miezi michache tu baadaye.

Si Zambia, si Mozambique, si Rwanda, si Congo wala Uganda waliofika msibani.

Si nchi za Comesa, SADC, Ulaya, Marekani kaskazini wala kusini, Si Asia zikiwamo Uarabuni, Afrika wala Australia waliotukumbuka.

Hamkani si shwari tena bila ya kujali makelele yetu yote, kwa hakika hatuko vizuri. Kama waungwana tunapaswa kujiangalia. Vinginevyo makelele yetu mengi yanaweza kuwa ni kutokea kwenye madebe matupu yasiyoacha kuvuma.

Tukumbuke maneno matupu hayavunji mfupa.

Alipotutoka baba wa taifa (rip), Afrika yote hata dunia walikuwa hapa. Marais karibia wote, SADC, COMESA, ECOWAS, nk achilia mbali wawakilishi wazito wazito mabeberu walikuwa hapa kutuhani msiba ule.

Walikuwapo hapa hadi kina Madeline Albright waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Hiyo ndiyo Tanzania iliyokuwa ikisomeka vilivyo duniani kote chini ya rais Mkapa (rip).

Uzi huu kwa hakika tulipo upo, unatuhusu sana na hasa katika zama za leo:

Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Matatizo hayatanzuliwi kwa kuyakimbia, kujificha au kuyafumbia macho.

Kupafahamu wapi tulipojikwaa ni hatua njema katika kujipanga vizuri zaidi. Kujitenga au kuruhusu kutengwa kamwe hauwezi kuwa uchaguzi ulio bora.

Kujikwaa si kuanguka.

Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu.
[/QUOTE]
i
 
Mkuu asante ,tatizo kubwa linalotufanya tuchukiwe ni lipi?mbona sisi tunajishughulisha na mambo yao mf misiba kwao?kwa nini watutenge? Ukiacha kenya !; nchi nyingine zina nini nasi?
Mkuu kama taifa tunatatizo kubwa,lakini badala ya kuangalia tumeanguka wapi ili tubadirishe strategy na kusonga mbele,kazi yetu ni kunyoshea watu vidole na kuwalaum wengine hasa Kenya.
 
Mkuu kama taifa tunatatizo kubwa,lakini badala ya kuangalia tumeanguka wapi ili tubadirishe strategy na kusonga mbele,kazi yetu ni kunyoshea watu vidole na kuwalaum wengine hasa Kenya.
Kenya tumemlaumu kwa lipi? yaani yeye kumwaga mboga sisi kumwaga ugali unaita huku ni kulaumu ?
 
Ndio muhimi ni kustiri mwili wa Mtanzania mwenzetu hao wengine waje au wasije hakuna umuhimu wowote , halafu Nani kakwambia shetani anachukiwa na wote ? ndio maana nikakwambia acha mawazo mgando kijana

Mbona sisi tumekwenda kuwasitiri wao?

Kwamba shetani hachukiwi na wote?

Bila shaka anachukia na wengi kama ilivyo sisi kwa sasa.
 
Back
Top Bottom